08/06/2023
Baada ya sakata lake na klabu yake ya zamani kumalizika, Feisal Salum ametangaza kuwa pesa alizochangiwa kwa ajili ya kumsaidia kwenda kupeleka sh*taka lake CAS sasa atazigawa kwenye makundi ya watu wenye uhitaji.
Akiongea katika kituo cha Azam TV, Feisal amesema kwa kuwa hamjui kila aliyechangia na ambaye hakuchangia basi yeye pesa hizo atazipeleka kwenye vituo vya watoto yatima, msikitini na kanisani.
Baadhi ya wadau wamekuwa wakihoji kuhusu hatima ya pesa zao walizomchangia huku wangine wakiwa na imani kuwa zinaweza zikarudishwa.
Feisal Salum amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita sasa kufuatia uamuzi wake wa kuondoka katika klabu ya Yanga kukwama hati hii leo ilipotangazwa kuwa suluhu ya uhamisho wake imepatikana.
Feisal amejiunga na Azam kwa uhamisho ambazo gharama zake hazijawekwa wazi.