19/10/2025
Ameandika George Ambagile kutoka Wasafi FM radio ✍️ 🚨
-Tumezoea kuiona Simba ikitumia viungo wawili wakabaji katikati (double pivot), lakini wiki mbili zimemtosha Pantev kuamua kutumia kiungo mmoja wa ukabaji leo (single pivot) Naby Camara.
Aliamini kwenye kasi yake, uwezo wake wa kuanzisha mashambulizi kutoka chini, na wepesi wake ambao aliamini angeutumia k**a silaha kwenye kukaba. Huyu ni versatile kweli japo kwangu sioni akifanikiwa akiwa na Naby pekee.
Simba imezoea kutumia mabeki wa pembeni zaidi
Kapombe na Zimbwe zamani, kwa sasa Mligo kutengeneza mashambulizi kupitia pembeni ila leo muda mwingi timu imecheza katikati ya mistari (between the lines).
Baada ya mchezo dhidi ya Al Hilal, Dimitar Pantev alisema anataka timu yake icheze kwa kupenya kati ya mistari, kila mchezaji akiwa na uwezo wa kufanya hivyo. Aliona Simba ina aina hiyo ya wachezaji alipokutana nao kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa.
Utakuwa umeelewa kauli ya kocha mzuri anatafuta mfumo unaoendana na wachezaji waliopo kikosini
Ukisubiri mfumo wako utafutwe na wachezaji, utachelewa kujenga timu ilimkuta Fadlu.
Kwa nini Wilson Nangu leo mbele ya Chamou?
Nangu anatumia mguu wa kushoto zaidi, jambo linalomfanya yeye na Rushine wawe na uhuru , kwa kuwa wakitanua uwanja ataisaidia timu kupiga pasi haraka kila mtu akiwa upande wake.
Chamou anatumia mguu mmoja wa kulia pekee; mipira mingi alikuwa akipoteza upande wa kushoto, hata kwenye kukaba alikuwa anateseka pia.
Wilson Nangu ametoa kitu tofauti akiwa na mpira mguuni, wakati De Reuck akiwa ni pressing resistant CB anayejua kuua shinikizo la wapinzani na kucheza kwenye maeneo finyu.
Viungo wanne wa kati kwenye mfumo wa 4-1-4-1 Ahoua, Mutale, Maema, na Mpanzu wanashikiliwa na Selemani mwalimu juu, kwa nini?
Pantev alikuwa na dhamira ya kuudhibiti mchezo (control the game) kutokea juu: tupress kwa nguvu, tukae na mpira muda mwingi, na tusiwaruhusu wapinzani kufikilia kushambulia watuwaze sisi tu kwanza.
Hints kutoka kwa Pantev