23/10/2025
Dua, Ni njia ya mawasiliano kati ya mtu na Mwenyezi Mungu, Inaweza kuwa ni kwa hitajio fulani katika maisha ya Mwanadamu. Ni kiunganishi cha moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu na katika hizo dakika nne au tano za Dua mtu anaweza kuzungumza chochote. Iwe ni jambo linamtia wasiwasi, au jambo ambalo anataka kumshukuru Mwenyezi Mungu kutokana nalo.
Sasa ni nyakati gani nzuri za kuomba Dua?
1. Muda wa usiku (kuanzia baada ya Sala ya Ishaai hadi adhana ya Fajr
Aliulizwa Mtume ﷺ “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni du’a gani inayosikika?” Akasema: "Katika theluthi ya mwisho ya usiku,". Imepokewa na al-Tirmidhiy, 3499; Thuluthi ya mwisho kwa makadirio ni masaa mawili kabla ya Sala ya Fajr.
2. Siku ya Ijumaa.
Mtume ﷺ alizungumzia kuhusu siku ya Ijumaa na akasema: “Kuna saa moja siku ya Ijumaa na ikiwa Mwislamu ataipata wakati wa kuswali na akaomba kitu kutoka kwa Allaah hakika atatimiza mahitaji yake.' [Sahih al-Bukhari]
3. Mvua inaponyesha.
Kuna mambo mawili ambayo hayatakataliwa: du’a wakati wa Adhana na mvua inaponyesha.” ( Sahih na al-Albani katika Sahih al-Jami’, (3078).
4.Wakati wa Sujudu
Mtume ﷺ alisema “Mja huwa karibu zaidi na Mola wake pale anaposujudu, basi muombeni sana Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hapo. [Muslim, abu Daawuud, an-Nasa'i na wengineo, Swahiyh al-Jamiy 1175]
5. Wakati wa Kunywa Maji ya Zamzam
Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume ﷺ amesema: “Maji ya Zamzam ni kwa ajili ya yale yanayonywewa. [Ahmad 3: 357 na Ibn Majah #3062]. Maana yake ni kwamba unapokunywa maji ya Zamzam unaweza kumuomba Allah (SWT) chochote unachopenda kupata au kufaidika na maji haya k**a vile uponyaji wa maradhi.... nk.
6- Wakati wa kusikia kuwika kwa jogoo
“Mnaposikia sauti ya jogoo, basi muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake, kwani amemwona Malaika. (Imesimuliwa na al-Bukhari, 2304; Muslim, 2729)
Na Allaah Anajua Zaidi..