Audible Online TV

07/05/2026
04/05/2026

Mtoto wa makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi Taifa Stephen Wasira, Kambarage Wasira " atema yai" bungeni Dodoma akiwa anaomba kura kuwania nafasi ya kuiwakilisha Tanzania 🇹🇿 katika bunge la Afrika Mashariki

20/04/2026

Kazini kuna kazi

BUNGENI DODOMA; Waziri wa nchi ofisi ya rais (Maendeleo ya vijana) Mhe. Joel Arthur Nanauka, leo tarehe 20 April 2026. Amewasilisha mpando na makadirio ya mapato na matumizi wa wizara yake kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Jambo la kushangaza ni kwamba alionekana akiwa anachechemea huku mguu wake mmoja ukionekana na itirafu.

Imam ashour ni moja ya mchezaji aliyebarikiwa kipaji kikubwa sana cha mpira, kiasi kwamba unaweza sema kwa sasa ndio mch...
04/02/2026

Imam ashour ni moja ya mchezaji aliyebarikiwa kipaji kikubwa sana cha mpira, kiasi kwamba unaweza sema kwa sasa ndio mchezaji bora barani Africa kwa wachezaji wa ndani

K**a wasemavyo wahenga kwamba“mungu hakupi vyote” hilo limemtokea pia imam ashour 27, Raia wa taifa la Egypt mchezaji wa the lions anayekipiga katika club ya al ahly ya Misri

Uwezo wake wa kusakata kabumbu dimbani ni tofauti kabisa na matendo yake nje ya uwanja, akiwa na historia mbaya katika masuala ya nidhamu ndani ya club

Kiasi cha kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyelimwa faini kubwa zaidi katika historia ya club, EGP 1.5 million ambayo ni sawa na sh milioni 82+ za kitanzania, aliyolimwa hivi karibuni ikiambatana na kusimamishwa wiki mbili kwa kushindwa kusafiri na timu zanzibar kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa CAF dhidi ya young Africans

Ikumbukwe kuwa hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyu wa zamani wa zamalek mara kadhaa amekua akikutwa na makosa ya kinidhamu kiasi kupelekea uongozi wa club kumpa adhabu mbalimbali ikiwemo kumlima faini kwa lengo la kumkanya

Mapema Novemba 2024 kijana huyu alilimwa faini ya EGP 1 million kwa kugombana na kumtusi Mlinda mlango mkongwe na nahodha wa timu hiyo Mohammed El Shannawy katika uwanja wa mazoezi, pamoja na kugomea mchezo wa club bingwa Africa dhidi ya stade d' abidjan

October 2020, akiwa zamalek pia alisimamishwa mchezo mmoja pamoja na kupigwa faini ya EGP 50,000, kwa kosa la kugombana uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Al masry

Mwendelezo huu wa faini kwa kijana huyu sio mzuri kwa afya ya soka lake, na uongozi umekua ukifanya hivyo kwa malengo ya kumjenga kitabia

Wachezaji kadhaa akiwemo super Mario baloteli(Italy), el hajj diouf(senegal), balton (England) walishindwa kutamba katika ligi mbalimbali kwa sababu ya tabia zao tukutu.

Ukiwa k**a mdau wa soka unamshauri nini IMAM ASHOUR, nyota ya Africa inayokaribia kuzizima kwa tabia zisizorafiki mchezoni? Huku ikiaminika kuwa mpira ni mchezo wa kiungwana?

Katika hatua muhimu mnamo January 29, 2026, serikali ya kijeshi ya bukinafaso inayoongozwa na Captain Ibrahim Traore,ime...
30/01/2026

Katika hatua muhimu mnamo January 29, 2026, serikali ya kijeshi ya bukinafaso inayoongozwa na Captain Ibrahim Traore,

imetangaza rasmi kuvifuta vyama na vikundi vya siasa nchini humo, ikiambata na kufutwa kwa sheria iliyokuwa ikisimamia uendeshaji wake,

serikali iliidhinisha muswada wa kufuta sheria zilizopo za vyama vya siasa, ufadhili wa umma, na hadhi rasmi ya "Kiongozi wa Upinzani,

huku mali zote zilizokuwa zikimilikiwa na vyama hivyo zikihamishiwa serikalini,

Waziri Emile Zerbo alisema uvunjaji huo ulikuwa muhimu kwa sababu vyama "vimekengeuka" vimetoka katika misingi yao ya awali, wanachokifanya sasa ni kuchochea migawanyiko ya kitaifa, na kudhoofisha mifumo ya kijamii",

huku akisisitiza kuwa uamuzi huo unalenga kujenda umoja na mshikamono wa kweli ki taifa,

Captain Traore amekosoa hadharani muundo wa demokrasia, akisisitiza kwamba “hakuna nchi inayoweza kuendeleza chini ya mfumo wa demokrasia” na kubainisha utawala wake k**a "mapinduzi maarufu, yanayoendelea" badala ya mfumo wa kidemokrasia,

Address

Kihonda
Morogoro

Telephone

+255653402014

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Audible Online TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Audible Online TV:

Share