New_Drop_News

New_Drop_News This is the page of social, economic, political and sports news.

01/09/2023

Movie flan la mapenzi yaliyo shiba

14/07/2023
  #    Unapo yakaribia mafanikio tambua mafanikio hayo yataambatana na changamoto nyingi.    Jifunze kuzikabili changamo...
14/04/2023

#
Unapo yakaribia mafanikio tambua mafanikio hayo yataambatana na changamoto nyingi.
Jifunze kuzikabili changamoto zako,Epuka kukata tamaa kwa maana mafanikio yako yapo ndani ya izo changamoto zako unazotaka kuzikwepa šŸ™.
āœļøIbrahim haule

Naitwa sanze nna miaka 14,ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wawili,Mdogo wangu anaitwa Simoe ana miaka 11.Ni w...
13/07/2021

Naitwa sanze nna miaka 14,ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wawili,Mdogo wangu anaitwa Simoe ana miaka 11.Ni watoto wapekee katika familia ya Mzee samson.

Baba yetu ni fundi ujenzi,Mzee ambaye anajitahidi kutafuta pesa ili zikaishie kwenye ulevi,Baba ambaye hatujali kwa chakula wala mavazi.Nguvu kubwa ya malezi yetu ilikuwa inatoka kwa Mama,
Mama ambaye ni mlemavu wa mguu na alitumia muda mwingi kukaa chini kwa ajiri ya kuponda kokoto ili tuweze kujipatia kipato kwaajiri ya kukidhi mahitaji madogo madogo.

Mama alilazimika kujiongeza katika utafutaji na akabuni biashara ya mboga mboga za majani,Biashara ambayo mimi na mdogo wangu Tuliitembeza mtaa kwa mtaa uku tukiwa tumeibeba katika mabeseni kwaajiri ya kutafuta wateja.
Safari ya maisha yetu ilikua ni ngumu sana hasa ukizingatia umri wetu ulikua ni mdogo sana ,Tulipaswa kuwa shuleni ila shida zimelazimisha tuwe mtaani na Watu wanao tuzunguka wametupa jina (Chokolaa).
Maisha yalizidi kusonga mbele Mama hakujali ulemavu wake alizidi kupambana kwaajiri yetu na kauli yake kubwa aliyokua akituambia ni kuwa '"siku moja tutasoma" ,Kauli hii ilitupa sana Imani lakini siku zilikua zinazidi kwenda ,Umri unazidi kwenda na kauli ya mama haitimii.

Siku moja baba aliludishwa nyumbani akiwa amebebwa na watu walio dai kuwa wamemuokota njiani huku akitwokwa na mapovu mdomoni..........

Itaendeleaaaaaa

Dodoma
03/07/2021

Dodoma

28/02/2020

Flamingo Hotel ni hotel mpya iliyopo morogoro Maeneo ya msamvu inatafuta wafanyakazi wa usafi katika vyumba vya kulala wageni.sifa,unatakiwa uwe umepitia mafunzo maalum ya hotelia katika chuo kinachotambulika.

We are on air....
16/10/2019

We are on air....

TAFITI: DAR kinara mikoa mitano Tanzania yenye watu wengi wenye magonjwa ya akiliMkoa wa Dar es salaam umetajwa kuongoza...
10/10/2019

TAFITI: DAR kinara mikoa mitano Tanzania yenye watu wengi wenye magonjwa ya akili

Mkoa wa Dar es salaam umetajwa kuongoza kuwa na watu wengi wenye magonjwa ya akili ikiwa mbele ya mikoa mitano yenye watu wengi wenye magonjwa ya akili Tanzania.

Imeelezwa kuwa sababu za kimazingira ikiwemo ugumu wa maisha na matumizi ya vilevi, Ndio chanzo kikubwa cha tatizo hilo mijini kuliko vijijini.

Akizungumza na gazeti la Nipashe jana Oktoba 9, 2019, Daktari wa Afya ya Akili katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Omary Ububuyu, Amesema takwimu zilizopo kwa miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2018 zinaonyesha magonjwa ya akili yameongezeka kutoka 301,000 hadi 356,000.

ā€œKwa mwaka 2016 kulikuwa na wagonjwa 301,000 wanahusisha na magonjwa ya akili, kifafa na matumizi ya kilevi,ā€ alisema wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani leo.
Ameeleza kuwa magonjwa ya kifafa kwa ujumla wake baadhi yametibiwa kwenye idara ya magonjwa ya akili na mengine nje ya idara ambapo yana takribani asilimia 50 ya wagonjwa wote. ā€œSasa magonjwa haya matatu katika takwimu za Wizara ya Afya na Tamisemi zinaonyesha katika vituo vya afya takribani wagonjwa 356,000 kwa mwaka 2018, pia asilimia 50 ya magonjwa ni ya akili na nyingine ni kifafa,ā€ alisema na kuongeza:
ā€œHii ni kwa hospitali ya mkoa na vituo vya afya, hapa hatujahusisha takwimu kutoka hospitali k**a Muhimbili na Mirembe na hospitali zingine kubwa.ā€œ.

Akitaja mikoa inayoongoza, Dkt. Ububuyu Dk. Ububuyu amesema mijini kuna wagonjwa wengi zaidi ambapo takwimu hizo zinaonyesha Dar es Salaam inaongoza kuwa na wagonjwa asilimia 20 bila kujumuisha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
ā€œMkoa mwingine ni Kilimanjaro, Tanga, Morogoro na Mwanza, yote mitano ipo juu na hali hii hapo katika magonjwa ya akili peke yake hata magonjwa yasiyo ya kuambukiza hali ipo hivyo hivyo.ā€œamesema Dkt. Ububuyu.
ā€œDar es Salaam inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza halafu mikoa mingine inafuata, Dar es Salaam ina asilimia 20, Kilimanjaro 9, na mingine asilimia 7 hadi 5. Mikoa yenye wagonjwa kidogo ni Katavi 0.1, Rukwa 4, Songwe pia ina asilimia chache ya wagonjwa,ā€ amesema Dkt. Ububuyu.

Hata hivyo, alisema hali za kimazingira na vilevi ndizo zinazochangia zaidi kuliko viashiria vya kibaiolojia kwenye maeneo ya mijini kuliko vijijini.

ā€œKuna vihatarishi vinavyosababisha magonjwa ya akili ambapo kikubwa namba moja ni vinasaba, vitu vya kibaiolojia kuna kupata majeraha ambayo yanaathiri ubongo, baadhi ya magonjwa yanayopanda kichwani ikiwamo malaria, HIV. ā€œPia matumizi ya vilevi k**a pombe, bangi, sigara na vilevi vingine kwa kuwa vilevi kazi yake kubwa ni kushusha uwezo wa ubongo kufanya kazi na mambo yaliyokuwa yakitarajiwa,ā€amesema Dkt. Ububuyu.

Mtaalamu huyo alisema: ā€œUtakuta vilevi vingi vinaweza kuwa vihatarishi, unaweza ukatumia bangi ukaumwa, pia hali ya kijamii yaani ya kiuchumi ikiwamo ugumu wa maisha yaani kuwa na hali ngumu kupita kiasi ambayo mtu hawezi kuimudu k**a kufiwa mtu akashindwa kustahimilivu maumivu ya kupoteza kitu anachokipenda k**a kazi, mwenza, rafiki au ndugu.

Ibrahim haule

05/10/2019

RAIS MAGUFULI AMPONGEZA RC MBEYA KWA KUWACHAPA VIBOKO WANAFUNZI

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kwa kuwachapa viboko wanafunzi wa shule ya sekondari Kiwanja wilayani Chunya kwa madai ya kuchoma mabweni ya shule.

Tiwa Savage afunguka mahusiano yake na Wizkid ā€œNipo single, Hakuna hata mtu anayenitafuta DM’Ibrahim hauleMsanii maarufu...
05/10/2019

Tiwa Savage afunguka mahusiano yake na Wizkid ā€œNipo single, Hakuna hata mtu anayenitafuta DM’

Ibrahim haule

Msanii maarufu wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage amefunguka kuwa kwasasa bado yupo single hajapata mwanaume wa kuishi naye tangu aachane na mumewe, Tee Billz mwaka 2016.

Akihojiwa jana asubuhi na kituo cha radio cha The Beat 99.9 cha Jijini Lagos, Nigeria. Tiwa Savage amesema hajawahi kuwa kwenye mapenzi na mwanaume yeyote tangu aachane na mumewe na wanaume wote anaoonekana nao ni marafiki wa kibiashara tu.
Kuhusu tetesi za kuwa anatoka kimapenzi na Wizkid, Tiwa amesema kuwa ā€˜Mimi na Wizkid ni marafiki wa kibiashara tuā€, Na akaendelea kujibu kuhusu mustakabali wa mahusiano yake mapya kwa sasa.
ā€œBado nipo single kwasasa na hakuna hata mwanaume anayenitafuta DMā€œ, amefunguka mrembo Tiwa Savage na kukazia kuwa kwasasa yupo bize na kazi yake ya muziki.

SOMA ZAIDI KISA CHA TIWA SAVAGE KUACHANA NA MUMEWE MWAKA 2016.

Mwaka 2016 kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote pale alipolazwa hospitali nchini Jamaica alikoenda kufanya video na Busy Signal.
Anasema wakati anajiandaa kwenda kushoot, alianza kutoka damu nyingi ukeni kiasi cha kupoteza fahamu. Alimpigia simu na kumtumia ujumbe mumewe ikiwa pamoja na kumtumia picha akiwa hoi kitandani lakini hakujibiwa hadi anatoka hospitali.

Siku amerejea Nigeria na akiwa amelala usiku wa saa nane, simu ya mumewe iliita kwa namba iliyohifadhiwa kwa jina la biashara lakini alishangaa iweje kampuni impigie usiku huo. Anadai alichukua simu ya mumewe na kuanza kusoma ujumbe wa WhatsApp na ndipo alipogundua kuwa huyo alikuwa ni mwanamke na maongezi yao yalionesha kuwa walikutana hotelini na kufanya mapenzi. Kutokana na kitendo hicho aliondoka na kwenda kwa rafiki yake.

Anadai kuwa amekuwa akificha kwa muda mrefu kuhusu mume wake, lakini amedai tangu mtoto wao azaliwa, hajawahi kutumia hata senti kwaajili ya familia yao kwamba Tiwa ndiye kila kitu.
Amesimulia pia jinsi ambavyo mume wake amekuwa na tabia ya kumzunguka kwenye malipo ya show zake ambapo ametolea mfano wa harusi aliyotakiwa kwenda kutumbuiza London. Anasema alibaini kuwa mumewe alilipwa gharama zote lakini hadi anaenda kutumbuiza alimueleza kuwa hakuwa amelipwa. Kwakuwa alikuwa anafahamiana na miongoni mwa waandaji wa harusi hiyo alimuuliza na kujibiwa kuwa walikuwa wameshamlipa mume wake hela yote, miezi minne nyuma.

ā€œUnamuibia mke wako, na yeye haoni k**a ameniibia mimi, kwahiyo ilibidi nitumbuize kwenye harusi bure, kwasababu alikuwa ameshatapeli hela na sijui alizifanyia nini,ā€ anasimulia.
Kwa upande mwingine staa huyo alieleza jinsi ambavyo mume wake alikuwa akiishia maisha ya zaidi ya kipato chake na hivyo wakati mwingine kumfanya ajikute kwenye madeni makubwa ambayo alilazimika kuyalipa.

Tiwa alisema jambo ambalo mume wake alizingua zaidi na ambalo limesababisha mgogoro wao ni pale alikopa naira milioni 45 ambazo ni sawa na shilingi milioni 495 za Kitanzania na kuchikichia. Kwa hali hiyo Tiwa alianza kuhofia usalama wake kwamba wanaomdai mumewe wangeweza hata kumdhuru ama kumteka yeye na mwanae kwasababu ya deni hilo.

Pia Tiwa amezungumzia jinsi ambavyo aligundua mume wake anatumia co***ne kitu ambacho kilimuumiza sana.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alikanusha kwa msisitizo kuwa hajawahi kamwe kumsaliti mume wake na Don Jazzy, Dr Sid wala 2Face na kwamba yupo tayari hata kuwekewa kifaa cha kubaini k**a anasema uongo.

Mh Ally happy akitembelea ukaguzi wa nyumba  za polisi kwa awamu ya kwanza itakayochukua familia sita pindi utakapo kami...
08/06/2019

Mh Ally happy akitembelea ukaguzi wa nyumba za polisi kwa awamu ya kwanza itakayochukua familia sita pindi utakapo kamilika Ujenzi uo

Address

Mafisa
Morogoro

Telephone

+255745414730

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when New_Drop_News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to New_Drop_News:

Share