
22/06/2024
Esther wa UMISSETA na mwandishi wa TBC
Esther Seme ni mmoja wa wanafunzi wanaoonyesha vipaji katika mashindano ya Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yanayoendelea mkoani Tabora, yakizikutanisha timu kutoka mikoa 28 nchini.
Esther mwenye umri wa miaka 14, ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Kutwa Mbeya na anashiriki mchezo wa netiboli katika mashindano hayo.
Mwanafunzi Esther ana urefu wa futi 6.3 akiwa ni mwanafunzi wa netiboli mrefu zaidi katika mashindano hayo ya UMISSETA kwa mwaka huu.
Picha: Ni mwanafunzi Esther akifanya mahojiano na mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Steven Kigora.