Mwambani LEO

Mwambani LEO Kwa story mbali mbali kutoka ndani na nje ya tanzania ungana na .COM kwa info zitakazo kuhabarisha wakati wote mahala popote.

21/07/2016

Ikiwa leo ni july 21 ,2016, bado matukio ya ajari yanaendelea katika manispaa na mkoa wa morogoro baada ya leo hii boda boda kugonga wanafunzi wakiwa wamepakiana katika baiskeli.
Tukio hilo lmetokea katika maeneo ya njiapanda ya hotel ya B-Z iliyopo maeneo ya oilcom wakati wanafunzi hao wakitoka shuleni na kuelekea nyumban kwao.
Aidha katika ajali hiyo hakuna alyepoteza maisha ila wote wakiwa wameumia katika miguu yao.
Katika maeneo hayo hayo ya kituo cha oilcom jana gari zagongana uso kwa uso na kusababisha kuwaka moto zikiwa babarani.
Chanzo cha ajali hiyo ni baada ya gari la kubebea maji mtaan kutoshika breki na kuingia katika semi iliyobeba mbao.
Hata hivyo hakuna aliyepoteza maisha katika tukio hilo.!!!

19/07/2016

BREAK NEWZZZ!!! Muda si mrefu moto mkubwa walipuka katika kiwanda cha utengezenezaji wa nguo mkoani morogoro polista.
Chanzo cha tukio hilo kwa mujibu wa shuhuda wetu kwamba ni shoti iliyotokea kwenye mashine katika kitengo cha ukaguzi(inspection).
Mpaka sasa hakuna taarifa za mtu yeyote aliyejeruhiwa katika tukio hilo

11/07/2016

Asante sana kwa wote wanaeondelea ku like,endelea kushare na washkaji ili nao waweze kulike zaid na hivi karibuni page itakwenda kufanyiwa marekebisho so don go any where

04/07/2016

Hellow guyz

01/07/2016

Hellow guys nmewamic sana !! Lakn bado npo ,ila msijili leo nataka kuwapa taarifa kuwa hivi karibuni jina la page litafanyiwa mabolesho na kuanza kukujuza vyema kabisa katka habari na burudan

14/01/2016

Asante sana na hizo ndio story zote ambazo utapata kuzisikia kwa siku ya leo ,hivyo basi endelea kushare na washkaji nao waweze ku like zaidi ili wapate story mbali mbali kila siku ...................have a nice day

Liberia yatangazwa kuwa isiyo na Ebola    http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015...
14/01/2016

Liberia yatangazwa kuwa isiyo na Ebola

http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/12/22/151222151718_last_ebola_patient_guinea_624x351_getty_nocredit.jpg

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kumalizika kwa ugonja wa ebola nchini Liberia na kusema kuwa maambukizi yote ya ugonjwa huo yamemaliziwa katika eneo la Afrika Magharibi.

Lakini WHO inasema kuwa bado kazi haijamalizika. Visa zaidi vinatarajiwa na ufuatiliaji wa hali ya juu utakuwa mkubwa miezi inayokuja.

Liberia ilitangazwa kwanza kuwa isiyo na ugonjwa wa ebola mwezi Mei mwaka 2015 lakini ugonjwa huo ukalipuka tena mara mbili ambapo kisa cha mwisho kiliripotiwa mwezi Novemba mwaka 2015.http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/17/151117081253_ebola_guinea_624x351_getty_nocredit.jpg
Image copyright Getty
Image caption Hata hivyo umoja wa mataia umeonya kuwa eneo la afrika magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa wa ebola

Tangazo la leo linatolewa baada ya siku 42 tangu mgonjwa wa mwisho kutopatikana na virusi vya ebola.

Liberia inajiunga na Guinea pamoja na Sierra Leone ambazo zilipata kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo mwaka uliopita.

Licha ya hilo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, ameonya kuwa eneo la Afrika Magharibi huenda litashuhudia visa vya ungowa huo. Ebola umewaua zaidi ya watu 11,000 tangu mwezi Disemba mwaka 2013 .

Bei ya mafuta soko la kimataifa yashukahttp://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/02...
14/01/2016

Bei ya mafuta soko la kimataifa yashuka
http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/02/03/150203165218_us_oil_well_624x351_getty_nocredit.jpg


Mshirikishe mwenzako
Image copyright Getty
Image caption Visima vya mafuta

Bei ya mafuta katika soko la kimataifa imeendelea kushuka hadi kiwango cha chini kabisa ndani ya miaka 20 hadi sasa.

Kushuka kwa bei hiyo ya mafuta kimataifa kufikia kiwango cha chini ya dola 30 kwa p**a inatajwa kuwa ni matokeo ya kuongezeka kwa hifadhi ya mafuta nchini Marekani.

Kumekuwa na mtikisiko katika bei ya mafuta Duniani tangu mwaka 2014 ambapo matokeo yake ni kuongezeka kwa uzalishaji wa mafuta nchini Marekani na kupungua kwa uhitaji nchini China.

Hata hivyo wataalamu wa uchumi wanasema kuwa China umeingia katika uhitaji mdogo wa mafuta kutokana na kudorola kwa ukuaji wa uchumi wa taifa hilo.

Taarifa za kushuka kwa kasighafla kwa bei ya mafuta kimataifa kumesababisha kushuka kwa mauzo ya siku katika masoko makuu matatu ya hisa kwaununuzi kwa Zaidi ya asilimia mbili

Miripuko ya bomu yatikisa Jakarta, saba wauawa http://media.ws.irib.ir/image/4bk19b3e44e3582jh9_620C350.jpgMiripuko ya b...
14/01/2016

Miripuko ya bomu yatikisa Jakarta, saba wauawa


http://media.ws.irib.ir/image/4bk19b3e44e3582jh9_620C350.jpg
Miripuko ya bomu yatikisa Jakarta, saba wauawa
Kwa akali watu saba wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya miripuko ya mabomu kuutikisa mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Msemaji wa Polisi Anton Charliyan amesema miongoni mwa waliopoteza maisha katika hujuma hiyo ni raia watatu na afisa wa polisi. Rais wa nchi hiyo, Joko Widodo ameitaja miripuko hiyo k**a shambulio la ugaidi na kuagiza wahusika kusakwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa polisi ya Indonesia, miripuko hiyo imetokea nje ya jengo moja la kibiashara linaloitwa Sarinah Mall katika kitovu cha Jakarta. Kadhalika milio ya risasi imesikika katika eneo hilo, muda mfupi baada ya miripuko hiyo.

Habari zaidi zinasema kuwa, eneo hilo lenye shughuli nyingi lina mahoteli ya kifahari, balozi na afisi nyingi za serikali na za binafsi.

Itakumbukwa kuwa, watu 202 waliuawa katika shambulio kubwa la ugaidi lililowahi kuikumba nchi hiyo mwaka 2002 katika eneo la Bali.

Wednesday, January 14, 2016Pato la Taifa laendelea kukuahttp://2.bp.blogspot.com/-QSaTrTUnDYI/VpaH593vNsI/AAAAAAAAu8s/7B...
14/01/2016

Wednesday, January 14, 2016

Pato la Taifa laendelea kukua

http://2.bp.blogspot.com/-QSaTrTUnDYI/VpaH593vNsI/AAAAAAAAu8s/7BvFAPnH0T0/s1600/1.jpg

Pato la Taifa katika kipindi cha Robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.4 katika kipindi cha mwaka 2014.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Albina amesema kuwa kutokana na ongezeko hilo Serikali imeendelea kutoa huduma za kijamii zikiwemo umeme, afya na maji.

“ Pato la Taifa kwa robo tatu ya mwaka 2015 limeendelea kukua kwa kasi ya asilimia 6.3 ukilinganisha na asilimia 5.4 katika robo tatu ya mwaka 2014” Alisema Dkt. Albina.

Dkt. Albina ameongeza kuwa kuongezeka kwa Pato la Taifa kumeenda sanjari na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa na huduma nje ya nchi kwa takribani asilimia 3.3 ambapo bidhaa na huduma zilizochangia ongezeko hilo ni pamoja na dhahabu, Almasi, madini mengine na Utalii.

Aliongeza kuwa utangazwaji wa Takwimu za Pato la Taifa unazingatia matakwa ya Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inayotoa mamlaka kwa Tume ya Taifa ya Takwimu kukusanya, kuchambua na kutangaza takwimu za Pato la Taifa.

Aidha alitaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi kubwa katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2015 kuwa ni pamoja na Ujenzi (17.6%), Uchukuzi na Uhifadhi (10.6%), Uendeshaji Serikali na Ulinzi (10.6%) na Uchimbaji Madini na Kokoto (8.0%)

Dkt. Albina amesema kuwa jumla ya thamani ya Pato la Taifa kwa bei za miaka husika katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba 2015 ni takribani shilingi tilioni 71.7 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 6.9.

Thursday, January 14, 2016Waziri Lukuvi Atoa siku 18 jengo la Ghorofa 16 Livunjwe D’salaamhttp://2.bp.blogspot.com/-ugwG...
14/01/2016

Thursday, January 14, 2016
Waziri Lukuvi Atoa siku 18 jengo la Ghorofa 16 Livunjwe D’salaam

http://2.bp.blogspot.com/-ugwG85-F1NQ/VpdADHF6AsI/AAAAAAAAu-0/TZu59r5roro/s1600/1.jpg
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi kabla halijaleta maafa.

Akizungumza jana katika jengo hilo, Lukuvi alisema anashangaa hadi sasa kazi ya kuvunja jengo hilo haijaanza licha ya manispaa kuelekezwa kulivunja.

Uamuzi wa Serikali kulivunja ulikuja baada kuporomoka kwa jengo katika mtaa huo lililosababisha vifo vya watu 37 na wengine 18 kujeruhiwa mwaka 2013.

“Ni aibu, manispaa mnataka jengo hilo liporomoke na kuua watu tena! Tutachekwa kwa uzembe k**a ikitokea tena ajali,” alisema.

Lukuvi alisema kuanzia Februari Mosi uvunjaji wa jengo hilo unatakiwa kuanza vinginevyo wahusika wajiandae kuchukuliwa hatua.

“Nataka nikipita hapa siku yoyote kuanzia mwezi ujao nikute mkandarasi anabomoa jengo hili vinginevyo hatutaelewana,” alisema.

“Hili ni eneo hatarishi hata tuliosimama hapa hatari yoyote inaweza kutukuta lakini Manispaa ya Ilala haioni kwamba hapa kuna tatizo,” alisema.

Waziri alisema uvunjaji wa jengo hilo utakapoanza, wananchi wanaoishi jirani watatakiwa kuhama kwa muda kwa tahadhari.

“Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakianza kuvunja jengo hilo tafadhali waondoeni wakazi wote kwa sababu eneo hili litakuwa hatarishi,” alisema.

Jengo hilo linamilikiwa kwa pamoja kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Ali Raza Investment.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngulumi alisema kilichochelewesha ni makandarasi walioshinda zabuni hiyo kujitoa katika hatua za mwisho wakitoa sababu mbalimbali.

Alisema hivi sasa amepatikana mkandarasi Patty Interplan ambaye yuko katika hatua za mwisho za kupewa kazi hiyo.

“Tutaanza kazi k**a ulivyoelekeza,” alisema Mngulumi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, alisema atatoa ushirikiano kwa manispaa hiyo ili kuhakikisha jengo hilo linabomolewa.

14/01/2016

Habari za asubuhi wana Mwambani LEO ,leo ni siku bora kabisa tukiwa tunaelekea kumaliza week na kuelekea weekend,story mbali mbali zinazogonga vichwa vya watu wengi na leo nimekuwekea lakini pia usisahau kushare na washkaji mbali mbali waendelee kulike page ili waweze kuzipata wenyewe daily.
na kati ya story nlizokuandalia leo ni pamoja na ..........

Thursday, January 14, 2016

Maalim Seif Sharif Hamad Amwandikia Barua Papa Francis Kumwomba Aingilie Kati Mzozo wa Zazibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, amemwangukia Papa Francis kwa kumwandikia barua, akimuomba kutumia ushawishi wake na Tanzania kumaliza mzozo wa kisiasa kisiwani humo kabla hali haijawa mbaya.

Kwa mujibu wa barua yake ya Novemba 25, mwaka jana, Maalim Seif alimwomba Papa kutumia ushawishi alionao kwa serikali ya Tanzania ili kuhakikisha haki inatendeka na kuepusha vurugu zinazoweza kutokea.

“Ni wiki tatu sasa tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu na hali hii imesababisha kusimama kwa baadhi ya shughuli za kuichumi kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu kuhusu mustakabali wa hali hii….watu wanashindwa kujua nini kitatokea maana wana hofu kwamba hali hii inaweza kuharibu umoja wa kitaifa kwa watu kuishi kwa upendo bila kujali dini wala kabila,” ilisema barua hiyo.

Barua hiyo ya Maalim Seif ilisema, Zanzibar ina mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo, hivyo hakuna mgawanyiko kwa misingi ya udini lakini hatua ya wananchi kukosa haki yao ya kidemokrasia kupitia sanduku la kura baada ya miaka 20 ya chaguzi visiwani humo kunaweza kusababisha vijana ambao hawafurahishwi na mwenendo huo kutumia njia mbaya kutafuta haki yao.

“Badala ya kuchukua hatua za pamoja kuzuia uovu huu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo chama chake kilishinda kwenye uchaguzi mkuu uliopita, imekuwa ikisaidia serikali ya Zanzibar kwa kutumia askari na majeshi yake kutishia watu wa upinzani,” ilisema.

“Wakati mmishenari wa kikristu alipomuomba Sultan wa Zanzibar mwaka 1840 kibali cha kujenga asasi ya kusaidia jamii kwenye eneo lake, Sultani yule ambaye alikuwa Muislamu alimtambua k**a mtumishi wa Mungu aliyekuwa na lengo la kuendeleza neno la Mungu” ilisema sehemu ya barua hiyo kwenda kwa Papa.

Iliongeza kuwa, Zanzibar ilipopata Uhuru wake mwaka 1963, kwa kiwango kikubwa watu wake waliishi kwa amani na ushirikiano baina ya watu wa madhehebu yote ya Katoliki, Anglikana, Sunni, Shia na Hindu na hakukuwahi kuwa na mgogoro wala hofu ya watu hao kuhitilafiana kwa misingi ya tofauti ya dini.

Ilisema Chama cha Wananchi CUF kimekuwa kikishinda chaguzi zote tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, lakini haijawahi kupewa ushindi wake hata muhula mmoja.http://3.bp.blogspot.com/-uT4Bjg5fUbI/VpdD8ilr0xI/AAAAAAAAu_c/ld1LvmyAFLs/s1600/1.jpg

Address

Morogoro

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mwambani LEO posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category