Kilimanjaro Revival Fm

Kilimanjaro Revival Fm Most Credible Christian Radio broadcast from Moshi-Kilimanjaro."Power Of Revival"

17/10/2025

Watu walimkubali Raila Odinga kwa sababu alitembea pamoja nao katika safari ya matumaini na changamoto. Alijua namna ya kugusa hisia za wananchi — kwa maneno, kwa vitendo, na kwa upendo wa kweli kwa taifa lake.

Raila hakuwa kiongozi wa mbali; alikuwa miongoni mwao, akiishi maisha ya kawaida, akilia na wenye huzuni na kucheka na wenye furaha.

Alipokuwa akizungumza, watu walihisi nguvu ya ukweli. Alipokuwa akisimama jukwaani, aliamsha imani iliyoonekana kufa. Alikuwa kiongozi aliyegusa roho — mtu ambaye alibeba maumivu ya wanyonge k**a yake binafsi. Kwa hiyo, wananchi walimkubali si kwa sababu ya siasa, bali kwa sababu ya utu wake.

Cc

17/10/2025

VIDEO: Rais wa Kenya William Ruto ameongoza Viongozi wa kiserikali pamoja na wageni kutoka Mataifa mbalimbali Afrika na Duniani kuaga mwili wa Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambapo mapema asubuhi ya leo shughuli za kuaga mwili zimefanyika katika viwanja vya Bunge.

Mwili wa Raila Odinga ulilazwa nje ya viwanja vya Bunge ambapo Viongozi wa Kiserikali wamepata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kitaifa na kisha kupelekwa katika Uwanja wa Nyayo kwa ajili ya ibada ya mazishi ya kitaifa.

Aidha Kaka wa Marehemu Dkt. Oburu Oginga ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa k**ati ya mazishi jana Alhamisi alisema kuwa Raila Odinga atazikwa katika Jumapili katika hafla ya faragha itakayohudhuriwa na watu wachache walioteuliwa pekee.

16/10/2025

Watu wasiopungua wawili wameuawa kwa risasi jijini Nairobi baada ya vikosi vya usalama vya Kenya kufyatua risasi hewani katika jitihada za kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika katika uwanja mmoja kwa ajili ya kutazama mwili wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.

Taarifa kutoka chanzo cha polisi na vyombo vya habari vya ndani zinasema vurugu hizo zilianza baada ya umati mkubwa wa watu kujitokeza kwenye uwanja huo, ambapo mwili wa Odinga ulipelekwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.

16/10/2025

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeutaarifu Umma wa Watanzania kuwa linaendelea kufuatilia kwa karibu na kutathmini hali ya Ulinzi na Usalama nchini katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika tarehe 28 na 29 Oktoba, 2025 k**a ilivyotangazwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa ujumla JWTZ linaridhishwa na hali ya usalama iliyopo nchini katika kipindi hiki ambacho Vyama vya Siasa vinaendesha kampeni zao kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, kuheshimiana na kuvumiliana kunakooneshwa kupitia kwa wagombea wao wa ngazi za Urais, Ubunge na Udiwani. Jeshi linaviomba vyama vya siasa kuendeleza hali ya amani na utulivu wakati wote wa kampeni zinazoendelea kote nchini.

Katika hatua nyingine, JWTZ linalipongeza Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Usalama kwa jinsi vinavyoendelea kusimamia hali ya usalama katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Pamoja na hali ya amani na utulivu iliyopo, kumejitokeza baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati kutoka ndani na nje ya nchi kutumia mitandao ya kijamii kupotosha umma kwa kuweka maudhui yenye lengo la kuleta uchochezi kwa kulihusisha Jeshi na siasa kwa lengo la kuwafanya wananchi kukosa Imani na Jeshi lao.

Jeshi linauomba Umma wa watanzania kupuuza machapisho/taarifa ambazo zimekua zikionekana kwenye mitandao ya kijamii. Wananchi wanakumbushwa kuwa taarifa zote zinazolihusu Jeshi zitatolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi.

16/10/2025

Chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kimemteua Seneta wa Siaya, Dkt. Oburu Oginga, kuwa Kaimu Kiongozi wa Chama kufuatia kifo cha aliyekuwa kiongozi wake wa muda mrefu, Raila Amolo Odinga.

Uteuzi huo ulifanyika Alhamisi, Oktoba 16, 2025, katika kikao maalum cha Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) ya ODM kilichofanyika jijini Nairobi, ambapo viongozi wa chama walikubaliana kwa kauli moja kumpa Oburu jukumu hilo kwa muda.

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa chama hicho, Edwin Sifuna, alisema uteuzi wa Dkt. Oburu Oginga unalenga kuhakikisha kuwa shughuli za chama zinaendelea kwa utulivu wakati taifa bado linaomboleza kifo cha Raila Odinga.

“Tumeamua kumteua Dkt. Oburu Oginga kuwa kaimu kiongozi wa chama ili kuhakikisha uongozi wa ODM haukwami. Ni hatua ya mpito hadi tutakapoamua rasmi kuhusu urithi wa uongozi wa kudumu,” alisema Sifuna.

Dkt. Oburu Oginga ni kaka yake marehemu Raila Odinga na mwana wa mwanzilishi wa kisiasa mashuhuri, hayati Jaramogi Oginga Odinga, ambaye pia alikuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Kenya.

Oburu, ambaye alizaliwa mwaka 1943, amehudumu katika siasa za Kenya kwa miongo kadhaa. Amewahi kuwa Mbunge wa Bondo, Naibu Waziri wa Fedha, Mwakilishi wa Kenya katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), na kwa sasa ni Seneta wa Kaunti ya Siaya.

16/10/2025

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali pingamizi lililokuwa limewasilishwa na Jamhuri katika kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Malawi na Cuba Humphrey Polepole dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake .

Katika shauri hilo, ambalo limefunguliwa na Wakili wa familia ya Polepole, Peter Kibatala kwa hati ya 'dharura sana', upande wa Jamhuri uliwasilisha pingamizi ukiomba kuwafanyia maswali ya dodoso (cross examination)

'k**a mashahidi' watu wawili (Peter Kibatala na Godfrey Polepole) kutoka upande wa mleta maombi ambao wamewasilisha viapo Mahak**ani hapo Kupitia pingamizi hilo lililokuwa limewasilishwa na kusikilizwa jana, Jumatano ya Oktoba 15.2025 Jamhuri iliieleza Mahak**a kuwa kupitia viapo vya watu hao vilivyowasilishwa Mahak**ani, ambapo baada ya kuvipitia wanaamini endapo wangewafanyia maswali ya dodoso, ingesaidia Mahak**a kufikia uamuzi wake kuhusiana na kesi iliyoko Mahak**ani hapo

Kesi hiyo inayohusu kutoweka katika mazingira tatanishi kwa Humphrey Polepole, hata hivyo pingamizi hilo lilipingwa vikali na Wakili Peter Kibatala na hivyo kuiomba Mahak**a kutupilia mbali Katika maamuzi yake muda mfupi uliopita leo, Alhamisi Oktoba 16.2025, Jaji Mfawidhi wa Mahak**a Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo ametupilia mbali pingamizi hilo, na sasa Mahak**a imeanza kusikiliza kesi ya msingi iliyowasilishwa Mahak**ani hapo.

16/10/2025

Ndege ya Shirika la Ndege la Kenya RAO01 iliyobeba mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Marehemu Raila Amolo Odinga tayari imewasili kenya ambapo imetua salama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Mazishi ya Raila Odinga ambaye alifariki dunia Oktoba 15, 2025 wakati akipatiwa Matibabu nchini India

15/10/2025

Jeshi la Polisi nchini limesema litaendelea kufuatilia kwa kina, kuzuia, kubaini na kutanzua matishio ya Usalama siku ya Oktoba 29, huku likitoa rai kwa Wananchi kujitokeza kushiriki ili kutimiza haki na wajibu wao wa Kikatiba bila ya kuwa na hofu yoyote.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 15, 2025 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro.

15/10/2025

VIDEO: Mamia ya wakenya wamejitokeza Kuomboleza Kifo cha Raila Odinga

𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐔𝐅𝐔𝐀𝐓𝐈𝐋𝐈𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐊𝐀 𝐌𝐈𝐓𝐀𝐍𝐃𝐀𝐎 𝐘𝐄𝐓𝐔 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐀𝐌𝐈𝐈

@ Kilimanjaro revival fm
Kilimanjaro Revival Tv

Usikose kufuatilia Kipindi cha Gospel Revibal Hub Kupitia 95.9 Kilimanjaro Revival Fm HOST  GUEST
15/10/2025

Usikose kufuatilia Kipindi cha Gospel Revibal Hub Kupitia 95.9 Kilimanjaro Revival Fm

HOST
GUEST

Address

Moshi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kilimanjaro Revival Fm posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kilimanjaro Revival Fm:

Share