19/09/2024
TULIA TRUST UYOLE CUP 2024 YATIKISA MBEYA NA VIUNGA VYAKE!
Taasisi kubwa ya TULIA TRUST Jana imehitimisha ligi yake ya TULIA TRUST UYOLE CUP 2024 na kutoa Kombe kwa washindi Ambapo mgeni rasmi Mh Khamis MWINJUMA naibu Waziri wa tamaduni, Sanaa na Michezo, amekabidhi zawadi kwa;
* mshindi wa kwanza (Benja FC) - tsh Milion 5,
* mshindi wa pili (Mbeya Smart) - Milioni 3,
* mshindi wa Tatu (Rojas FC) -Milioni 2,
* mshindi wa nne (Chipukizi FC) - Milioni 1.
Zawadi Nyingine zilizotolewa ni Pamoja na Mchezaji Bora, Kipa Bora, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu Wakipata Shilingi Laki Moja (Tsh.100,000/=) kila Mmoja na Kikundi Bora cha Ushangiliaji Kikizawadiwa Shilingi Laki Tatu (Tsh.300,000/=)