Tiba Facts

Tiba  Facts Katika ukurasa huu utajifunza namna mbalimbali ya kujitibu kupitia Qur'an,mimea na matunda ukiwa nyumbani.

ELIMU YA NYOTA.10.NYOTA YA MBUZI.                Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu...
24/10/2025

ELIMU YA NYOTA.
10.NYOTA YA MBUZI.


Hii ni nyota ya kumi katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 21 Disemba na 19 Januari au wenye majina yalio anza na herufi J au V au K.

Asili yao ni Udongo.Siku yao ya bahati ni Jumamosi. Namba yao ya bahati ni 8
Sayari yao ni Saturn (Zohal).

Malaika wake anaitwa Kafyaeel, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa, Abuu Nuhu.

Rangi zao za bahati ni Nyeusi na Bluu iliyoiva. Wenye nyota hii wanashauriwa wapake rangi zifuatazo kwenye nyumba zao, rangi ya Kahawia (Brown) Rangi ya Kijivu (Grey) au Nyeusi (Black).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Hudhurungi (Puce) na Fedha (Silver).
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Rangi ya Samawi (Ultramarine).

Kito (Jiwe) ni Black Onyx. Madini yao ni Risasi (Lead).

Manukato yao ni yale yatokanayo na Msonobari (Pine), Maua yanayofanana na ya Jamii ya Choroko, Njegere au Dengu (Sweet pea) na Magnolia.

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Uongozi.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye Uchangamfu na Furaha.

Maadili yao ni Uvumilivu, Utiifu, Ustaamilivu, Kuratibu, Kuandaa na Uwezo wa kuona mbali.
Matakwa yao ni Kutawala, Kusimamia na Kuongoza.
Tabia za kujiepusha nazo ni Kutokutegemea kuwa mambo mabaya yatatokea, Kuwa na masikitiko, Kutokupenda mabadiliko na Kupenda vitu na mali kupita kiasi.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Ng’ombe na Mashuke.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Punda, Kaa na Mizani.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mizani.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Punda.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Ndoo.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Kaa.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Mashuke na Mshale.

KIPAJI CHA MBUZI:
Mbuzi wana kipaji cha kuchambua mambo kidogo kidogo au kufuatilia kitu bila watu kujua na kupata ufumbuzi wa uhakika mwishoni.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Mbuzi wanapenda kuwajibika, ni wenye bidii ya kazi, katika kazi yeyote watakayofanya hata k**a ikiwa ni ya kipuuzi.
Ni viumbe waaminifu sana, watu wastahamilivu na wenye kuweza kuvumilia matatizo yeyote.

Kwa upande mwingine ni watu wenye tamaa kubwa ya kimaisha na kimaendeleo, na kwa sababu ya kutekeleza malengo yao basi huwa wanakuwa wabinafsi na wenye uroho na uchu.

Watu wenye nyota hii wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao, lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.

Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.
Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.

Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.

KAZI NA BIASHARA ZA MBUZI:
Mbuzi kitu muhimu katika maisha yake ni kazi na maisha mazuri na yanayoeleweka ambayo yako katika mpangilio wanaoutaka wao.
Ni watu ambao wanazingatia sana muda wa maisha na wana mpangilio maalum kwamba katika umri fulani awe amepata nini au awe na fedha kiasi gani.

Ni wenye kupenda utekelezaji wa kazi wa hali ya juu na wao wanapoagizwa hufanya hivyo.Kazi zao zinazowafaa ni zile za kutumia akili, Uhandisi, Usanifu Majengo, Saveya, kazi za Serikali, Siasa na Daktari wa Meno.

MAVAZI NA MITINDO:
Mbuzi wanatakiwa wavae nguo za mitindo, zilizoshonwa kwa ustadi. Nguo hizo ziwe za rangi ya kijivu au Kijani iliyoiva au hudhurungi nzito.Kitambaa kiwe cha kitani (Linen) au cha ngozi.
Nguo ziwe ni suti na ziambatane na saa za mikononi.

MAGONJWA YA MBUZI:
Nyota hii inatawala Mifupa, Magoti na Ngozi.Matatizo yao makubwa ya kiafya huwa yanasababishwa na muda mrefu ambao wanafanya kazi au kujishughulisha. Hii ni kwa sababu hawamwamini mtu mwingine afanye shughuli zao ambazo zina mipangilio ya muda mrefu,nguvu nyingi, na akili hutumika.

Shughuli zao nyingi za mizunguko na kufikiria huwaletea maradhi k**a Baridi Yabisi .
Maradhi yao mengine makubwa ni ugonjwa wa Ngozi, matatizo ya Magoti na maradhi ya mifupa.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MBUZI:
Mbuzi wanashauriwa wapende kula vyakula au matunda yafuatayo.ambayo ndio yanatawaliwa na nyota yao.Wapende sana vyakula vya N**i na Nyama yeyote. Vile vile wapendelee kula Viazi Vitamu na Samaki .

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa watu wenye uwezo wanashauriwa aidha waishi au watembelee miji au nchi zifuatazo ambayo inatawaliwa na nyota ya Mbuzi.
Miji hiyo ni Brussels (Ubelgiji) na Oxford (Uingereza) au nchi za Mexico na India

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mbuzi ni Risasi (Lead). Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Black oneyx
Mafusho ya Mbuzi ni Miatun- saila. unachoma siku ya Jumamosi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya mbuzi ni "natumia" basi yeye pale ambapo huwa anatumia vitu hovyo basi huzidi kupata vingine

ELIMU YA NYOTA          9.NYOTA YA MSHALE​Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu walioz...
18/10/2025

ELIMU YA NYOTA

9.NYOTA YA MSHALE

Hii ni nyota ya tisa katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Novemba na 20 Disemba au wenye majina yalio anza na herufi I au D au P au U.

Asili yao ni Moto.Siku yao ya Bahati ni Alkhamisi. Namba yao ya Bahati ni 5 au 7
Sayari yao ni Jupiter (Mushtara).

Malaika wake anaitwa Israfeel na Jini anayetawala alkhamisi anaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini

Rangi zao ni Bluu na Bluu iliyokolea.
Wenye nyota hii wanatakiwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au sehemu zao za biashara rangi zenye kusisimua na uchangamfu na zinazoashiria hali ya kumkaribisha mgeni. Rangi hizo ni Nyekundu iliyochangamka (Warm Red) rangi ya Zambarau (Purple) na rangi ya hudhurungi au kahawia (Brown).

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi za Njano na Njano-machungwa.
Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Nyeusi na Bluu iliyoiva.

Kito (Jiwe) ni Feruzi (Turquoise) na Kito chekundu (Carbuncle).Madini yao ni Bati.

Manukato yao ni Yasmini (Jasmine), Manemane (Myrrh).

MAMBO MUHIMU:-

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni kuwa wenye uwezo wa Kuongoza, Kuratibu, Kuandaa, Kupanga na Kusikiliza kwa makini.

Maadili yao ni Ukweli, Kuona mbali, Ukarimu na Kuwa na uwezo wa kusikiliza mawazo ya wenzake japokuwa siyo lazima akubaliane nayo.

Matakwa yao ni Kupanuka kimawazo.

Tabia za kujiepusha nazo ni Kutegemea mambo kuwa yatakuwa mazuri siku zote, Kutia chumvi mambo na Kuzidisha Ukarimu kwa kutegemea hela za watu wengine.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Punda na Simba.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Mapacha, Mashuke na Samaki.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Mashuke.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Samaki.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mbuzi.

Nyota inayomsaidia katika ubunifu ni nyota ya Punda.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Mapacha.

Nyota bora ya kujifurahisha ni nyota ya Punda.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Simba na Nge.

KIPAJI CHA MSHALE:
Mshale wana kipaji cha kutabiri na kujua mambo ambayo yatatokea mbele au muda utakaokuja, na mara nyingi wanalolisema huwa linatokea hata likiwa la kipuuzi.

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:

Mshale ni wenye tabia ya kuwa na matumaini ya mafanikio kwa lolote wanalolitegemea. Wanapenda kuwa na uhuru wa kupenda na kuchagua na wanapenda watu wengine wawe k**a wao.
Hawapendi mambo nusunusu.
Ni watu ambao wako wazi na wanaopenda kusoma. Ni wakweli na ukitaka kuelewana nao na wewe uwe mkweli.
Mshale ni watulivu, waaminifu na wanapenda uadilifu,.hawapendi kuamrishwa kufanya jambo kwa sababu wanaamini kwamba wao wenyewe wana uwezo mkubwa wa kutekeleza jambo lolote, lakini likiwaudhi wanakuwa wakaidi na wasioweza kutii amri.
Wenye nyota hii hawaoni taabu kusema lolote bila kujali athari zake, mradi jambo hilo liwe la kweli.

Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe, huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Katika mapenzi ni wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.

Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanapoonyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.

Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali, inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.

KAZI NA BIASHARA ZA MSHALE:
Mshale ni waaminifu wanaopenda sana mafanikio, wako tayari wakati wowote katika kazi. Kutokana na hili wana bahati ya kuwa katika sehemu muafaka na katika muda unaotakiwa.
Wenye nyota hii ni wafanyakazi waaminifu na hawapendi kuwasimamia watu katika kazi. Wanawaamini wafanyakazi wao na wanapokuwa ofisini huleta mazingira ya urafiki na kuaminiana.
Kazi zinazowafaa ni za usafiri, kazi za sheria, Wakili au Hakimu, kazi za uandishi, ualimu, dini, sheikh au padri au makanisani au misikitini, michezo, kazi za kijeshi na uuzaji.

MAVAZI NA MITINDO:
Mshale wanatakiwa wavae nguo zenye kuathiri na za mzaha mzaha k**a koti au blauzi isiyo rasmi au nguo za kitamaduni zilizoongezwa ongezwa vitu vingi k**a maua au nakshi nakshi.
Rangi ya nguo zao iwe ya Zambarau au rangi ya Hudhurungi iliyochangamka au rangi ya blue.
Vitambaa viwe vya sufu. Nguo ziambatane na mikanda, na viatu viwe vya buti. Wanawake wapendelee kuvaa sketi.

MAGONJWA YA MSHALE:
Nyota hii inatawala sehemu ya chini ya kiuno. Wenye nyota hii hawapendi kuugua. Lakini huwa wanapata maradhi kutokana na kujishughulisha kupita kiasi na kutumia nguvu zao na akili zao kwa muda mrefu bila mapumziko. Wanathamini sana mizunguko kuliko mapumziko.Vile vile ni watu wasiopenda ushauri kuhusiana na afya zao.

Tatizo lao lingine ni kuwa wanapenda sana kula na kunywa na hiyo huwaletea unene usiotakiwa. Wakitaka kujikomboa na matatizo wanashauriwa wawe na tabia ya kujipumzisha.

Magonjwa yanayohusiana na nyota hii ni majereha na maradhi ya nyonga, mapaja, maradhi ya ini (Liver Disorder) kupooza kwa miguu (paralysisi of limbs) na ugonjwa wa kuumwa mishipa au misuli ya nyuma ya paja.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA MSHALE:
Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao. Nyama mwitu, kunazi za rangi ya bluu, maboga na juice ya mapera.
Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota zao.
Nchi hizo ni USA na SPAIN na miji ni Budapest (Romania) na Cologne (Ujerumani).

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Mshale ni Bati. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Yakuti ya njano au Lapis Lazuli

MAFUSHO:
Mafusho ya Mshale ni Udi Kafur. unachoma siku ya Alkhamisi kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:
Funguo ya nyota ya mshale ni "nalenga" yeye akilenga kitu basi huwa hakosi hata akikipania

18/10/2025

ELIMU YA ABJAD;JINSI YA KUVUTA UTAJIRI NA MAFANIKIO MAKUBWA KWA HERUFII YA LAAM.

ELIMU YA NYOTA         8. NYOTA YA  NGEHii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa ...
17/10/2025

ELIMU YA NYOTA

8. NYOTA YA NGE

Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12. Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya Tarehe 23 Oktoba na 22 Novemba au wenye majina yaliyoanza na herufi H au N au Y au S

Siku yao ya Bahati ni Jumanne, Namba yao ya bahati ni 9.Asili yao ni Maji.
Sayari yao ni Pluto.

Malaika anayetawala nyota hii anaitwa Samael au Israeel na Jini wa siku hii anaitwa Abuu Muhriz al Hammar

Rangi zao ni Urujuani nyekundu. Nge wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia k**a rangi ya damu ya mze

Rangi zinazowapa uwezo wa mapenzi, mahaba na furaha ya kujumuika na watu ni rangi ya Kijani.

Rangi inayowapa uwezo wa Kipato ni Bluu.

Kito (Jiwe) ni Bloodstone, Ruby,Rhodochrosit, Diamond
Madini yao ni Chuma, Radiamu (Radium) na Chuma cha pua (Steel).

Manukato yao ni ya Msandali (Sandalwood)

MAMBO MUHIMU:-

Sifa ya Nyota hii ni Kuwa Imara.

Ubora unaohitajika kusawazisha mambo ni uwezo wa kuangalia na kujua mambo kwa upana zaidi.

Maadili yao ni Utiifu, Kuwa Imara, Kuazimia jambo, Ujasiri na Undani.

Matakwa yao ni Kuingilia undani wa kitu na kukibadilisha.

Tabia za kujiepusha nazo ni Wivu, Kupitiliza kisasi, Kutokubali Kusamehe, kutoshawishika au kutobadilika, kuwa mbishi, mng’ang’anizi.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota za watu ambao anaelewana nao ni nyota za Kaa na Samaki.

Nyota za watu ambao haelewani nao ni nyota za Ng’ombe, Simba na Ndoo.

Nyota inayomsaidia kikazi ni nyota ya Simba.

Nyota inayomsaidia kihisia ni nyota ya Ndoo.

Nyota inayomsaidia kipesa ni nyota ya Mshale.

Nyota inayomsaidia katika Ubunifu ni nyota ya Samaki.

Nyota bora ya Mapenzi, Ndoa na Ushirikiano ni nyota ya Ng’ombe.

Nyota bora ya Kujifurahisha ni nyota ya Samaki.

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya kidini na kiroho ni nyota za Kaa na Mizani.

KIPAJI CHA NGE:
Nge wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji. Mystical

TABIA ZAO KIMAUMBILE NA KIMAPENZI:
Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni wenye uelewa mkubwa, majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.
Wana tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.
Ni wasiri na wanaopenda kufanya mambo yao kwa siri sana. K**a ilivyo alama ya nyota yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.

Ni wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Nge vile vile wanaweza kujidhuru wao wenyewe. Mambo yanapowawia magumu.
Wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi k**a njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.

Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.

Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.

KAZI NA BIASHARA ZA NGE:
Nge ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni waerevu na wenye kung’amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.

Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono au biashara zinazoendana na mambo hayo.

MAVAZI NA MITINDO:
Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong’ara, zenye kuonekana na maridadi, zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja. Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta. Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali

MAGONJWA YA NGE:
Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, mlango wa kizazi (cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).

Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono.
Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya k**e na mabusha.

VYAKULA, NCHI, NA MIJI YA NGE:
Nge wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.

Miji hiyo ni Liverpool (Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.

MADINI, VITO NA MAFUSHO:
Madini ya Nge ni Chuma. Vito vyao vya kuvaa katika pete ni Bloodstone, Ruby na diamond

Mafusho ya Nge ni Qist. unachoma siku ya Jumanne kati ya saa 12-1 asubuhi na saa 7-8 mchana.

FUNGUO:

Funguo za nyota hii ni "natamani" wao wakitamani kitu kikawa kaa rohoni basi hukipata

ELIMU  YA  ABJAD     FAIDA  YA HERUFI YA BE/BA  (B )   Hii ni herufi  ya 2  katika mpangilio wa herufi za  ABJAD.Herufi ...
17/10/2025

ELIMU YA ABJAD

FAIDA YA HERUFI YA BE/BA (B )
Hii ni herufi ya 2 katika mpangilio wa herufi za ABJAD.Herufi hii inauzito wa 2, siku yake ni juma pili(shamsi) na ina maana ya Bee.
Herufi hii ina kazi nyingi sana, moja kati ya kazi za herufi hii ni pamoja
na;

1.KINGA DHIDI YA WEZI WACHAWI NA MAJINI.
K**a mtu yeyote ataiandika herufi hii katika kikombe cheupe cha udongo kwa lugha ya kiarabu kwa idadi ya X21 kwa kutumia dhafarani au makapeni nyekundu, kisha kikombe hicho ukakisomea jina hili YAA RAHMAAN YA RAHIIM X 221, kisha kikombe hicho ukakiweka katika nyumba yako au shamba lako au sehemu
yako ya biashara au chumba chako n.k kwa nia ya kuhitaji kuweka kinga katika eneo hilo,
hakika hatoweza kuingia mwizi, wala kiongozi jeuri wala jinni wala mchawi katika eneo hilo.

2.KUONDOA NUKSI NA MABALAA KATIKA MWILI
K**a mtu yeyote ataiandika herufi Bee kwa kiarabu katika karatasi kwa kutumia wino wa dhafarani kisha akayaosha maandishi hayo kwa maji safi kisha maji hayo akatumia kwa kujipakaa mwili
mzima, huondoa nuksi na mbalaa katika mwili.
Tumia kujipakaa asubuhi na jioni kwa muda wa
siku saba mfululizo inshaaallah utakuwa vizuri.

3.KUMDHALILISHA MTAWALA AU KIONGOZI JEURI.
K**a unahitaji kumdhalilisha mtawala au kiongozi jeuri basi utaiandika herufi hii ya B kwa kiarabu kwa idadi ya X 12 Katika karatasi siku ya jumanne asubuhi saa moja au saa nane mchana. Kisha karatasi hiyo utaikunja vizuri kisha itie mfukoni alafu
nenda kakutane nae kiongozi huyo hakika
atadhalilika sana na atakunyenyekea kweli.

4.KUONDOA UCHAWI NA MAJINI KATIKA MWILI.
K**a unahitaji kumtibu mgonjwa mwenye uchawi na majin,basi utaiandika herufi Bee kwa idadi ya X 12 Katika chombo cha udongo kwa kutumia wino wa
dhafarani kisha utayafuta maandishi hayo kwa maji safi.Kisha maji hayo utatumia kwa kunywa kidogo kidogo na maji mengine utachanganya katika maji
yako ya kuoga kisha utatumia kwa kuoga asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba mpaka 14 hakika hundoa uchawi na majini katika mwili.
Wakati unaiandika herufi hii utakuwa unasema maneno haya mpaka utakapomaliza kuandika “YAA RAHMAAN YAA RAHIIM”

5.KUMTOA MTU KIFUNGONI
K**a mtu amefungwa gerezani naye akahitaji kutoka basi atamke herufi B kwa idadi ya mara 500 kila siku kisha amuombe mwenyezimungu amfanyie
wepesi wa kutoka gerezani hakika ataachiwa huru mtu huyo baada ya muda kidogo tu kupita.

6.KUONDOA HUSDA ZA KIJINI NA UCHAWI.
K**a mtu amefanyiwa husda za kijini au uchawi naye madhara ya husda hiyo yakadhihiri au akapata shida yoyote kutokana na husda hiyo basi utaandika
herufi hii ya Bee kwa idadi ya X 71 kwa wino wa dhafarani kisha utayafuta maandishi hayo kwa maji
safi kisha tia nia yako ya kuhitaji kuondoa husda hizo,kisha mgonjwa atatumia maji hayo kwa kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba inshaallah
husda na madhara hayo yataondoka kwa idhini ya mwenyezimungu.

7.KUTIA MOYO NURU NA KUONDOA UVIVU KATIKA AKILI.
Iwapo k**a utaiandika herufi Bee mara 400 katika siku ya jumatano au saa ya Atwarid kwa kutumia wino wa dhafarani kisha ukayaosha maandishi hayo kwa maji safi, kisha maji hayo ukatumia kwa kunywa kila linapozama jua kwa
muda wa siku saba ,hakika hutia moyo nuru,kuipa akili nguvu na kutakasa moyo, na kuondoa uvivu katika akiri.
Wakati unaiandika herufi hiii utakuwa unasema au
unasoma uradi huu “ YAA QAYUUM YAA WAHAAD”

8.KUPENDWA SANA NA WATU NA KUWA KARIBU NAO.
K**a mtu ataisoma herufi Bee kwa idadi ya X 120 kila siku , basi watu watampenda sana na watapenda kuwa karibu nae kwa kuhitaji kushirikiana nae.
Herufi Bee huondoa maradhi ya baridi, huvuta mahaba kwa umpendae mke au mume inaongeza Qubri,huondoa uvivu na msongo wa mawazo kinga
ya wezi katika mji na mashambani,pia hufunga macho ya majambazi inafunga ndimi za watu
wanaokusema vibaya n.k, hakika herufi hii ina kazi nyingi sana.

Unaweza kufatilia masomo haya ya Herufi za Abjad kwa ufafanuzi zaidi katika chanel yangu ya Youtube kwa kubofya link hiyo hapo chini👇👇👇
https://bit.ly/3QXJP4s

ELIMU  YA NYOTA.            7.NYOTA YA MIZANIHii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12,Nyota hii ni kwa watu wali...
16/10/2025

ELIMU YA NYOTA.

7.NYOTA YA MIZANI

Hii ni nyota ya saba katika mlolongo wa nyota 12,Nyota hii ni kwa watu waliozaliwa kati ya tarehe 23 september hadi 22 october au wenye majina yanayoanzia na R au T.
nyota hii Usawa wake ni Dume
Hali yake ni: Thabiti
Mizani ni nyota ya utendaji,ulaini wa mambo,yenye amani,kupenda uzuri na sifa njema,kidoplomasia na yenye kung'ara katika jamii.

Sayari yako ni VENUS (ZUHURA).
sayari hii wengine huitambua k**a kiumbe wa mapenzi au mtawala mapenzi:
kinyota hujulikana k**a sayari inayosimamia maelewano,amani,radhi ya uraia na kukimbilia mambo yakijamii,sanaa na kupamba, lakini pia ni yenye kujishughulisha na mapenzi ya starehe.

alama yake ni mizani: ambayo humaanisha usawa,msawazo,mpangilio na hak

Siku yako ya Bahati ni Ijumaa.

Namba ya Bahati ni 6 na 9.

Malaika wa sayari na nyota hii huitwa Anyail na Jini wa nyota hii huwa ni Jini wa sayari ya Venus pia anaitwa Zawbat na shetani wake anaitwa Succubi(jini mahaba)

Manukato ya Mizani:
K**a ilivyo kwa maua yao basi wenye nyota hii wapendelee zaidi kupaka marashi yaliyochanganyika na mauwaridi ndani yake na yenye harufu isiyokera

Rangi za Bahati:
Rangi za bahati kwa wenye nyota hii ni Kijani isiyoiva. Blue pamoja na lavender rangi hizi huwafaa zaidi kwa sababu huwasilisha mapenzi,furaha na urafiki ambapo pia watu hawa hupenda sana kujihusisha na mapenzi na yanayohusu hayo.

Asili ya nyota hii ni UPEPO.

KIPAJI CHA MIZANI
(Extra Sensory Perception)
Wenye nyota hii wana kipaji cha kufumbua mafumbo na kujua siri za watu bila kuambiwa. na kuweza kumjua mtu vizuri kabla ya yeye kuanza kujielezea.

TABIA ZA MIZANI:
Wenye nyota ya Mizani wana tabia ya kupenda usuluhishi, amani na upatanishi. Ni watu wasikivu, watiifu, na wepesi kuongozwa. Ni wenye maumbo ya kupendeza hasa wanawake. Kwa ujumla ni watu wenye roho nzuri na wanajua kupenda na wenye mahaba mengi.
Ni watu wastaraabu, wenye adabu heshima na ni wakarimu kwa mtu yeyote na wanajipenda sana. Katika maisha yao wajipenda sana.

TABIA YA MIZANI KATIKA MAPENZI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina
matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (S*x) wao ni mabingwa. Wanajua sana
kumpendeza mwanamke kwa maneno matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri

MAMBO MENGINE:

wenye nyota hii wanatakiwa kuwa waangalifu sana kwenye mapenzi hasa kipindi cha kuoa kinapofika kwa maana ndio maamuzi ya mwisho ya maisha yao kinyota, wenye nyota hii ni rahisi kupendeka na wenye ulaini wa mapenzi na ni watu wa kuvutia na wenye kuvutia kimaongezi kwa sababu wana kipaji cha kimvutia mtu kimaelezo na kumfanya ajihisi raha kuzungumza nao, wenye nyota hii ni watu wenye Tabasamu laini na wenye hisia za kimapenzi wakati mwingi na pia huonekana k**a watu wa ajabu sana duniani,wao huzaliwa wakiwa na asili ya kujali wengine. Nyumba zao utakuta zimepambwa vizuri kwa maua kupendeza na mapambo ya thamani,nguo na manukato pia vinywaji huwa havikatiki ni nyota yenye kujipenda zaidi wao hufurahia kila kitu ambacho pesa inaweza kununua,
Nyota hii ni nyota ya mwenza hupenda sana kutembea na mtu na hawapendi kutembea peke yao hata barabarani unless imewalazimu.

USHIRIKIANE NA NANI?

Nyota inayomfaa zaidi kindowa ni nyota ya punda

Nyota za watu ambao “Wanaelewana” nao ni nyota za Mapacha na Mshale.

Nyota za watu ambao “Hawaelewani” nao ni nyota za Ng'ombe, Mashuke na Mbuzi.

Nyota inayomsaidia “Kikazi” ni nyota ya Mapacha

Nyota inayomsaidia “Kipesa” ni nyota ya Mshale

Nyota inayomsaidia katika “Ubunifu” ni nyota ya Mapacha.

Nyota bora ya “Kujifurahisha” ni nyota ya Punda

Nyota ambazo zinamsaidia katika mambo ya “Kidini na kiroho” ni Nyota za Mshale na Samaki.

MITIZAMO YA WATU:
Wenye nyota hii watu wakiwaangalia mara nyingi, huwaona kuwa ni watu wa muhimu sana hata katika familia au vikao vya ukoo mtu huyu huwa hasahauliki kwa sababu tu ya kuyatanua mawazo ya watu walioyatoa na lakini pia mara nyingine huonekana ni watu wanaoleta vurugu na ujuaji kwenye mijadala au wanakuwa ni watu wenye mitizamo tofauti na wengine na kuna muda huonekana wapumbavu kwa tabia yao ya kung'ang'ania kitu wanavyoelewa wao ndio na watu wengine waelewe hivyo hivyo kwa wengine muonekano wake wote huwaonyesha kuwa ni mtu asiye na maana kwa muonekano anaokuwa anajiweka hili huwa linamuumiza pia

MAGONJWA YA MIZANI
Wenye nyota hii hussumbuliwa sana na magonjwa ya mgongo hasa karibu na makalio ni watu wenye kusumbuka na figo pia na mgongo wa chini hasa kwenye maungio ya makalio na maambukizi ya figo huwa ni magonjwa yanapendelea sana nyota hii.

MADINI YA MIZANI:
Madini ya wenye nyota hii ni Copper.

WANYAMA:
Wanyama wa nyota hii ni Nyoka na Mijuzi

VITO:
Wenye nyota hii wanatakiwa wavae kito cha Opal kwa maana kito hiki huwaletea mafanikio kipesa au kipato na humuondoshea mwenye nyota hiyo wivu na tamaa na huwaletea uelewa na ufahamu wa mambo yote wanayohitajia kuyajua.

MAFUSHO:
Mafusho ya mizani ni Ubani Mashtaka:
una rangi ya kijivu na ni mgumu pia unapukutika unga mweupe.

KAZI NA BIASHARA:
Wenye nyota hii kazi nzuri kwao huwa ni kazi za uhusiano wa jamii, Ushauri wa Ndoa, Biashara ya Sanaa, Ushauri wa Mambo ya Urembo, Uanasheria, Uhakimu pia biashara za kuziba pancha na kujaza upepo au kupamba maharusi zinawafaa zaidi
Kazini wenye nyota hii huwa ni washiriki wazuri na wenye upendo wa wafanyakazi wenzao na pia wenye nyota hii ni wajanja pia katika mbinu za kazi za ushirikiano nao huusishwa sana kwenye kazi za pamoja.

MAUA:
Maua yanayofaa katika nyota hii ni Uwaridi kwa maana nyota hii hutawala zaidi kwenye mapenzi

UHUSIANO WA KIMAPENZI
(Punda na Mizani)
Tabia ya Punda ya haraka haraka. Vishindo na kutumia nguvu bila kufikiria, hulainishwa au kuzimwa na diplomasia, uerevu na ujanja wa mizani. Punda vile vile hupendezwa na uwezo au kipaji cha mahaba walichonacho wenye nyota ya mizani.

HATARI ZA MIZANI:
Nyota hii wao ni watu wa kupenda kuchochea hisia mbaya kutoka kwa wengine inapokuja kwenye suala la mapenzi na wao hujiweka rahisi sana katika kutamka maneno ya mapenzi kwa watu na kujieleza kimapenzi kirahisi yaani kujirahisi kimapenzi ni tabia walionayo Mizani na mapenzi yao huwa ya hasira na wenye kuvunja moyo wengine na ni rahisi sana wao kukusaliti na kutokukuamini. hivyo jiweke makini katika swala la mapenzi wewe na uwapendao.

FUNGUO:
Funguo ya mizani ni "ninalinganisha" akijilinganisha na kitu au mtu huyo basi humpata akifanya hivyo akilini kwake

OFAA       OFAA     OFAA    Ndugu  mfatiliaji wa group la Tiba Facts na Chanel ya Tiba Facts  Online Tv,  Tukiwa  tunael...
16/10/2025

OFAA OFAA OFAA

Ndugu mfatiliaji wa group la Tiba Facts na Chanel ya Tiba Facts Online Tv,
Tukiwa tunaelekea katika maazimisho ya NYERERE DAY katika mwezi huu, tunapenda kukupa fursa ya kupata vitabu vyetu vya elimu ya tiba kwa bei ya ofa.

k**a bado hujamiliki Nakala za vitabu vyangu vinavyofundisha elimu ya Tiba kupitia

Quran ,Mitishamba, Matunda, Elimu ya Barhatih, Elimu ya ABJAD , ulimwengu wa majini na vituko vyao, na Furaha ya ndoa,

Nawe ukatamani kujifunza elimu hizo basi leo nakupa OFAA YA KUJIPATIA NAKALA YA VITABU HIVYO KWA BEI YA OFAA k**a ifuatavyo;

Kitabu cha,
1."MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI" No.1
Huwa kinauzwa Tsh 7,000/=

2.Kitabu cha ,
"MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI" No.2
Huwa kinauzwa Tsh 10,000/

3.Kitabu cha,
"MAAJABU YA MITISHAMBA KATIKA KUTIBU MARADHI YA KIJINI NA UCHAWI" No.3
Huwa kinauzwa Tsh 16,000/=

4.Kitabu cha,
"TIBA MBADALA KWA MARADHI YA KIBAIOLOJIA"
Huwa kinauzwa 10,000/=

5. Kitabu cha,
"MAAJABU YA QUR'AN TUKUFU KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI"
Huwa kinauzwa kwa Tsh 12,000/=

6.Kitabu cha MAAJABU YA QUR'AN TUKUFU KATIKA KUTIBU MARADHI NA KUONDOSHA SHIDA MBALIMBALI, No.2 15,000/=



7.Kitabu cha,
"UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH" No.1
Huwa kinauzwa Tsh 15,000/=

8.Kitabu cha,
"UTUKUFU WA MAJINA 28 YA BARHATIH",No. 2
Huwa kinauzwa 15,000/=

9.Kitabu cha Elimu ya ABJAD
Huwa kinauzwa 20,000/=

10.Kitabu cha Ulimwengu wa majini na vituko vyao.
Huwa kinauzwa 30,000/=

11.Kitabu cha MUONGOZO WA TABIBU
Huwa kinauzwa 20,000/=

12.Kitabu cha FURAHA YA NDOA,
Huwa kinauzwa 15,000/=

Gharama ya kuvipata vitabu vyote ni Tsh 185,000/=

Leo utavipata vitabu vyote hivyo kwa BEI YA OFAA ya Tsh 45,000/= 🙏🙏🙏tu

Okoa Shilingi 140,000/=
kwa kujinyakulia vitabu hivyo kwa bei ya OFAA leo.

Lipa pesa kupitia namba hizi hapa 👇👇👇

+255764010104(Mpesa)
+255672410104(Tigo pesa)
+255782010104(Airtel money)
(Namba zote hizo zinapatikana WhatsApp)

Jina katika namba zote hizo ni BASHIRI HUSSEN LUGAMBA.

Kisha baada ya kufanya malipo nitumie screenshort ya muamala huo katika whatsApp yangu kupitia namba moja wapo kati ya hizo.

Ikifuatiwa na neno NYERERE DAY
Baada ya kuthibitisha malipo yako kwa kutuma ujumbe whatsApp, basi utatumiwa vitabu hivyo kwa njia PDF katika whatsApp yako au Email yako ukiwa nchi yoyote duniani, ndani ya dakika 30 tu.



NB: OFAA HII NI KUANZIA
Tarehe 1O/10/2025

MWISHO WA OFA NI
Tarehe 20/10/2025

Kumbuka ukiikosa OFA HII itakubidi ulipie 185,000/= ndipo uweze kumiliki vitabu vyote kumi (12)

Wahi mapema UJINYAKULIE NAKALA ZA VITABU KWA BEI YA OFAA.

Address

Majengo
Mpanda
50110

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tiba Facts posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tiba Facts:

Share