New Muleba Generation

New Muleba Generation Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from New Muleba Generation, Social Media Agency, Muleba.

NEW MULEBA GENERATION NI UKURASA AMBAO UNAWAKUTANISHA VIJANA WA MULEBA DUNIANI KOTE KWA AJIRI YA SHUGHULI ZA KIJAMII KAMA (CHARITY) PIA INAJIKITA KWENYE MASWALA YA KIMICHEZO NA KUTOA ELIMU KUHUSIANA NA AFYA, SHERIA, NDOA NA MAHUSIANO.

09/10/2025
NEW MULEBA GENERATIONNi muda sasa wa kuanza maandalizi rasmi kuelekea CHARITY WALK itakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu...
09/10/2025

NEW MULEBA GENERATION
Ni muda sasa wa kuanza maandalizi rasmi kuelekea CHARITY WALK itakayofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Tukio hili litakuwa ni sehemu ya kusherehekea kukutana pamoja k**a vijana wa NMG, tukionyesha umoja, upendo na kujitolea kwa jamii.

Kupitia CHARITY WALK hii, tutalenga kutoa tabasamu kwa wale wenye uhitaji, tukisisitiza dhamira yetu ya kuwa vijana wanaoleta mabadiliko chanya katika jamii.

Tunaanza sasa kuandaa Mkeka wa ushiriki na michango kwa wale wote watakaokuwa sehemu ya tukio hili muhimu.

🗓️ Muda: Mwisho wa mwaka 2025
📍 Mahali: Taarifa kamili itatolewa hivi karibuni
🎯 Lengo: Kusaidia wenye uhitaji na kuimarisha mshik**ano wa vijana wa NMG

Kila mwanachama anahimizwa kushiriki kikamilifu katika maandalizi na kuchangia kwa uwezo wake.
Pamoja tunaweza (Together we rise! 💪)

25/06/2025

NEW MULEBA GENERATION JOGGING CLUB KILA JUMAMOSI YA WEEK KM 12.

SIO DEAL
KWA AFYA YA AKILI

11/05/2025

Hili lilikuwa Zoezi ambalo Vijana wa New Muleba Generation kwa Kushirikian na Uongozi wa Wilaya walihamasisha zoezi la Uchangiaji damu ili kuokoa Vifo vya Wagonjwa Mahosptalini ambao wanapoteza maisha kwa kukosa Damu.

Moja ya Picha Kali sana Ya Mwaka 2024 Chini ya Vijana Makini Mabalozi wa Bidhaa za New Muleba Generation.Haya Yote Yapo ...
11/05/2025

Moja ya Picha Kali sana Ya Mwaka 2024 Chini ya Vijana Makini Mabalozi wa Bidhaa za New Muleba Generation.

Haya Yote Yapo ndani Ya Muleba Kupitia New Muleba Generation. Ukiwa Mbali na NEW MULEBA GENERATIONA unakuwa Mbali na dunia.

Karibu Tuijenge Muleba Yetu kwa Kiwango kinachostahiki.

11/05/2025

Tunajivunia kuwa zao la Muleba kupitia Brand yetu ya MADE IN MULEBA.

Ukiwa Kijana Wa Muleba asili yako, chanzo Chako ni ardhi ya Muleba wewe ni zao ni product ya Muleba umetengenezwa Muleba ndo maan halisi ya MADE IN MULEBA.

11/05/2025

Kwenye Moja na Mbili Mashindano ya Ngoma ya asili siku ya NEW MULEBA GENERATION DAY.

K**a mdau wa michezo natumaini utavutiwa makala haya yanayohusu Sheria mbalimbali na Kanuni za Mpira wa Miguu.1. UWANJA....
08/05/2025

K**a mdau wa michezo natumaini utavutiwa makala haya yanayohusu Sheria mbalimbali na Kanuni za Mpira wa Miguu.

1. UWANJA.

Kwa kawaida uwanja wa mpira wa miguu huwa na Urefu wa mita 100 – 120 na Upana wa mita 50 – 90 .Mpira wa miguu una alama za mistari ambazo ni pamoja na

– Mstari mrefu pembeni mwa Uwanja unaoashiria mwisho Wa Uwanja .

– Mstari mrefu wa katikati unaogawa Uwanja katika pande 2 zilizolingana.Pia katikati ya uwanja kuna mduara wenye nusu kipenyo cha mita 9.15.

– Mstari mrefu Upande wa goli Unaoashiria mwisho wa Uwanja upande wa goli .

– Pia kuna nusu duara katika makutania ya mstari wa pembeni na mstari wa goli ambapo huitwa Kona .

2. MPIRA.

Mpira wa miguu unaweza kutengenezwa kwa kutumia Ngozi , plastiki , au makunzi mengine yanayofaa . Kwa kawaida mpira wa miguu huwa na kipenyo cha sm 68 – 70 na uzito wa gramu 410 – 450 na Ujazo wa 1.1 – 1.6 .

– Utofauti wa Kipenyo na Uzito wa mpira wa miguu hutegemea uwezo ama rika la mchezaji au watumiaji .

3. IDADI YA WACHEZAJI.

Mpira wa miguu huchezwa na wachezaji 22 maana ya wachezaji 11 Kwa kila timu , Wachezaji wa akiba wanaoruhusiwa ni 7 na kati ya hao wanaoruhusiwa kucheza ni wachezaji watatu (3) tu .

Katika mashindano ambayo hayatambuliwi na FIFA Idadi ya wachezaji wa akiba inategemeana na makubaliano ya timu 2 husika .

4. VIFAA VYA MICHEZO.

Vifaa vya michezo ni muhimu katika mchezo wa mpira Wa miguu , kwa kawaida mpira wa miguu unahitaji vifaa k**a vile Sare ambazo hazifanani na timu pinzani wala mwamuzi wa mchezo na walinda milango , Viatu , soksi , Kitambulisho/Kitambaa cha Unahodha , Filimbi , Daftari la kutunzia Kumbukumbu za mchezo , Saa , Kadi ya Njano na Nyekundu , Pia na Ubao Unaotumika kubadilishia wachezaji , Kibendera Kwaajili ya Waamuzi wasaidizi na Nyavu za magoli .

5. MWAMUZI.

– Mwamuzi ndiye anayeongoza mchezo na Kutafsiri sheria wakati wa mchezo .Hutoa maamuzi ndani ya Kipindi cha mchezo na kutoa taarifa ya mchezo husika .

– Ndiye msemaji au mwamuzi wa mwisho, Pale inapobainika kwamba Sheria ya mchezo imekiukwa kwa namna yeyote ili ikiwa ni pamoja na kutoa adhabu pindi mchezaji anapofanya Kosa ndani ya Uwanja .

6. WAAMUZI WASAIDIZI.

Hawa ni Watendaji wengine wanaomsaidia mwamuzi wa katikati wakati mchezo unaendelea .

– Humsaidia mwamuzi mkuu kuhusu matukio yanayotendeka nje na ndani ya Uwanja .

– Idadi ya waamuzi wasaidizi Hutegemea mashindano au mchezo husika , Waamuzi hao hutambulika k**a washika vibendera Namba 1&2 na Kamisaa wa mchezo anayetunza kumbukumbu. Pia mashindano mengine huruhusu waamuzi wakae nyuma ya goli. mfano, LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA.

7. MUDA.

Kwa kawaida mpira wa miguu huchezwa kwa dakika 90′ katika Vipindi 2 Yaani dk 45′ Kwa kila kipindi , Baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza cha mchezo mchezo husimama ( mapumziko) kwa muda Usiopungua dk 10 na Usiozidi 15 .

Pia , K**a muda Wa nyongeza dk 30′ Utaongezwa kwa Lengo la kumpata mshindi , timu zitapumzika kwa dk 5′ tu baada ya dk 15′ wa kipindi cha kwanza katika dk 30 za nyongeza ( Extra time ) na kipenyo kisha kubadilishana magoli tayari kwa kumalizia kipindi cha 2 . Ila muda waweza kupunguzwa kwa makubaliano ya timu husika .

8. KUANZA NA KUANZISHWA TENA MCHEZO.

Mpira huanzishwa kwa timu 1 kucheza mpira baada ya mwamuzi kuruhusu mchezo kuanza .

Mchezo huanzishwa tena baada ya goli kufungwa na baada ya kosa kutendeka na mwamuzi akapuliza Filimbi au k**a mpira ukatoka nje au mchezaji kuumia N.K

9. MPIRA KUWA NJE NA NDANI YA UWANJA.

Mpira Utakuwa nje ya mchezo k**a mpira Utatoka nje ya Uwanja na pia baada ya goli kufungwa .

Na pia , mpira Utakuwa ndani ya mchezo k**a uko ndani ya Uwanja na Unaendelea Kuchezwa .

10. NAMNA YA KUFUNGA GOLI.

Katika mchezo wa mpira Wa miguu , goli litahesabiwa k**a mpira utavuka Mstari wa goli na kuingia katika eneo la wavu kwa Kufungwa au Kujifunga .

Pia goli litahesabiwa k**a mpira Utavuka mstari chini ya Uwanja au Ukiwa hewani na Ukaonekana kuvuka Mstari wa goli .

11. KUOTEA.

KUOTEA Ni kitendo cha mchezaji kuzidi au kupokea mpira akiwa mbele ya wachezaji wote wa timu pinzani na akiwa ndani ya Eneo la timu pinzani .

– Mchezaji anaweza akawa katika nafasi ya kuotea lakini asitafsiriwe k**a ameotea k**a hajajishughulisha kabisa na mpira .

– Dhana ya kuotea hutegemea mambo matatu muhimu ambayo ni Nafasi , Kucheza na Kutoa .

– Pia mchezaji hatakuwa ameotea ikiwa walinzi wa timu pinzani watamkimbia au kutojishughulisha kabisa pale mchezaji wa timu pinzani atakapo pokea mpira na kufunga goli .

– Mchezaji hatatafsiriwa k**a ameotea akiwa amepasiwa na mchezaji wa timu pinzani kwa Kujua au Kutojua .

– Pia, Ikiwa mchezaji yuko katika nafasi ya kuotea na mwenzake mwenye mpira akapiga mpira golini moja kwa moja bila kumpasia mpira huyo aliyeko katika nafasi ya kuotea na kufunga goli, hapo mwamuzi ataruhusu goli bila kutafsiri Kuotea .

– Mchezaji atakuwa ameotea Iwapo mpira Utapigwa golini Ukagonga mlingoti mojawapo wa goli au mlinda mlango na kurudi ndani ya Uwanja na kuguswa na mchezaji aliyekuwa katika nafasi ya Kuotea .

– Aidha, hakutakuwa na dhana ya kuotea pale mchezaji atakapokutana na mpira Uliochezwa na mlinda mlango .

– Mpira wa kurushwa hauna kuotea , Pia mchezaji hatakuwa ameotea endapo atapokea mpira katika eneo lake kabla hajavuka Mstari wa katikati ya Uwanja .

12. MAKOSA YA UTOVU WA NIDHAMU.

Ni kutenda jambo ambalo lililo nje ya kanuni za kimchezo wa mpira Wa miguu au kuonyesha tukio lisilo la Kiungwana pale mchezaji anapokuwa nje au ndani ya Uwanja .

Makosa atendayo mchezaji anaweza kuonywa kwa kadi ya Njano au Nyekundu na kutolewa nje ya Uwanja. Kwa kawaida makosa yanayoonywa kwa kadi ya manjano ni k**a Vile kushika na Kuunawa mpira bila kukusudia , Kumsukuma mchezaji Wa timu pinzani katika hali ya kutaka kuchukua mpira , Kupoteza muda , Kumvuta au kumshika mchezaji wa timu pinzani wakiwa katika hali ya kucheza mpira .

Makosa ya kadi nyekundu ni k**a vile , Kutukana , Kupigana , Kucheza rafu kwa nyuma , Kukaba kwa nguvu kwa kunyoosha miguu mmoja au yote miwili mbele wakati mchezaji mwingine anataka kupokea mpira au kucheza N.K

Kwa mujibu Wa sheria hii

– Mchezaji atakayeonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja atakosa mechi 3

– Mchezaji atakayeonywa kwa kadi za njano 2 katika mchezo mmoja atatolewa kwa kadi nyekundu na kukosa mchezo 1 .

– Mchezaji akionyeshwa kadi za njano katika michezo 5 ndani la Ligi 1 au mashindano atakosa mechi 1 , kadi 10 atakosa michezo 2 na kadi 15 atakosa michezo 3 .

– Endapo mchezaji atafikisha kadi za njano 20 katika msimu mmoja , basi k**ati ya maadili ya wachezaji itakaa na kuamua adhabu kwa mchezaji huyo .

13. PIGO HURU.

Ni hali ya mwamuzi wa michezo kuamuru mpira upigwe kuelekea upande wa timu ya mtenda makosa .

– Wakati mpira Unapigwa golini , Wachezaji wengine wanatakiwa kuwa katika Umbali Usiopungua mita 9.15 au hatua zisizopungua 10 kutoka pale mpira Ulipo .

14 . PIGO LA PENATI.

Ni kitendo cha mpira kutengwa kwenye Kisanduku cha meta 12 kutoka goli. Pigo la penati linawahusisha wachezaji wawili tu, mpigaji na mlinda mlango na wachezaji wengine wote wanatakiwa kuwa nje ya 18 .

Kuna aina 2 za pigo la penati ambazo ni , Penati ndani ya muda wa mchezo yaani ndani ya dk 90′ na pigo la penati baada ya muda wa mchezo ambalo linalenga kutafuta mshindi wa mchezo Mara baada ya timu zote kutoshana nguvu ndani ya dakika za mchezo.

Mpiga penati ndani ya muda wa mchezo hufanya mambo mawili ambayo ni Kupiga mpira golini moja kwa moja au kumtengea mwenzake aliye nje ya 18 ..mfano mzuri ni Lionel messi na Luis Suarez msimu wa 2015/2016.

– Mpigaji wa penati anaruhusiwa kuucheza tena mpira uliorudi ndani ya Uwanja baada ya mlinda mlango kuucheza na hatoruhusiwa kuucheza endapo Utagonga mlingoti na kurudi Uwanjani .

15. MPIRA WA KURUSHA.

Hutokea pale ambapo timu pinzani watakapokuwa wameutoa .

Hauhusiani na Goal Kick, na Utarushwa kuelekea katika lango la aliyeutoa .

16 . PIGO LA GOLI.

Hii ni Goal Kick, Hutokea endapo timu shambulizi ikatoa au kupaisha Juu au pembeni ya lango shambuliwa .

17. PIGO LA KONA.

Baada ya timu shambuliwa kutoa mpira katika Mstari wa goli lao, timu shambulia hupewa nafasi ya Kupiga Pigo la kona katika timu pinzani ( shambuliwa ) .

Katika upigaji wa kona mchezaji anaweza kupiga moja kwa moja au kuanza kwa Kupasia .

🥚 FAIDA ZA MAYAI KWA MWANAUME 💪🔥Mayai ni moja ya vyakula bora kwa afya ya mwanaume! Hapa kuna sababu kwanini unapaswa ku...
08/05/2025

🥚 FAIDA ZA MAYAI KWA MWANAUME 💪🔥

Mayai ni moja ya vyakula bora kwa afya ya mwanaume! Hapa kuna sababu kwanini unapaswa kuyajumuisha kwenye mlo wako kila siku:

✅ Huongeza Misuli – Mayai yana protini nyingi, inayosaidia kujenga na kurekebisha misuli. 🏋️‍♂️💥

✅ Huimarisha Nguvu za Kiume – Yana vitamini D na cholesterol nzuri, zinazosaidia kuongeza uzalishaji wa testosterone. 🥚🔥

✅ Huimarisha Ubongo – Yana choline, kirutubisho kinachosaidia kuboresha kumbukumbu na umakini. 🧠⚡

✅ Hulinda Moyo – Licha ya imani potofu, mayai yana mafuta mazuri yanayosaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. ❤️🥑

✅ Huimarisha Macho – Yana antioxidants k**a lutein na zeaxanthin, zinazosaidia kulinda macho dhidi ya uharibifu wa mwanga mkali. 👀☀️

🛑 JINSI YA KULA MAYAI KWA AFYA BORA:
🥚 Chemsha badala ya kukaanga
🥚 Kula pamoja na mboga k**a spinach na nyanya
🥚 Usiongeze chumvi nyingi au mafuta mabaya

LEO KTK IFAHAMU AFYA
THABITI

08/05/2025

New Muleba Generation ilifika Shule ya Msingi Kaigara kwa ajiri yakutoa Mchango wao kwa Wale watoto wenye Mahitaji maalumu wanaendelea na Masomo yao.

Hakika Jamii inatuhitaji kufika Pale kadri ya tuwezavyo ili kuwatia Moyo katika masomo yao nakutoa sapport kwenye baadhi ya vitendea kazi ili Vijana hawa waweze kutimiza ndoto zao.

08/05/2025

Hii Shule ya Watoto wenye Mahitaji Maalumu iliyopo Shule ya Msingi Kaigara inaamasisha kuwaleta wale watoto wenye ulemavu ili wapte haki yao ya Msingi.

Akiongeza Mkuu wa Shule alisisitiza hilo jambo maan kuna watu wanaamini kuwa Mtoto uyo hawezi kufika mbali kielimu wala kufanya vizuri katika Masomo yao.

Hivyo tusiwafiche majumbani tuwapeleke watoto wape haki yao Msingi.

Address

Muleba

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when New Muleba Generation posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share