31/08/2024
KUELEKEA DPPJ 2024
Ujumbe Toka Kwa Askofu
New Life Gospel Community Church
Sababu 12 zinazotupa jukumu la kuomba Kwa ajili ya Amani ya Israeli
Kuna sababu nyingi, sababu zisizo na mashaka zipatikanazo katika Biblia. Kimsingi leo tutaona kwa nini tunapaswa kuombea amani ya Israeli na kwa watu waliochaguliwa na Mungu yaani Wayahudi. Sababu ambazo sisi k**a Wakristo hatuwezi kuzipuuza; kwani sababu nyingine zina maana ya unabii.
Sababu 12 zisizokuwa na shaka.
1. Mungu anatuamuru tufanye hivyo. Katika Zaburi 122: 6, Mungu kupitia Daudi anatuambia,"Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao." Yerusalemu haiko Kenya wala Saudi Arabia iko katika Israeli hata k**a kwa hila mtu akipinga.
2. Kwa kufuata mifano ya wengine ambao waliiombea. Zaburi 25:22 inasema, "Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote/shida yake yote." (Soma pia 51: 18-19; 137: 6-7; Rom 10: 1.)
3. Kwa hiyo kwa maombi yako, watu wake watakuwa na amani na mafanikio. Zaburi 122: 8: "Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe.'"
4. Kwa ajili ya wokovu wao. "Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe/kwa ajili ya wokovu wao" (Warumi 10: 1).
5. Kwa sababu wao (Wayahudi) ni watu maalum wa Mungu. Katika Kumbukumbu la Torati 32:10 inasema, Alimkuta katika nchi ya ukame, Na katika jangwa tupu litishalo; Alimzunguka, akamtunza; Akamhifadhi k**a mboni ya jicho;
Tena, katika Kumbukumbu la Torati 14: 2 Mungu anasema juu ya Wayahudi, "Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi."
6. Kuleta agano la Mungu la amani. Ezekieli 37:26 "Tena nitafanya agano la amani pamoja nao; litakuwa agano la milele pamoja nao; nami nitawaweka na kuwazidisha, na patakatifu pangu nitapaweka katikati yao milele."
7. Ili kusudi serikali yake (hasa katika milenia) ipate kuwa serikali ya amani.
Isaya 9: 7 Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Wivu wa Bwana wa majeshi ndio utakaotenda hayo.
8. Kwa sababu ni makazi/maskani ya Mungu wa amani hapa duniani.
Isaya 9: 6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
9. Mungu anaahidi baraka kwa wale wanaowabariki Israeli. Mwanzo 12: 3 Nami nitawabariki wale wanaokubariki, Na mtu atakayekulaani nitamlaani. Na ndani yenu jamaa zote za dunia zitabarikiwa. "(Soma pia Hes. 24: 9; Zab 122: 6).
10. Tumeitwa kuwa watetezi. Mathayo 5: 9 inasema, "Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu."
11.Tumeamriwa kuwa na amani na wote. Warumi 12:18 inasema, "Ikiwezekana, kwa kadiri inategemea wewe, kuwa na amani na watu wote."
12. Sisi kanisa tuna wajibu wa Israeli. Sisi kanisa tuna uhusiano wa kipekee na Israeli. Tumeunganishwa kwenye mzabibu wao na tunapata ahadi zao za kiroho. Kwa hakika tunawajibika kwao (Warumi 11).
KWA NINI LEO TUSIMAME NA ISRAELI?
Israeli ni nchi ambayo kwayo Mungu husema Ki-pekee, Ki-unabii, Ki-ukombozi, na kujirudia katika biblia akisema “Huyu ni Wangu.” Mungu anairejea Israeli kimaelezo tofauti na nchi yoyote duniani. Neno la Mungu lawaita Wayahudi kuwa “shina” na mataifa yanaitwa “Matawi.” Kwa muda tumekumbushwa vivyo “kwa sababu ya kutokuamini, wengine wao walivunjika na mkasimama mahala pao kwa Imani,” Hatustahili kujivunia hili bali tuogope: “Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.” Patakapokamilika uaminifu wa Mataifa, “Hivyo Israeli wote wataokoka.” (mst. 11:16-27)
• Mungu aliwachagua kwa makusudi: “…ambao ni Waisraeli, wenye kule kufanywa wana, na ule utukufu, na maagano, na kupewa torati, na ibada ya Mungu, na ahadi zake; ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.” (Warumi 9:4)
Kimsingi, maandiko husema nasi wazi kabisa: twashughulika na mashina ya kila kitu kinachohusiana na ufunuo wa Mungu kwa binadamu. Uthibitisho wa hili uko katika ule uwepo wa Wayahudi k**a watu na ukweli kwamba wamepata kuponywa k**a taifa. Leo hii mapambano yako juu ya Yerusalemu, dhidi ya Israeli, na kinyume cha uwepo wa Wayahudi na haki yao k**a wengine kuwa na nchi. Yapo mataifa machache yaliyokubali kufanya mafungamano ya kujitoa kusimama na Wayahudi na Israeli, bali Mungu anaahidi kuwaheshimu watakaofanya hivyo.
• Maandiko yanaazimia kuwa, katika roho, unapompokea Bwana, unafanyika kuwa Myahudi (Warumi 2:28-29; Wagalatia 3:26-29).
• Ikiwa wewe ni mwenye kuamini, basi hautashupaza shingo dhidi ya jumla ya maandiko yawahusuyo Wayahudi na Israeli.
• Mambo ya Walawi 25:23 – Nchi ni ya Bwana, na imedhihirishwa kutokupotezwa wala kuuzwa pale asemapo: “Nayo nchi haitauzwa kabisa kabisa; kwani nchi ni yangu mimi;…”
• Kumbukumbu 32:43 – “Furahini, enyi mataifa, pamoja na watu wake;…atafanya kafara kwa nchi yake, na watu wake.”
• 2 Mambo ya Nyakati 7:20 – Mungu anasema kuwa wakiniasi Mimi “…Nitawang’oa katika nchi yangu niliyowapa…”
• Zaburi 85:1-2 – “Bwana umeiridhia (umependelea) nchi yako, umewarejeza mateka wa Yakobo (Israeli). Umeusahau uovu wa watu wako, umezisitiri hatia (Dhambi) zao zote.”
• Isaya 8:8 – Nchi hii ni milki ya Baba Mungu na ni nchi ya Masihi wake: “…na kule kuyanyoosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli.”
• Yeremia 2:7 – Bwana anawaambia watu kwa nini patatokea upotevu, kuangamia kwa mji wa Yerusalemu. “Nami nikawatia katika nchi ya shibe…lakini ninyi mlipoingia katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo.”
• Ezekieli 38:16 – Mungu anasema na watu wa nyakati za mwisho watakaoinuka kinyume na Israeli. Mungu anasema juu ya majibizano yatakayofanyika katika nchi yake. “Nawe utapanda juu uwajilie watu wangu, Israeli,….nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kwako…”
• Yoeli 1:6, 2:18, 3:2 – Mara tatu katika kitabu hiki, nchi inarejewa k**a milki ya Bwana. “Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu…” (1:6) “Hapo ndipo Bwana alipoona wivu kwa ajili ya nchi yake…” (2:18) “Nitakusanya mataifa yote, nami nitawaleta chini katika bonde la Yehoshafati, na huko nitawahukumu kwa ajili ya watu wangu, kwa ajili ya urithi wangu Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kuigawanya nchi yangu.” (3:2)
• Hosea 9:3 – Hili linarejea katika kutawanyika kwa Israeli: “Hawatakaa katika nchi ya Bwana; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula kinajisi katika Ashuru.”
• Zekaria 9:16 – “Na Bwana, Mungu wao, atawaokoa siku hiyo, k**a kundi la watu wake; kwa maana watakuwa k**a vito vya taji, vikainuliwa k**a Bendera juu ya nchi yake…”
Tunapozungumzia kuihusu Israeli, tunakabiliana na: 1) Kipande cha mali ambacho Mungu amekifanyia agizo kukihusu 2) Watu wa Mungu waliopewa nchi.
Ni jambo kubwa kwake yeye aliye muumba wa vyote, hili halina mjadala. Mambo ambayo Mungu ameyasema, kipekee, kuihusu Israeli hayajawahi kubatilishwa.
• Siyo tu kwamba nchi ni milki ya Mungu, lakini pia Mungu amemkabidhi Abraham nchi, kupitia kwa uzao wa Isaka, siyo kwa muda, bali kapewa milele. (Mwanzo 17:7-8)
• “Kwa kitambo kidogo nimekuacha (nimekuficha uso wangu)…lakini, kwa fadhili za milele nitakurehemu, wala agano langu la Amani halitaondolewa…” (Isaya 54:8-10)
• Upotevu wa Israeli kutawaliwa kutokana na dhambi na kutawanyika kwao hakujauondolea mbali msimamo wa maagano ya Mungu ya milele (Ezekieli 37:1-28)
Bishop Daniel & Debra Ouma
Bonde la Baraka - Musoma