05/08/2020
Mlipuko mkubwa umetokea katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut, Agosti 4,2020.
Salamu za rambi rambi kwa watu wa Lebanon zimetumwa kutoka sehemu mbali mbali Duniani, ikiwemo jirani zake Israel ambao walisema haraka kwamba hawajahusika na mlipuko huo
Rais wa Lebanon, Michel Aoun anatoa wito kwa baraza la mawaziri kutangaza wiki mbili za hali ya dharura ya kitaifa huko Beirut baada ya mlipuko mkubwa mapema Jumanne ulioharibu sehemu kubwa ya bandari ya mji huo na kuuwa angalau watu 70 na kuwajeruhi zaidi ya 3,500.
Japokuwa chanzo rasmi cha mlipuko huo hakijulikani, Aoun aliandika kwenye mtandao kwamba sitapumzika hadi tunampata mtu aliyehusika na kile kilichotokea na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria na kumhukumu