
16/09/2025
Ameandika ✍️ BIN KAZUMARI MTIPA
FT: Yanga 1-0 Simba.
Mnyama kafa mara 6 mfululizo, walichofanikiwa leo ni walau kuonyesha wamefungwa lakini Yanga hawakuwa so dominant, vinginevyo wana safari ndefu dhidi ya Yanga na hawa akina KANTE wao, labda wapate wakina DE.REUICK 5 ndo watawafunga Yanga.
Bado Yanga ni imara mbele ya Simba hata k**a siku hiyo hawakutawala mchezo ila wanauwezo wa kushinda, maana yake bado Yanga watatawala ligi tena na ile ahadi ya ubingwa mara 10 mfululizo ISIDHARAULIKE.
Mohamed Mkono Mwamuzi msaidizi namba 1 wa mchezo wa leo ambaye ni FIFA referee AMEWAUA Simba, ile ni OFFSIDE kabisa, hakupaswa kuruhusu lile bao. Pacome alikuwa offside position akaja kufanya obstruction kwa De.REUICK ambaye alikuwa anamkimbiza Max, Kisha akaukuta mpira akafunga, kufanya obstruction ukitoka kwenye offside position ni KOSA na Mkono anajua hilo.