25/07/2022
‘Barbershop,’ ambazo mbali na kuwanyoa nywele kichwani wateja, pia huwasinga sehemu mbalimbali za mwili (massage).
Mwandishi wa habari hii amefuatatilia huduma hiyo kwa siku kadhaa katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.
Awali, akizungumza na mwandishi kuhusu yanayotendeka ndani ya saluni za kisasa, Israel Joachim anasema, “niliwahi kwenda saluni, lengo halikuwa kunyoa nywele, bali nifanyiwe ‘massage,’ kweli nilifanyiwa tena na msichana, haikuwa rahisi kuvumilia, kuna maeneo hatarishi nilikuwa nashikwa na huyo dada akaniambia k**a hali ni mbaya nijiongeze.”
Anasema baada ya kuingia kwenye saluni hizo kupata huduma, alichokutana nacho, hakimtoki kichwani kwa kuwa mbali na kulainisha misuli na kupunguza uchovu, vyumba vilivyomo saluni vina ushetani mwingi.
“Nilijiuliza nijiongeze na nini, kumbe alitaka (mtoa huduma mwanamke) nimpatie Sh30,000 anisaidie kuondoa hali niliyokuwa nayo, sikuwa na ujanja, nilitekeleza takwa lake sababu sikuwa na la kufanya kutokana na hali yangu,” anasema Joachim.
Hata hivyo, Mwandishi alibaini baadhi ya vyumba hivyo ni kichaka kipya cha biashara ya ngono na inaelezwa asilimia 80 hadi 90 ya wanaume wanaokwenda huko hufuata huduma hiyo ya ngono, ingawa huzuga kwa kuanza kwanza na huduma ya ‘massage.
“Wanaanza na huduma ya kwanza kwa sababu ile ya pili hawana uhakika k**a inatolewa pale, kwa baadhi ya watu niliowauliza kwa nini wanakwenda kule wanasema wale wanawake wanaotoa huduma hizo wana uwezo mkubwa wa kuwaandaa wanaume kushiriki ngono,” alisema Ramadhani Masenga, mtaalamu wa saikolojia kutoka Mental Health Hygiene Institute ya Dar es Salaam.