Sauti Ya Mwandishi

Sauti Ya Mwandishi Maoni ya Mwandishi juu ya hisia za jamii Africa

Ooh my God!   Christine Mboma malkia wa Namibia. Mwaka 2021 ulikuwa mwaka wa furaha sana kwake pale alipovunja rekodi ya...
18/04/2024

Ooh my God! Christine Mboma malkia wa Namibia.

Mwaka 2021 ulikuwa mwaka wa furaha sana kwake pale alipovunja rekodi ya mwanadada mwenye umri mdogo kushinda mbio za olimpiki ulimwenguni na kubadili historia ya familia yake.

Kuanzia hapo maisha yake yalibadilika na kuwa yenye furaha tele kwa sababu aliuaga umasikini ulio itesa familia yake kwa kipindi kirefu. Mboma ambaye ni mtoto wa pekee katika uzazi wa mama yake aliishi maisha duni akiwa anaishi na mjomba,pia na bibi ake sehemu moja hali hii ili tokea mara baada ya mama ake kufariki na kumuacha mpweke bila malezi yake .

Licha ya mafanikio ya mboma na kuwa mkombozi wa familia yake, amakweli mbuzi wa masikini hazai , niseme historia ya malkia huyu imebeba maumivu na machungu mengi ya wadada wa Afrika .

Christine Mboma inasemekana kuwa hakutakiwa kukimbia tena mbio za kulipwa hususani mbio za mita 400 na maili moja, hii ni kutokana na kusadikika kuwa na home nyingi za testosterone.

Hivyo basi Christine mbona ili kuweza kunusuru kipaji chake amelazimika kukubali masharti ya kupunguzwa kwa home hizo za kiume. Ripoti iliyotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, hii leo Mboma amerejea tena katika mchezo wa riadha mara baada ya kukaa nje ya mchezo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Nikiwa k**a muumini wa michezo, na mzalendo wa bara langu la Afrika naona kuwa kitu kilichofanya na mamlaka za mchezo wa riadha siyo sawa, kwanza kinakinzana na sheria ya asili ya uumbaji ya mwenyezi Mungu kwani si kwa matakwa ya mtu binafsi juu ya kuwa na homoni pungufu au zaidi, lakini pia kilichofanywa na mamlaka ya mchezo wa riadha ni ukatili wa kijinsi kwani mamlaka hizo zimefanya ubaguzi juu ya jinsi ya mtu jambo ambalo siyo sawa kabisa.

Yote hayo ni kutokana na bara letu la Afrika kukosa watetezi katika mamlaka mbalimbali za ulimwengu kwani sheria hizi nik**a zipo ili kuwakandamiza zaidi watu weusi.

God bless Africa God bless Tanzania.

Mmmh! K**a kawaida sisi k**a Mataifa ya kimaskini lakini jeuri tunaomba tuwe wa mwisho katika hili maana ata kula yetu t...
18/04/2024

Mmmh! K**a kawaida sisi k**a Mataifa ya kimaskini lakini jeuri tunaomba tuwe wa mwisho katika hili maana ata kula yetu tu shughuli sembuse usafiri wa kijani ?

Mtandao bora wa marafikiMarafiki nijumla ya watu tunao kumbana nao katika harakati za kimaisha, watu hawa wanaweza kuwa ...
15/04/2024

Mtandao bora wa marafiki
Marafiki nijumla ya watu tunao kumbana nao katika harakati za kimaisha, watu hawa wanaweza kuwa wenye umri wa kutuzidi, kuwazidi au tukawa sawa.

Ni wazi kuwa wengi wetu tumefika hapa tulipo kutokana na nguvu ya marafiki tulio Kutana nao katika mazingira tofauti tofauti yaweza kuwa kipindi tuko shule,chuoni na kadhalika. Mchango wa marafiki umekuwa mkubwa sana katika kufikia ndoto zetu kwa sababu wengi wetu tumetokea familia zenye maisha ya chini kabisa ambapo mzazi hawezi ata kwenda kutoa au kuweka pesa bank hivyo tumekuwa tukitegeme marafiki kuishi ndoto zetu.

Mabibi na mabwana, natambua kuwa mara ilipo fika karne ya ishirini na moja (21c) hali imebadilika sana imekuwa ni vigumu sana kumtambua rafiki wa kweli na yule wa uongo na matokeo yake imekuwa ni kutapeliwa na kupotezeana dira ya maisha.

Kwa kulitambua hilo naomba ni changie kwako juu ya aina za marafiki ambao wanaweza kuwa sahihi kwako hivyo kuambatana nao katika safari hii ya kupambana na vita ngumu ya maisha.

Moja ya marafiki bora kabisa wa kuwa nao ni marafiki wasikivu, hawa ni wale ambao wako tayari kukusikiliza kipindi uko katika mood isiyo ya kawaida hivyo hukupa nafasi ya kukusikiliza mpaka pale utakapo kuwa sawa pasina kujarisha kuwa sinario unayomueleza ameipenda au hajaipenda. Watu hawa ni wamuhimu sana kwetu kwa sababu wanadamu hupitia katika vipindi ambavyo huwa vigumu sana kuvivumilia na kuvibeba katika mioyo yetu hivyo hurazimika tuviseme ili tuwe huru. Katika maisha ni lazima tuwe na marafiki ambao wapo tayari kutusikiliza, kwa asilimia kubwa wenza wa ndoa au watu walio katika mahusiano huangukia katika kundi hili la marafiki.

Lakini pia ni lazima katika maisha uwe na rafiki mshauri, hawa ni marafiki ambao hawako tayari kuvumilia mwenendo mbaya unao upitia, yuko radhi kuacha kila kitu ila akueleze juu ya hali halisi ya mtindo unao ufanya. Wazazi wetu kwa asilimia kubwa huangukia katika kundi hili la marafiki.

Tatu, ni marafiki wanao kupa changamoto, mabibi na mabwana ni wazi kuwa watu wengi tumekuwa walevi wa sifa, hata kwa kufanya kitu ambacho hakina masla mapana kwa wengine tumekuwa tukihitaji kusifiwa na kupongezwa, hii siyo sawa kabisa. Sasa aina hii ya marafiki ni wale ambao hukupa cha ngamoto kwa nia ya kukufanya ufikiri kwa mapana ili kufikia ndoto yako yani yupo tayari kukukosoa kwa jambo ambalo wakati mwingine umerifanya kwa kiwango kizuri kabisa ili mradi uongeze juhudi na ubunifu zaidi katika utendaji wako.NB aina hii ya marafiki haifanani na wale wanao kuponda kwa kukuonea wivu kwa mafanikio yako hapana.

Nne,ni aina ya marafiki ambao wao hupenda kushiriki kikamilifu ili kutimiza malengo ya kundi au taasisi kwa ujumla, hawa mda wote wanakuwa busy kuhamasisha wenzao kuchangia mchango au maoni katika vikao kadha wa kadha vinavyo husu maslahi ya wengi. Watu hawa husifika kwa.kujali sana wenzao na mda mwingine hutumika k**a chachu ya kundi, ndio wale wasipo kuwepo katika discussion siku hiyo zoezi linastishwa. Nao jitahidi sana kuwa nao katika maisha watakusaidia sana.

Mwisho ila kwa Umuhimu napenda kutumia fursa hii kukusihi kujenga mtandao sahihi ili kufikia malengo malengo yako kwa sababu huwezi kufika mbali bila kuwa na marafiki sahihi, lakini pia jitahidi kujenga mazoea ya kupata marafiki wapya kila unapopiga hatua moja kwenda nyingine epuka sana kumantain marafiki kila unapo anza lengo mpya

Hataivo kwa undani wa jambo hili la marafiki jitahidi kutafuta kitabu cha Joel Nanauka kiitwacho "Jinsi ya kutengeneza mtandao wa marafiki utakao kusaidia kutimiza malengo yako kwa kasi" utajifunza mengi zaidi kuhusu marafiki nk.

Mimi ni Raymond Elgius unaweza kunipatia kwa jina hilo katika mtandao wa instagram.

Asante & see you next.

Ujinga wa karine hii ya 21 siyo kutokujua kusoma na kuandika hapana ila  nikutokutaka kujifunza, kujifunza na kujifunza ...
11/04/2024

Ujinga wa karine hii ya 21 siyo kutokujua kusoma na kuandika hapana ila nikutokutaka kujifunza, kujifunza na kujifunza tena. Mabibi na mabwana make sure unasoma angalau vitabu kumi na mbili kwa mwaka ama hakika utakuwa umeisha sana.

WINNING WITH PEOPLE Hapo chini ni cover ya kitabu mahususi kabisa kwaajili ya kuchechemua hisia za ushirikiano baina ya ...
11/04/2024

WINNING WITH PEOPLE
Hapo chini ni cover ya kitabu mahususi kabisa kwaajili ya kuchechemua hisia za ushirikiano baina ya watu. Kitabu hiki ni chemistry ya vitabu viwili ndani ya kitabukimoja yani Volume 1 na Volume 2. Mwandishi ni John Maxwell mwalimu na mshauri wa mambo mbalimbali ya kijamii kiuchumi na kisiasa, na ndio maana jamaa ana kitabu kingine kinachoelezea namna ya kuwa kiongozi bora. Ukihitaji mwendo ni uleule tuma request kwa normal text kupitia nambari 061 2680 598 mimi nitakudondeshea bila kuchelewa.

Licha ya hayo yote kwa mtu ambaye ameshakisoma chote bila shaka aligundua kuwa mchanyiko wa vitabu hivi viwili amakwahikika vimwana vizuri Ani huwezi kujua kwamba hiki ni chakwanza na hiki ni cha pili. Kitabu cha kwanza ni THE 17 INDISPUTABLE LAW OF TEAM WORK cha mwaka 2001 chapili ni WINNING WITH PEOPLE Cha mwaka 2004.

Hii leo nitajikita kueleza juu ya kitabu cha pili cha WINNING WITH PEOPLE (2004).

Winning with people nikitabu kinachokazia sana suala la ushirikiano miongoni mwa watu katika jamii zaidi ikiwa ni kwa wale wenye common interests kwa mfano. Wafanyakazi wa kampuni moja, Team za mpira familia nakadhalika.

Na hapa ndipo utaweza kugundua changamoto inayo zisumbuaga team nyingi za mpira wa miguu Duniani,

Ndani ya kitabu hiki kimeunganishwa na sheria 17 zile za kitabu cha kwanza yani Volume 1 ya mwaka 2001 ili kuweza kuonyesha vile mambo yanapaswa kuwa ili kupata matokeo yanayo tegemewa na kampuni au taasisi yoyote ile hapa Duniani.

Hapa chini nitaeleza sheria ya kwanza ya kushinda na watu mpaka ya tatu lakini zingne nitakubembeleza kwa Lugha ya upendo ili na wewe ukafaidike k**a Mimi na hii ndiyo maana halisi ya WINNING WITH PEOPLE.

1.The law of significance, sheria hii ina sema kwamba "one is too small number to achieve greatness".kwa tafsiri rasmi ni kwamba, moja ni namba ndogo kabisa ili kuweza kufikia mafanikio.

Hiyo ina maana gani?, Ukweli ni kwamba watu wengi tunamjua christian Ronald, Lionel Messi, Zitto Zuberi kabwe, Mack Zuckerberg, Elon musk, Diamond platinumz na wengine wengi ambao hata sijawataja hapa kuwa watu walio fanikiwa zaidi katika taaluma zao si ndio....? Lakini ni lazima tukumbuke kwamba kidole kimoja hakivunji chawa kwahiyo hakuna mtu yeyote hapa duniani anaweza kusimama na kupambana mwenye kufikia malengo makubwa ni lazima kuwa kila mtu mwenye mafanikio makubwa nyuma yake kuna timu kubwa ya watu wanao msapoti na kuonekana mwenye mafanikio zaidi mbele ya watu.

2. Sheria ya pili ni, The law of a big picture, sheria hii inasema kuwa " The goal is more important than the role" sheria hii inanikumbusha simulizi ya maana riadha mmoja Raia wa Tanzania ambaye alikuwa na malengo makubwa ya kuwa mahindi katika mashindano ya riadha yaliyo fanyika nchini japani, ilistaajabisha sana siku kwanza hakuwa kipaumbele cha mwalimu hivyo alienda tu kwa kujaza nafasi ya ziada iliyo tangazwa na mamlaka hivyo hakuwa amejianda vilivyo katika mashindano yale.

Inshu nikujianda ! Siku zote mtu mwenye big picture ya kile anachokifanya huwa na malengo makubwa na matarajio makubwa zaidi kuliko kile anachokifanya, yani mkulima wa zao la Michikichi hupanga kuzalisha zaidi ya bidhaa moja ndani zao moja la mchikichi hapa ata pata mafuta ya kupikia (mawese), atapata mafuta ya mise kwaajili ya kuzalisha sabuni za mawingu, atapata kuni za kupikia maafa baada ya kuvuna zao lile, atapata pesa ya ada nk.

Hivyo vivyo, kwa mama mjamzito huwa na picha kubwa ya kumpata mtoto kuliko maumivu ya uchungu wakati wa kujifungua atafanya hivyo zaidi ya mara tano katika maisha yake. Swali kubwa ni kwamba Kwanini akubari kubeba mimba wakati kuna maumivu yanayo sadikika kuwa Makari zaidi kuwahi kutokea hapa Duniani?
Jibu ni The law of big picture.
Malengo ni makubwa zaidi kuliko mchakato wa kujifungua.

3. Sheria ya tatu ni, The law of the niche, sheria hii inasema kwamba " All player have a place where they add the most value"

Kiukweli sheria hii inagusa maisha yetu moja kwa moja katika jamii zetu kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa, awali ya yote kumbuka wakati upo mdogo katika familia yenu pengine ulikuwa mtu ambaye hukuwa unadhaniwa k**a ungekuwa hapo ulipo aliyekuwa anadhani wa May be ni kaka ako mkubwa au yule mdogo wako anaye kufuata hii yote ni kutokana na jamii zetu kufremiwa katika Angle moja ya dunia na kusahau kuwa unaweza kufanikiwa katika Angle nyingine kabisa labda kupitia Muziki, kucheza mpira, kudance au ujasiriamali.

Ninachotaka kusema ni kwamba, kila mtu anakipaji chake. Yani kila mtu kunakitu ambacho anaweza kukifanya zaidi kuliko mwenzake iwe katika kampuni, familia, baraza, bungeni, ikuru au hata kule kwenye idara za ulinzi na usalama, na ndio maana kuna vitengo tofauti tofauti katika maisha na siyo kila sehemu kila mtu anaweza kufiti No. Mfano mimi niko vizuri katika suala la mawasiliano katika kampuni na taasisi kuliko mtu mwingine yeyote , hivyo siwezi kufanya vizuri zaidi ikiwa nitafanya majukumu ya kufanya upelelezi wa masoko (market intelligence).
Hivyo ni bora kutambua kuwa hakuna mtu yeyote yule asiye kuwa na thamani ndani ya kampuni yako au katika taasisi yako na ndio maana teuzi nyingi za serikali huenda kwa connection, na kuishia kuibua taaruki ndani ya jamii wafu wengi wa kinung'unika kuto kuzingatiwa na kuonekana k**a wamesahaurika, shida ni kutokutamburika kwa thamani yako katika serikali.

Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu ni kuombe sasa uchukue mda wako wa thamani kwa kufanya jambo la thamani zaidi, la kumalizia sheria hizi adhimu zilizo bakia kma unahitaji kuwa na thamani zaidi katika kazi yako na utakuja kunishukuru baadaye. Yapo mengi sana ndani ya kitabu hiki ambayo yataongeza thamani ya maisha.

Cha kufanya tuma ujumbe wa kuhitaji soft copy ya kitabu hiki na mimi ni takutumi bila kuchelewa, cha msingi fanya kunichek kwa 061 268 059 8 au kwa watsap namba 0624004071.

Insta Raymond Elgius.
All the Best.

ISHI NDOTO YAKOIshi ndoto yako ni miongoni mwao vitabu vyenye nguvu zaidi ya kumfanya mtu kuamka na kuchechemua akili ya...
10/04/2024

ISHI NDOTO YAKO

Ishi ndoto yako ni miongoni mwao vitabu vyenye nguvu zaidi ya kumfanya mtu kuamka na kuchechemua akili yake hususani kwa mtu aliye poteza mwelekeo wa maisha.

Kitabu hiki kimeandikwa na kijana mwenye ushawishi mkubwa hapa nchini Mr Joel Nanauka ambaye amejizolea umaarufu kutokana na mafundisho yake katika mitandao ya kijamii hususan YouTube juu ya mambo mbalimbali yanayo husiana na maisha,

Ishi Ndoto yako nikitabu ambacho binafsi kimenifanya kupata tumaini jipya la maisha zaidi kuhusu namna ya kutumia kipawa changu kupambana na changamoto za maisha na jamii kwa ujumla

Moja ya mafunzo makubwa ndani ya kitabu hiki ni ;-

1. Kupandikiza roho ya kutokukata tamaa ndani yetu
Joel ameweza kuonyesha Watu wakubwa na maarufu Duniani ambao maisha yao mwanzo wengi wao yalikuwa k**a yetu tu lakini kutokana na juhudi na mbinu mbalimbali waliweza kushinda vita ya maisha wengine katika umri wa kustaafu kabsa, kwaiyo kitabu hiki ni misaada na siraha hatari ya kushinda vita kuu ya maisha

2. Jinsi ya kutumia kipaji chako
Kuna msemo maarufu wa waswahili usemao " Mungu fundi bana" Swadatah! Kabisa Mungu ni fundi kweli kweli alimuumba mwanadamu katika namna ya pekee kabisa zaidi alimpa nguvu kubwa ya kuweza kushinda changamoto za aina yoyote ile atakayo kumbana nayo sehemu yoyote nguvu hii ni KIPAJI. Kila mtu anakipaji chake cha ajabu watu wengi wanaonekana kushindwa kutambua vipawa vyao.

K**a nawewe unayesoma makala hii ni miongoni mwao basi tafuta kitabu hiki cha ishi ndoto yako cha Joel Nanauka kitakusaidia na utakuja kunishukuru baadaye.

3. Jinsi ya kuishi na wakuu mbalimbali katika mazingira ya kazi yako.
Watu wengi wamekuwa wakishindwa kulinda kazi zao katika Makampuni flani flani walipo ajiliwa ikiwa ni kutokana na kukutana na waajili ambao ni kauzu kweli kweli. Lakini waswahili husema " kila jaribu lina mlango wa kutokea" sasa kwa changamoto k**a hizo na nyingine nyingi kitabu hiki cha kijana huyu msomi (Joel Nanauka) hakika ni mlango sahihi wa kutokea.

Mimi kimenisaidia sana, ni matumaini yangu na wewe kitakusaidia ishallah!

K**a uko huwezi kukipata madukani basi mimi nitakutumia soft copy yake kwa namba hii ya watsap dhumuni ikiwa ni kujenga jamii iliyo bora zaidi. 06 24004 071 .

Au unicheki kwa sms ya kawaida tu ! 06 1268 0598.
Unaweza kunifollow inst kma Raymond Elgius.

DAMU, MABUSU & MACHOZIHiki ni moja ya kitabu chenye stori nzuri ya mapenzi kuwahi kuonekana. Kitabu kina husu story ya b...
09/04/2024

DAMU, MABUSU & MACHOZI
Hiki ni moja ya kitabu chenye stori nzuri ya mapenzi kuwahi kuonekana. Kitabu kina husu story ya baba mmoja tajiri wa bagamoyo , mzee huyu alikuwa kauzu sana hakupenda vijana wa mtaani kumsigerea binti yake wapeke aliye itwa Nancy.

Nancy alikuwa msichana mrembo mithili ya Derilah wa Samsoni na kufanya wavulana wengi kuvutiwa naye kimapenzi hata kuishi naye k**a mke sasa kitendawili kilikuwa namna ya kuweza kumpa mrembo huyu wa geti kari.

Mzee katobe ambaye ni baba Mzazi wa Nancy hakuona ajabu kumuachia mbwa wake mkari kwa boy yoyote atakaye onekana mitaa yake akimfukuzia mwanae.

Licha ya ukari wote huu wa mzee Katobe Nancy alizama katika huba na kijana Tony mpka kufikia hatua ya kuapishiana kiapo cha Yamini siku Mashikaji alipotaka kuondoka China kimasomo ili kwamba asiweze kumsaliti.

Ila mapenzi bana ............any way ebu request soft copy ya kitabu hiki free kabisa kwa namba hii ya watsap 0624004071

Inst Raymond Elgius.

18/03/2024

Begin to the end !
"Uliza maana"
Every thing it will be good for you.

11/03/2024

Kiwango cha akili kilichotumika kutenda matatizo hakiwezi tumika kuyatatua.
Jifunze kutafuta ushauri kwa wanao kuzidi!

10/03/2024

UKIWEZA KUZITUMIA 4R ZA DKT SAMIA KILA SEHEMU UTAISHI.

06/03/2024

MAMBO MATATU YANAYO SUMBUA ULIMWENGU
1.Mabadiliko ya tabia ya nchi
2. Vita vya ukrain na irudi
3. Magonjwa k**a Corona ni.

04/03/2024

Tunapo watia moyo wengine kuelewa na kuthamini ushirikishwaji wa wanawake, tunatengeneza ulimwengu bora....

Address

Kirumba Road
Mwanza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sauti Ya Mwandishi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share