10/01/2021
SOMO:ONDOA VIZUIZI
2) Mipaka ya kibinadamu (udhaifu)
Kutoka 4:10 " Musa akamwambia Bwana Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito. "
Udhaifu unaoujua na usioujua unaweza kuwa kizuizi kwako, na kizuizi kinakunyima uwezo wa kujua na namna ya wewe kumuamini Mungu.
Neno la Mungu likiwa taa/nuru ndani yako linakuonyesha udhaifu ulionao. Tambua kwanza udhaifu ulionao na kisha utambue nguvu ya Mungu ndipo Mungu ataweza kuuondoa udhaifu huo.
Kulijua neno sio kujua mistari ya biblia bali ni kuliishi neno.
Unapokuwa katika kizuizi hiki cha mipaka ya kibinadamu muda wote unawaza ni nani atakuletea. K**a unapenda sana kulala ujue kuwa wewe ni mvivu.
3) Mambo yaliyopita (mambo ya nyuma)
Mwanzo 11:26-32 " Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani."
Inawezekana kabisa mambo yaliyopita yakawa kizuizi kwako kwasababu ya mambo maovu. Acha mambo maovu na uamue kutembea na Mungu.
Unaweza kusema kuwa wewe haupo huko lakini ni mpaka uamue kutoka hapo na kweli ya Mungu iwe na wewe ndipo utaweza kusonga mbele.
4) Kizuizi cha mipaka unayojiwekea wewe mwenyewe.
Kizuizi hiki kina vipengele viwili
a) Mawazo yako
Zaburi 19:14 " Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu."
K**a wewe unajiwazia vibaya ndilo litakalopata kibali mbele za Mungu. Mfano unajiwazia kushindwa ndilo litakalopata kibali mbele za Mungu. Unapowaza mawazo mazuri panakuwepo na amani.
K**a kuna kitu cha kumwambia Mungu mwambie akili yake ikae na wewe maana akili yako ikiwa na akili ya Mungu mawazo yako yatakuwa ya kimungu na ukiwa na akili ya kibinadamu siku zote utawaza mambo mabaya tu.
b) Maneno ya kinywa chako
Ili maneno yako yasiwe na kizuizi wewe angalia neno la Mungu linasema nini na sio maneno yako.
Mwenye kuondoa kizuizi ni wewe mwenyewe, hivyo jitamkie vizuri, jiwazie vizuri juu ya alichosema Mungu kwenye neno lake.