03/09/2026
Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania (ATCL) imetangaza kusitisha kwa muda safari zake za ndege kwenda nchini Urusi uamuzi huo umeanza kutekelezwa rasmi kuanzia tarehe 04 Septemba mpaka taarifa ya kurejesha huduma itakaporejeshwa.
Safari hizo zilizosimamishwa ni zile zilizokuwa zikihusisha namba za ndege za TC422 na TC423.Hatua hii inahusu usafiri uliokuwa ukifanyika kati ya Dar es Salaam na Moscow.Sababu kuu ya kusitishwa kwa safari hizi ni kufanyika kwa tathmini ya kiusalama.
Tathmini hiyo inalenga kuangalia kwa karibu mazingira halisi ya uendeshaji wa ndege hizo,iongozi wa shirika wamesema usalama wa abiria na wafanyakazi unapewa kipaumbele cha juu.Hivyo, uamuzi huu ulichukuliwa ili kuepusha hatari zozote zinazoweza kujitokeza angani.
Abiria wote walioathiriwa na mabadiliko haya watapewa huduma stahiki bila usumbufu mkubwa,Watakaopenda wanaweza kupata marejesho kamili ya fedha zao za tiketi walizolipa.Pia, wateja wanaruhusiwa kubadilisha tarehe za safari zao kwa kadri watakavyohitaji.
Shirika litaendelea kutoa taarifa rasmi pindi safari hizo zitakapopangiwa kuanza tena.
Follow Us On Social Media
Instagram - Jembe Fm
Facebook - Jembe Fm
X(Twitter) - Jembe Fm
TikTok - Jembe Fm
Thread - Jembe Fm