30/08/2022
*RC MALIMA ATAKA KIGHEI COMPANY KUONGEZA UZALISHAJI WA BIDHAA ZA NGOZI ILI KUPUNGUZA GHARAMA ZA UTENGENEZAJI WA VIATU VYA NGOZI KWAAJILI YA FAMILIA ZENYE KIPATO DUNI*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amepongeza kazi zinazofanywa na Kwenye uzinduzi wa maonesho ya Biashara ya 17 Afrika Mashariki yanayoandaliawa na *TCCIA* Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Mkoa wa Mwanza Viwanja vya NYamagana alipotembelea Banda la Konzi la Moyo TV Show.
Mhe. Malima amesema viatu vya Kighei Company Limited vina ubora hivyo ipo haja ikaongeza uzalishaji wake ili kuweza kupunguza bei ya bidhaa zake ili kuwafikia jamii kubwa yenye pato duni. Kadharika Mhe Malima akiwa bandani hapo hapo alipata Fursa ya kufikisha ujumbe kwa Jamii kupitia bango maalum na amepongeza Konzi la Moyo TV Show kuwa Vinara kwenye Dhamira ya dhati ya kutokomeza ukatili.
Naye Mkurugenzi wa Konzi La Moyo TV Show Bi. Florah Magabe amesema kipindi hicho ni matunda ya utafiti uliofanya na Yeye kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge Jimbo la NYamagana iliyobaini Kati ya wanafunzi 10 Sita Kati Yao ni Wahanga a wa ukatili. Hivyo kwa Sasa inatekeleza Miradi mitatu ikiwemo ugawaji wa Viatu vya ngozi pamoja na TAULO za k**e kwa Wanafunzi wanaotoka Katika familia zenye kipato duni. Uzalishaji wa Vipindi vyenye maudhui ya Kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwemo mkakati maalum wa Hamasa ya matumizi ya namba 116 inayoratibiwa na TAMISEMI sanjari na kutoa ushauri nasaha BURE.
Mhe Malima aliambatana na k**ati ya ulinzi na usalama Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Bi. Amina Makilagi. MAKAMU wa Rais TTCIA, Mwenyekiti wa TCCIA Mwanza Robert Mugini Chacha Kinene, Mwenyekiti UWT Mkoa wa Mwanza Bi. Ellen Bogohe. Maonesho hayo yaliyaanza tarehe 26.08.2022 yamezinduliwa tarehe 29.08.2022 yanatahitimishwa tarehe 04.09.2022.
Like
Share
Subscribe
*KM TV*
*Konzi La Moyo TV Show*