27/10/2025
USIDANGANYIKE, HAKUNA ALICHOSAHAU BUNGENI.
Baba Levo amehitimisha kampeni zake leo kwa mkutano mkubwa, mkutano wa kihistoria na inaweza isivunjwe hivi karibuni.
Mwanasiasa wa kwanza kuujaza uwanja wa Kawawa, sio mwanasiasa tuu ila mwana Ccm.
Kesho ni mapumziko, wapiga kura kutafakari na kuchagua hatma yao, watoto wao na kizazi kijacho kisha kesho kutwa ni kufanya kile tulichokitafakari.
K**a mpiga kura wa Kigoma Mjini sina haja ya kujiuma uma kura yangu ni kwa Baba Levo. Nina kila sababu na hii ni kulingana na aina mpya ya siasa duniani.
Zitto miaka 15 ilimtosha kufanya kila alichotaka kufanya, nini alisahau kufanya? Mtu ameingia bungeni akiwa 25 leo ana 45+ bado tu hataki kuridhika?
Miaka 15 ya utumishi wa Zitto kashindwa kununua japo ambulance au kununua vitanda mahospital. Ukigusa hapa anakwambia kazi ya mbunge ni kutunga sheria. Basi atuambie sheria gani alitunga ikamuinua mkazi wa Kigoma.
Tunahitaji mbunge asiyeona aibu kuwekeza Kigoma, Mbunge atakaye empower watu wa Kigoma kwa namna tofauti tofauti.
Ukipiga kura ya udini, basi mtuonyeshe yule bwana akienda msikitini kuswali ili uhadaike na uislam wake. Tupige kura kwa maendeleo ya mji wetu sio kwa sifa ya dalali mmoja.
Elimu aliyonayo imesaidia vipi majimbo aliyoongoza na mkoja kwa ujumla? Kawainua wangapi kielimu maana tulimpa nafasi ya kutusemea huku akinufaika kiuchumi.
Tarehe 29 ni siku ya kuamua mustakabali wa mji wetu kwa miaka mitano ijayo.
@
Follow GOOD ONE TV