31/08/2026
:Lionel Messi ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Argentina baada ya miaka 20 ya kuitumikia nchi yake.
Messi amecheza jumla ya michezo 207, akifunga mabao 125 na kutoa asisti 68 akiwa na Argentina
Katika kipindi chake na timu hiyo, Messi ameshinda Kombe la Dunia 2022, pamoja na Copa América mara mbili. Pia amefika fainali ya Kombe la Dunia 2026.
Ni mwisho wa safari ya kipekee kwa Messi akiwa mmoja wa wachezaji walioacha historia kubwa katika timu ya taifa ya Argentina.
| Follow us