31/03/2026
Vijana Njombe Waomba Kuthaminiwa na Kuwezeshwa Zaidi
Vijana katika Wilaya ya Njombe wameeleza haja ya kutambuliwa na kuthaminiwa k**a nguvu muhimu ya maendeleo ya sasa na ya baadaye. Wamesema kuwa mchango wao katika jamii ni mkubwa, hivyo wanastahili kupewa nafasi zaidi za kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.
Aidha, vijana hao wameomba kuandaliwa kwa semina na mafunzo mbalimbali yatakayowaongezea ujuzi na kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kushiriki katika ujenzi wa taifa.
Kwa upande mwingine, viongozi wamehimizwa kuchukua jukumu la kuibua na kukuza vipaji vya vijana, ili kuwasaidia kufikia ndoto zao na kuchangia maendeleo ya nchi kwa ufanisi zaidi.
Vijana hao pia wameeleza kutoridhishwa na tabia ya kutumika zaidi wakati wa dharura au misimu ya uchaguzi pekee, wakisisitiza umuhimu wa kushirikishwa kwao wakati wote katika michakato ya maendeleo.
Katika hatua nyingine, wametoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kutoa mkopo wa shilingi bilioni 200, ambao wanaamini utasaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi, hususan vijana.
Akizungumza katika kata za Idamba, Lupembe, Kidegembeye, Ikuna, Matembwe na Mtwango, Katibu wa UVCCM Wilaya ya Njombe, Ndugu Mengi Mwakisole,