
05/11/2022
Wafanyakazi wa Kampuni ya Twitter wameanza kupunguzwa kazi kutokana na mpango mpya wa kubana matumizi. Mpango huo umeanza baada ya kampuni hiyo kununuliwa na tajiri namba moja Duniani Elon Musk.
Baadhi ya wafanyakazi waliamka leo asubuhi na kukuta wamefungiwa kuingia kwenye komputa zao za kazi pamoja na kuona barua pepe za kazi, vilevile walijikuta wametolewa kwenye programu kadhaa za kazi.
Wafanyakazi hao walipewa taarifa za kupunguzwa kazi kupitia barua pepe.
Twitter imekuwa na wafanyakazi takribani 7500 ,taarifa zinadai kuwa kati ya hao asilimia 25 hadi 50 wanaweza wakapoteza kazi chini ya mpango huo.