Kata ya Utalingolo

Kata ya Utalingolo Ukurasa wa Matukio mbalimbali ya Maendeleo Kata ya Utalingolo Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoa wa N

TAREHE 04.07.2022
06/07/2022

TAREHE 04.07.2022

Kamati ya Ununuzi wa Gari Parokia Utalingolo (KUGPU)  yafanikisha ununuzi wa gari jipya LAND CRISER yenye thamani ya sh ...
08/05/2022

Kamati ya Ununuzi wa Gari Parokia Utalingolo (KUGPU) yafanikisha ununuzi wa gari jipya LAND CRISER yenye thamani ya sh 121,357,666.55 na kukabidhi Parokiani tr 08.05.2022. Tunawashukuru Wadau wote wa ndani na nje ya nchi waliochangia. Hakika ukimtanguliza Mungu hakuna linaloshindikana. Haikuwa rahisi, tulipijipa moyo na hamasa bila kukata tamaa MPAKA tunafanikisha. Tulianza Oct 2019 hadi leo 08.05.2022 tunapokabidhi gari rasmi. Mungu apewe sifa.

07/05/2022

*TANGAZO*
Parokia ya Utalingolo Jimbo Katoriki Njombe, inawakaribisha Wadau wote waliochangia Ununuzi wa gari, wananchi na waumini wote wa kanisa Katoliki katika hafla ya kukabidhi gari mpya kwa Parokia ya Utalingolo.
Hafla hiyo itakayofanyika baada ya Misa ya asubuhi hapo kesho 8/5/2022 kuanzia majira ya saa nne kamili Asubuhi katika kanisa la Roman Katoriki Parokia ya Utalingolo.

Hafla hiyo itahudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh Waziri Kindamba akiongozana na viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa, Mh Erasto Ngole katibu wa siasa na uenezi (CCM) Mkoa wa Njombe na Daktari Thobias Lingalangala ambaye ana mchango mkubwa ktk kufanikisha ununuzi wa hii gari, pia ni mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Njombe (NJOREFA) na ni mdau mkubwa wa maendeleo Njombe.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa ni Mhashamu Askofu John Chrisostom Ndimbo wa jimbo Katoliki la Mbinga na msimamizi wa kitume wa jimbo Katoliki Njombe.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MHESHIMIWA ERASTO MPETE MWENYEKITI KWA NIABA YA KAMATI YA UNUNUZI WA GARI LA PAROKIA YA UTALINGOLO (KUGPU)

*Misa na hafla hiyo itakuwa Mbashara (live) kupitia FACEBOOK kwa jina: Kata ya UTALINGOLO.*

*DC NJOMBE APONGEZA KUKAMILIKA KWA KASI UJENZI DARASA LA UVIKO 19 SHULE YA SEKONDARI UTALINGOLO, ASEMA NI NAMBA MOJA WIL...
18/12/2021

*DC NJOMBE APONGEZA KUKAMILIKA KWA KASI UJENZI DARASA LA UVIKO 19 SHULE YA SEKONDARI UTALINGOLO,
ASEMA NI NAMBA MOJA WILAYA YA NJOMBE.*

*Na Maiko Luoga Njombe*
TR 15.12.2021

Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe, Kissa Gwakisa amepongeza kasi ya ujenzi na ukamilishaji wa chumba cha darasa kilichojengwa kwa fedha za mapambano dhidi ya UVIKO 19 lililopo katika shule ya Sekondari Utalingolo mjini Njombe, akisema darasa hilo ni namba moja wilayani humo.

Mhe, Gwakisa amesema hayo Disemba 15/2021 alipofanya ziara ya kutembelea shule ya sekondari kata ya Utalingolo, kisha kufanya mkutano na wananchi wa kata hiyo akisikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.

“Leo ni Tarehe ya mwisho kukamilisha ujenzi wa madarasa haya ya fedha za UVIKO 19, nawapongeza Viongozi na wananchi wa kata ya Utalingolo mkiongozwa na diwani wenu Mhe, Erasto Mpete kwa kufanikisha ukamilishaji wa darasa hili kwa wakati, ninyi mmekuwa namba moja katika wilaya ya Njombe” Mhe, Kissa Gwakisa.

Diwani wa Kata ya Utalingolo na makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe, Erasto Mpete amesema, darasa hilo limetumia fedha ya UVIKO 19 kiasi cha shilingi milioni ishirini iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan.

“Tunamshukuru Mhe, Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha hii ambayo imefanikisha kukamilisha jengo hili, pia tunaendelea na ujenzi wa majengo mengine hapa shuleni ikiwemo maabara kwa kutumia fedha za serikali na nguvu za wananchi” Mhe, Erasto Mpete.

Mkuu wa wilaya ya Njombe aliahidi kutoa Kompyuta moja na Printa katika shule ya Sekondari Utalingolo ili kurahisisha utendaji kazi kwa walimu na wanafunzi, huku akipongeza juhudi za Mbunge wa Njombe Mjini Mhe, Deo Mwanyika na Diwani wa Kata ya Utalingolo Mhe, Erasto Mpete za kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo kutoa fedha zao kufanikisha kazi hizo.

“Nimeambiwa hapa kuwa Mhe, Deo Mwanyika Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini pamoja na kuchangia kazi za maendeleo, ametoa saruji mifuko 50 kwa kila kijiji cha Kata hii ya Utalingolo, licha ya kwamba hayupo hapa leo naomba nimpongeze sana yeye pamoja na diwani wenu hawa ni viongozi wa kuigwa” alieleza Mhe, Kissa Gwakisa.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Utalingolo walioshiriki mkutano huo walimweleza mkuu wa wilaya ya Njombe changamoto ya mlipuko wa bei ya mbolea wakisema, watashindwa kuzalisha mazao katika msimu huu wa kilimo, jambo ambalo Mkuu huyo wa wilaya ya Njombe amesema, Serikali inaendelea kutafuta namna ya kuimaliza kero hiyo.

*UVIKO 19 CHANJO ZAENDELEA KUTOLEWA NJOMBE*   *Na Maiko Luoga Njombe.* TR 15.12.21Wito umetolewa kwa wananchi na viongoz...
18/12/2021

*UVIKO 19 CHANJO ZAENDELEA KUTOLEWA NJOMBE*

*Na Maiko Luoga Njombe.*
TR 15.12.21

Wito umetolewa kwa wananchi na viongozi Mjini Njombe kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO 19 ili kujihakikishia usalama wa Afya zao kwakuwa homa hiyo bado ipo na inahatarisha nguvu kazi nchini.

Wito huo umetolewa na Mhe, Erasto Mpete Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe na Diwani wa kata ya Utalingolo, wakati akipatiwa chanjo ya pili ili kujikinga na UVIKO 19, zoezi lililofanyika mbele ya umati wa wananchi wa Kata hiyo waliojitokeza kwenye mkutano wa Mkuu wa wilaya ya Njombe uliofanyika Disemba 15 mwaka huu.

"Kwa muda mrefu nilitulia nikiendelea kutafakari na kuona k**a jambo hili ni jema, sasa nimepata majibu na kuamini kuwa Chanjo hii ni salama ndio maana nimeamua kuchanja kwa usalama wa afya yangu, natoa wito kwa jamii kutumia chanjo hii" alisema Erasto Mpete Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe.

Aidha Mpete alipongeza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suluhu Hassan za kuhakikisha anapigania Afya za Watanzania kwa kuhakikisha chanjo zinaendelea kutolewa nchini bila kujali wananchi wa hali ya chini waliopo Vijijini.

"Tunajua kuchanja ni hiari ya mtu lakini naomba niwaeleze kuwa ukichanja unajihakikishia afya njema zaidi kuliko mtu ambae hajachanja pia chanjo hii ni salama haina shida ndio maana leo nimeamua kuchanja mbele yenu mnione nanyi mniunge mkono, Wananchi na viongozi wenzangu tutumie kinga hii" Mpete.

Akikabidhi hati ya chanjo hiyo kwa Mhe, Erasto Mpete, Mkuu wa wilaya ya Njombe Mhe, Kissa Gwakisa alipongeza ujasiri wa kiongozi huyo wa kuamua kuchanja mbele ya umati wa wananchi huku akitoa elimu kwa wananchi na watumishi wengine wa serikali kuamua kupata chanjo hiyo kwa usalama wa Afya zao.

"Nampongeza Mhe, Mpete kwa kupata chanjo hii ya UVIKO 19 naomba sasa wananchi tuungane kwa pamoja tuchanje kwa amani ili tuishi salama pia kwakuwa ni hiari yako basi hulazimishwi lakini ukichanja unakuwa huru na salama zaidi katika kukabiliana na homa hii" Kissa Gwakisa DC Njombe.

Hatahivyo Mkuu wa wilaya ya Njombe, aliwataka Viongozi wengine kuiga mfano huo kwani katika uchanjaji awamu ya kwanza Mhe, Mpete alifanya hivyo siku ya Tamasha la NJOMBE YA MAMA SAMIA lililofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani akisema, watu wengi walihamasika na kuiwezesha Halmashauri ya Mji wa Njombe kuwa kinara katika Wilaya ya Njombe kwa uchanjaji, hadi kufikisha jumla ya asilimia 123.

Kufuatia elimu na ufafanuzi wa chanjo hiyo uliotolewa na wataalamu wa Afya, wananchi wengi waliamua kutumia haki yao ya kupata chanjo huku wakisema hawajaona madhara yeyote mara baada ya kutumia chanjo hiyo.

UTOAJI DAMU, UWE ENDELEVU, UWE NI UTAMADUNI WETU,. TUSISUBIRI SIKU TU YA MATAMASHA, MAONESHO NK
17/11/2021

UTOAJI DAMU, UWE ENDELEVU, UWE NI UTAMADUNI WETU,. TUSISUBIRI SIKU TU YA MATAMASHA, MAONESHO NK

CHANJO YA CORONA/UVIKO 19 NI SALAMA. TR 15.11.2021
17/11/2021

CHANJO YA CORONA/UVIKO 19 NI SALAMA.
TR 15.11.2021

TAARIFA KWA WANANCHI WA JIMBO LA NJOMBE MJINIMheshimiwa mbunge wa Jimbo la njombe mjini Mhe DEO MWANYIKA katika kuunga m...
19/09/2021

TAARIFA KWA WANANCHI WA JIMBO LA NJOMBE MJINI

Mheshimiwa mbunge wa Jimbo la njombe mjini Mhe DEO MWANYIKA katika kuunga mkono juhudi za maendeleo ktk shughuli za ujenzi mbalimbali. Mheshimiwa amefanya yafuatayo
1. Amechangia saruji mifuko 50 kwa vijiji vyote vya Jimbo la njombe mjini
2. Amechangia saruji mifuko 150 kwa kila kata tarafa ya Njombe mjini
Dira mpya, Njombe mpya
Kazi iendelee

IMETOLEWA NA
KATIBU WA MBUNGE
ANDREAS MAHALI
0763874373

OFISI YA MBUNGE JIMBO LA NJOMBE MJINI
Kwa maoni, ushauri, mapendekezo piga namba zifuatazo saa 24

0763874373
0623910139
Katibu wa mbunge
Andreas MAHALI

*Kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Utalingolo, tunawatakia kila la heri watoto wetu wote -Tz waanzao mtihani wao wa Taifa...
08/09/2021

*Kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Utalingolo, tunawatakia kila la heri watoto wetu wote -Tz waanzao mtihani wao wa Taifa STD VII. Mungu awaongoze wafanye kwa utashi na bila woga kadri walivyofundishwa na walimu wao*
*Mungu awabariki.*
*Erasto Mpete*
*DIWANI*

TAREHE 10.8.2021WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAMISEMI, MH UMMY MWALIMU ALITEMBELEA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE KTK KATA YA...
08/09/2021

TAREHE 10.8.2021
WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS TAMISEMI, MH UMMY MWALIMU ALITEMBELEA HALMASHAURI YA MJI NJOMBE KTK KATA YA UTALINGOLO, MATOLA NA MAKOWO.

Kata ya Utalingolo alikagua mradi wa barabara ya Utalingolo to Njengerendeti. Alisomewa taarifa ya mradi na kuongea na wananchi ktk kijiji cha MFEREKE

16/07/2021

⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

*MPETE DIWANI CUP 2021*

Karibuni nyote ktk uzinduzi huu tr 18.7.21. Vijana Ni nguvu kazi ya Sasa.
Haya pia ni Maandalizi ya ligi kubwa ya Mh Deo Mwanyika Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini

JENGO LA MIONZI KATA YA UTALINGOLO KITUO CHA AFYA IHALULA
04/07/2021

JENGO LA MIONZI KATA YA UTALINGOLO KITUO CHA AFYA IHALULA

Address

Njombe Mjini
Njombe

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kata ya Utalingolo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share