24/08/2025
*NENO LA SHUKRANI*
Ninaandika Ujumbe huu kwa moyo wa shukrani na unyenyekevu mkubwa kwenu nyote ndugu na Wananchi wenzangu wa Jimbo la Lupembe.
Mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM umefika tamati tar 23/08/2025. Sasa tunayo kazi moja ya Uchaguzi Mkuu wa mwezi Octoba, 29.
Natoa shukrani kwa chama changu Chama Cha Mapinduzi na Kamati Kuu ya CCM Taifa kwa imani yao kwangu. Nawashukuru pia wajumbe wa CCM kwa kuonesha imani yao kwangu katika kura za maoni. Wagombea wote 6 tulikuwa na sifa za kutosha za uongozi lakini Hekima yao iliona mimi nipewe nafasi tena ili kuwaongoza wenzangu. Ahsanteni sana WAJUMBE.
Aidha kwa dhati ya moyo wangu nawashukuru wale wote ambao wameendelea kutoa muda wao kuniombea na kunitakia kila la heri katika uongozi wa Jimbo letu. Kazi hii ni ngumu, yenye lawama nyingi, na wakati fulani kukatishwa tama. Yote hayo ni sehemu ya uongozi. Ashukuliwe Mungu anayetupa Nguvu kila iitwapo leo katika kuifanya kazi hii kwa bidii na haki kwa watu wote.
Kwa uzito wa pekee nawashukuru sana wale wote waliotoa muda wao, mali na nguvu kwaajili ya kuniunga mkono mimi, kunitia moyo na kunipigania kuhakikisha ninashinda kura ya maoni. Hakika haikuwa rahisi. Demokrasia ilichukua nafasi yake kisawasawa.
Nawapongeza sana washindani wenzengu. Walishindana na mimi kwa Bidii, maarifa mengi, ufundi na weledi wa Kampeni.Walishindana nami kwa staha, na mbinu zote za siasa. Ninaamini walishiriki mchakato wa uchaguzi siyo kwasababu hawanipendi au wanadhani sina uwezo, la hasha bali waligombea ili kutumia haki yao kikatiba. Haki ya kuchaguliwa. Nawapongezeni sana nyote mlioshiriki katika mchakato huu wa Demokrasia ndani ya chama kwa moyo wa uzalendo, uvumilivu na staha kubwa!
Wale walioniunga mkono mimi walitumia haki yao pia kuniunga mkono. Na Ninajua walifanya hivyo siyo kwasababu wale washidani wangu wengine hawakuwa na sifa, la hasha bali waliamini kwamba kwa sasa mimi bado ninao wajibu wa kuongoza wenzangu. Hivyo leo Wakifurahi ni haki yao. Wakicheka ni haki yao pia. Tuvumiliane. Asanteni sana wapiganaji woote kwa imani yenu kwangu! Tuhongidze hilo!
*Mwisho,* Kura hukomesha mashindano (Mith 18:18). Mashindano ya kura za maoni yamekwisha. Sasa twendeni pamoja kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Octoba,29. Jimbo letu la Lupembe linahitaji Umoja wetu zaidi kuliko tofauti zetu. Mmoja wetu akishinda Jimbo zima litakuwa limeshinda. Umoja wetu ndiyo nguvu yetu!!.
Asanteni sana.
*Swalle, E. E*