Rasilimali Zetu Plus Tv

Rasilimali Zetu Plus Tv Tunatoa maarifa yanayosaidia jamii wa utunzaji wa rasilimali na kutafuta suluhisho zinazohusiana na mazingira. Kauli Mbiu: "Elimu kwa Maendeleo Endelevu"

Lengo letu ni kukuza uelewa wa umma kuhusu matumizi endelevu ya rasilimali na athari za mazingira.

TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO 🔴Tunatoa taarifa kwa umma kuhusu kupotea kwa mtoto wetu mpendwa:👦 Jina: Andrew Christopher ...
15/09/2025

TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO 🔴

Tunatoa taarifa kwa umma kuhusu kupotea kwa mtoto wetu mpendwa:

👦 Jina: Andrew Christopher Kamonga
📍 Alipotelea: Kata ya Lugarawa, Wilaya ya Ludewa
📅 Tarehe: 03.09.2025

Licha ya jitihada mbalimbali za kumtafuta, bado hajapatikana. Tunaomba ushirikiano wa wananchi wote kumsaidia kurejea nyumbani salama.

👉 Iwapo utamuona au kuwa na taarifa zozote, tafadhali wasiliana nasi kupitia:
📞 0625 838 000 – Christopher Kamonga (Charles)
📞 0769 392 240 – Fransisco
📞 0693 716 220 – Mtendaji Kata Lugarawa

Au toa taarifa kwenye kituo chochote cha polisi kilicho karibu nawe.

🙏 Tunawaomba msaada wenu na dua zenu ili Andrew apatikane salama.

Taarifa imetolewa na
Ndugu Christopher Charse Kamonga
Wa Ludewa Mjini

Gari Triple star Aina ya Rosa, iliyo kuwa ikifanya safari za Makambako Mlangali Lusala, Imegongana na Gari nyingine Aina...
31/08/2025

Gari Triple star Aina ya Rosa, iliyo kuwa ikifanya safari za Makambako Mlangali Lusala, Imegongana na Gari nyingine Aina ya Rosa iliyo kuwa ikielekea Mlangali. Na kupoteza mwelekeo na kugonga Nyumba Lusitu wilaya ya Ludewa .
Endelea kubak Nas Kwa taarifa zaidi

RIPOTI YA MASHINDANO NA TUZO ZA MSIMU WA 2025Tarehe: Jumamosi, 23 Agosti 2025Mahali: Ludewa---MATOKEO YA TIMU BINGWA1. B...
26/08/2025

RIPOTI YA MASHINDANO NA TUZO ZA MSIMU WA 2025

Tarehe: Jumamosi, 23 Agosti 2025
Mahali: Ludewa

---

MATOKEO YA TIMU BINGWA

1. Bingwa wa Mashindano

Timu: SHUMA FC (Ngelenge)

Zawadi: Shilingi 1,000,000/=, Kikombe na Medali za Dhahabu

2. Mshindi wa Pili

Timu: MASASI FC (Kingole)

Zawadi: Shilingi 500,000/= na Medali za Shaba

3. Mshindi wa Tatu

Timu: LUILO FC (Luilo)

Zawadi: Shilingi 300,000/= na Medali za Fedha

---

TUZO NA ZAWADI BINAFSI NA KIKUNDI

1. Timu yenye Nidhamu: IDUSI FC (Nkomang’ombe) – Tsh. 100,000/=

2. Kikundi Bora cha Ushangiliaji: Mashabiki wa MAKALI FC (Kingole) – Tsh. 100,000/=

3. Mwamuzi Bora: Ndugu John Janken Haule – Tsh. 50,000/=

4. Golikipa Bora: Erick B. Haule (LUILO FC) – Tsh. 100,000/=

5. Kocha Bora: Ndugu Thadei Macheso Mwela (SHUMA FC) – Tsh. 100,000/=

(Ameshinda tuzo hii kwa misimu mitatu mfululizo)

6. Mtoa Taarifa Bora (Best Reporter): Ndugu Njenje Ze Lopo (Rafiki FM, Ludewa)

---

HAT-TRICKS ZILIZOPIGWA

Hassan Mbeya (SAGALU FC) – 1 Hat-trick – Tsh. 20,000/=

Jacob Mapunda (MASASI FC) – 1 Hat-trick – Tsh. 20,000/=

Emilias Gowe (NYASA VETERANI FC) – 1 Hat-trick – Tsh. 20,000/=

Efraim Ngatunga (ILELA FC) – 2 Hat-tricks – Tsh. 40,000/=

Ched Mapunda (SHUMA FC) – 1 Hat-trick – Tsh. 20,000/=

Emanuel Mwinuka (LAKE STARS) – 1 Hat-trick – Tsh. 20,000/=

---

MCHEZAJI BINAFSI WALIOSHINDA TUZO KUBWA

Mfungaji Bora (Top Scorer):

Jacob Mapunda (MASASI FC) – Magoli 11

Waliomfuatia: Emanuel Mwinuka (Lake Stars) na Efraim Ngatunga (ILELA FC) – Magoli 9 kila mmoja

Mchezaji Bora (MVP):

Jacob Mapunda (MASASI FC)

---

SHUKRANI MAALUM

Kwa niaba ya Kamati ya Mashindano, tunapenda kutoa shukrani zetu kwa:

Mdhamini Mkuu wa Mashindano na familia yake

Wadhamini wenza wote

Mratibu Mkuu wa Mashindano kwa ushauri na mwongozo

Afisa Habari wa Mashindano kwa maelekezo na mchango wake

Waandishi wa Habari wakiongozwa na Ndugu Njenje Ze Ropo

Kamati za Ulinzi na Usalama

Waamuzi, Watoa huduma ya kwanza na Wahudumu wa uwanja

Viongozi wa Timu shiriki, Wachezaji na Mashabiki

Tunatambua mchango wa kila mmoja wenu katika kufanikisha msimu huu wa mashindano. Endapo kwa namna yoyote k**ati au mimi binafsi k**a Mtendaji Mkuu tulimkosea mtu au t

KUAMBIANA AJITOLEA KUJENGA ZAHANATI YA KINGOLE . DC LUDEWA ATOA WITO WA USHIRIKIANO AWEKA JIWE LA MSINGILudewa – MasasiZ...
25/08/2025

KUAMBIANA AJITOLEA KUJENGA ZAHANATI YA KINGOLE . DC LUDEWA ATOA WITO WA USHIRIKIANO AWEKA JIWE LA MSINGI

Ludewa – Masasi
Ze ropo

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olivanus Paul Thomas, ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati ya Kingole, iliyopo Kata ya Masasi, Wilaya ya Ludewa. Zahanati hiyo inajengwa kwa ufadhili wa mdau wa maendeleo wa wilaya hiyo, Ndugu Iman Haule Kuambiana.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, DC Thomas aliwaasa wakazi wa Ludewa na Masasi kurudi makwao kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo, ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa na kuendeleza miradi ya kijamii. Aidha, aliwahimiza wananchi kujitolea nguvu kazi ili kurahisisha ujenzi wa zahanati hiyo.

> “Tunapaswa kushirikiana na kushik**ana k**a jamii moja. Kila mmoja awe tayari kutoa mchango wake, iwe kwa nguvu kazi au kwa njia nyingine, ili mradi huu mkubwa ukamilike kwa wakati,” alisema DC Thomas.

Mradi huo unakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi milioni 150 hadi kukamilika kwake.

Kwa upande wake, mdau wa maendeleo, Ndugu Iman Haule Kuambiana, alisema aliguswa kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo baada ya kushuhudia changamoto kubwa wanazokabiliana nazo akinamama wajawazito katika kata hiyo.

> “Sina fedha nyingi k**a watu wanavyodhani. Nilichonacho ni moyo wa kujitolea na kupenda kusaidia jamii yangu,” alisema Haule.

Katika hafla hiyo, DC Thomas aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Bw. Sunday Deogratious, ambaye aliahidi ushirikiano wa karibu kwa kuhakikisha vifaa tiba na wataalamu wa afya vinapatikana mara tu ujenzi wa zahanati hiyo utakapokamilika.














TEACHER'S DAY OUT KWA MARA YA KWANZA TANZANIA YAFANYIKA LUDEWA KWA KISHINDO.Ludewa, Agosti 22, 2025Kwa mara ya kwanza ka...
25/08/2025

TEACHER'S DAY OUT KWA MARA YA KWANZA TANZANIA YAFANYIKA LUDEWA KWA KISHINDO.

Ludewa, Agosti 22, 2025

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Wilaya ya Ludewa imeandika ukurasa mpya kwa kuandaa Teacher's Day Out, sherehe maalum ya kuwatambua na kuwapongeza walimu kwa mchango wao mkubwa katika sekta ya elimu.

Sherehe hiyo imefanyika kwa ushirikiano kati ya Uongozi wa Wilaya ya Ludewa na wadau mbalimbali wa maendeleo, ikiwa na lengo la kuonyesha kutambua jitihada za walimu zilizosaidia kupandisha ufaulu wa wanafunzi mwaka hadi mwaka.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mheshimiwa Olivanus Thomas, aliyeambatana na watumishi mbalimbali wa halmashauri akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Ndugu Sunday Deogratias.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na walimu kutoka shule zote za msingi na sekondari ndani ya wilaya, wananchi, pamoja na wadau wa elimu na maendeleo, na ilipambwa na michezo mbalimbali k**a vile kuvuta kamba, kukimbia na yai, mpira wa miguu, kukimbiza kuku, na kukaa kwenye viti yote ikiwa ni sehemu ya burudani na motisha kwa walimu.

Akizungumza kwenye tukio hilo, Mhe. Olivanus alisema sherehe hii ni njia ya kuthamini na kuwapa hamasa walimu kutokana na mchango wao wa pekee unaochochea maendeleo ya elimu. Alieleza kuwa Ludewa imeonyesha maendeleo makubwa katika ufaulu kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, hivyo ni haki kuwatambua walimu k**a nguzo kuu ya mafanikio hayo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Sunday Deogratias aliipongeza sherehe hiyo kwa ubunifu wake na akalibariki rasmi tukio hilo, akieleza kuwa litakuwa tukio endelevu ili kuendelea kuwahamasisha walimu kuleta matokeo chanya katika elimu. Alisisitiza kuwa walimu ni moyo wa maendeleo ya wilaya na Taifa kwa ujumla.
-gwakisa

Hii ni safi sana! Mashabiki wa Kuambiana Cup Ludewa 2025 wameonesha kitu cha kipekee kabisa – upendo, mshik**ano na msha...
24/08/2025

Hii ni safi sana! Mashabiki wa Kuambiana Cup Ludewa 2025 wameonesha kitu cha kipekee kabisa – upendo, mshik**ano na mshangilio wa hali ya juu. Hizi picha za juu kwa drone zinaonyesha wazi kwamba hii ligi sio tu mpira wa miguu, bali ni tamasha la kijamii linalowaunganisha watu wa Ludewa k**a familia moja.

🌟 Maneno ya Kuwasifu Mashabiki:
"Shukrani kubwa kwa mashabiki wote wa Ludewa mliojitoa kwa moyo wote kushiriki na kushangilia ligi ya Kuambiana Cup 2025. Uwepo wenu uwanjani na nguvu zenu za kutia moyo wachezaji ni ushindi mkubwa kuliko kombe lenyewe. Nyinyi ndio mnaofanya mchezo huu kuwa na ladha, mnaweka heshima na thamani ya kweli kwa michezo ya kijamii. Hata jua kali na vumbi havikuwazuia – mmeonesha kwamba mpira ni zaidi ya mchezo, ni urithi wa mshik**ano wa Ludewa. Hakika nyinyi ni mabingwa wa kweli wa uwanjani na nje ya uwanja!"

📸 Maelezo ya Picha za Drone:

1. Picha ya Kwanza – Jukwaa la wageni rasmi na viongozi wa wilaya, likiwa limepambwa vizuri chini ya kivuli cha mti mkubwa. Hapa ndipo historia ya Kuambiana Cup 2025 inapoandikwa kwa heshima kubwa.

2. Picha ya Pili – Uwanja ukiwa na wachezaji katikati ya pambano kali huku mashabiki wakipanga mstari mrefu pembezoni mwa uwanja, wakifurahia kila dakika ya mchezo.

3. Picha ya Tatu – Mtazamo wa juu zaidi ukionesha uwanja mzima uliojaa mashabiki, nyumba za jirani na mazingira ya Ludewa yakitoa taswira ya kipekee ya mashindano haya.

⚽🔥 Kuambiana Cup sio tu michuano ya soka, ni sehemu ya historia ya Ludewa na urithi wa mshik**ano wa jamii.

⚽🔥 *SHUMA FC YAENDELEA KUTISHA – YATWAA KOMBE LA KUAMBIANA CUP LUNDEWA MARA TATU MFULULIZO!* 🔥⚽Na Njenje ze ropoLudewa ....
24/08/2025

⚽🔥 *SHUMA FC YAENDELEA KUTISHA – YATWAA KOMBE LA KUAMBIANA CUP LUNDEWA MARA TATU MFULULIZO!* 🔥⚽

Na Njenje ze ropo
Ludewa .

Mashindano ya Kuambiana Cup Ludewa (Tarafa ya Masasi) yamehitimishwa kwa kishindo baada ya fainali kali iliyowakutanisha Masasi FC na wababe kutoka Ngelenge, SHUMA FC.

Dakika zote 90 zilikuwa na msisimko mkubwa, mashabiki wakipiga kelele, vuvuzela na nyimbo za kishujaa zikisikika kila kona ya uwanja. Masasi FC walijitahidi kupambana, lakini ukuta na mashambulizi ya SHUMA FC yalikuwa moto usioweza kuzimika. 💥

Mwisho wa mchezo, SHUMA FC waliibuka na ushindi wa mabao 3–1, na kwa mara nyingine tena kuonyesha hawana mpinzani. Huu ni ubabe wa historia – kutwaa kombe hilo mara tatu mfululizo 🏆🏆🏆.

Mgeni rasmi wa fainali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mh. Olvanus Paul Thomas, aliwapongeza wachezaji na viongozi wote wa timu, huku akiwataka vijana wa Ludewa waige mfano wa SHUMA FC kwa kujituma, kushirikiana na kuwekeza katika michezo na maendeleo ya jamii.

Kwa ushindi huu, SHUMA FC wameweka alama ya dhahabu katika ramani ya michezo Ludewa. Ngelenge imewaka moto 🔥 – mashabiki wakicheza, wakipiga ngoma na kushangilia hadi usiku, wakitangaza kwa sauti moja:
👉 “Mabingwa hawabahatishi, SHUMA FC ni zaidi ya timu – ni historia, ni familia, ni nguvu ya Ludewa!” 💚⚽

HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA YANG’ARA, YASHINDA TUZO YA HALMASHAURI BORA KATI YA HALMASHAURI 40 ZA NYANDA ZA JUU KUSI...
08/08/2025

HALMASHAURI YA WILAYA YA LUDEWA YANG’ARA, YASHINDA TUZO YA HALMASHAURI BORA KATI YA HALMASHAURI 40 ZA NYANDA ZA JUU KUSINI

Mbeya, Agosti 8, 2025 – Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imeibuka kinara na kutunukiwa cheti pamoja na tuzo ya “Halmashauri Bora” katika kundi la halmashauri 40 kutoka mikoa saba ya Nyanda za Juu Kusini, ikiwemo Iringa, Njombe, Ruvuma, Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi.

Tuzo hiyo imetolewa leo katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, yaliyofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhe. Makongoro Nyerere, akimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Ndugu Sunday Deogratias, pamoja na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, walisema ushindi huo ni matokeo ya mshik**ano na mshirikiano mkubwa uliopo kati ya viongozi wa ngazi zote, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Mhe. Olivanus Thomas, sambamba na viongozi wa vijiji na kata.

“Hii ni heshima kwa wananchi wote wa Ludewa. Ushirikiano wa viongozi na wananchi ndio umetufikisha hapa,” alisema Deogratias.

Ushindi huu umeonesha dhamira ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa kuendelea kuboresha sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, na kutoa mchango chanya kwa maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ujumla.

"MASASI WAWATIMUA NKOMANG’OMBE KWA MATUTA! MAPUNDA NA MHAGAMA WATESA, PENALTI ZAWALIZA WAPINZANI!"Katika mchezo wa kusis...
08/08/2025

"MASASI WAWATIMUA NKOMANG’OMBE KWA MATUTA! MAPUNDA NA MHAGAMA WATESA, PENALTI ZAWALIZA WAPINZANI!"

Katika mchezo wa kusisimua wa robo fainali ya Kuambiana Cup 2025, timu ya MASASI imefanikiwa kuibuka kidedea dhidi ya wapinzani wao wakali NKOMANG’OMBE fc almaarufu k**a matajir wa MAKAA ya mawe kwa ushindi wa penalti 4-3 baada ya sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 90.

Mchezo huo uliopigwa kwa kiwango cha juu, ulianza kwa kasi na ushindani mkubwa kutoka pande zote mbili. Steve Mhagama aliweka MASASI kifua mbele kwa bao safi lililowachanganya walinzi wa NKOMANG’OMBE, Jacob Mapunda wa MASASI aliwatikisa tena mashabiki kwa bao la pili, kabla ya Frances Haule kuwasawazishia wapinzani hao kwa kombora kali lililompita kipa bila jibu.

lakini furaha yao haikudumu kwani Yohana Kilumbo wa NKOMANG’OMBE alifunga bao la kusawazisha, na kufanya mchezo kuwa wa mabao 2-2 hadi dakika ya mwisho.

Kwa kuwa hakuna mshindi aliyetokea ndani ya muda wa kawaida, mchezo ulielekea kwenye mikwaju ya penalti — na hapo ndipo moyo wa chuma wa MASASI ulipojitokeza.

Kwa penalti:

MASASI walifunga 4,

NKOMANG’OMBE walifunga 3,
huku penalti moja ikipanguliwa na kipa wa MASASI kwa ujasiri wa ajabu.

🔥 Mashabiki wa MASASI waliripuka kwa shangwe, huku nyimbo na vuvuzela vikichangamka kuashiria ushindi mkubwa uliowapeleka kwenye hatua ya nusu fainali!

🚀 Je, kombe litabaki kwao? Muda ndio utaamua!

KUAMBIANA CUP 2025: ILELA FC YATUPWA NJE YA MASHINDANOKatika mchezo wa kusisimua wa Kombe la Kuambiana 2025, Ilela FC im...
06/08/2025

KUAMBIANA CUP 2025: ILELA FC YATUPWA NJE YA MASHINDANO

Katika mchezo wa kusisimua wa Kombe la Kuambiana 2025, Ilela FC imetupwa nje ya mashindano baada ya kuchapwa bao 1-0 na Luilo FC.

Mchezo huo uliochezwa kwa ushindani mkubwa ulimalizika kwa ushindi wa Luilo FC, bao pekee likifungwa na Calvin Mpume, ambaye aliibuka shujaa wa mchezo kwa timu yake.

Licha ya juhudi za Ilela FC, walishindwa kupata bao la kusawazisha, na hivyo ndoto zao za kuendelea kwenye mashindano zikafikia kikomo.

Matokeo ya mwisho:
Luilo FC 1 - 0 Ilela FC
Mfungaji: Calvin Mpume ⚽
Game Over ✅

Mashabiki wa Luilo FC walifurahia ushindi huo, huku timu yao ikisonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano.

06/08/2025
🕊️ Taarifa ya Msiba – Ndg. Nestory Kayombo (Mtaalamu)Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Ndugu yetu mpendwa Nest...
05/08/2025

🕊️ Taarifa ya Msiba – Ndg. Nestory Kayombo (Mtaalamu)

Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Ndugu yetu mpendwa Nestory Kayombo, maarufu kwa jina la Mtaalamu, ambaye pia alikuwa Diwani mstaafu wa Kata ya Mkongongobaki.

Taarifa zinasema kuwa baada ya kushiriki katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupoteza nafasi hiyo, hali yake kiafya ilibadilika ghafla. Inadaiwa kuwa alikumbwa na shinikizo la damu (BP), hali iliyosababisha kufariki dunia. 😭😭

Tunatoa pole za dhati kwa familia yake, ndugu, jamaa na wakazi wote wa Kata ya Mkongongobaki kwa msiba huu mzito wa kumpoteza kiongozi, rafiki na mzalendo wa kweli.

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe.

🕯️ Pumzika kwa amani Mtaalamu.

Address

Ludewa
Njombe

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Telephone

+255755666795

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Rasilimali Zetu Plus Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Rasilimali Zetu Plus Tv:

Share