HabariHub

HabariHub HABARI | BURUDANI | FILAMU MPYA | MICHEZO | MAKALA| Karibu kwenye Habari Hub. Tunathamini maoni na mawazo yako. Asante kwa kujiunga na Habari Hub!

Ukurasa huu ni maalumu kwa ajili ya kutoa habari za hivi karibuni katika uwanja wa burudani, michezo, siasa, na makala mbalimbali. Tunapenda kuwapa wafuasi wetu taarifa za kuvutia, za kuaminika, na za kuelimisha, zinazowapa ujuzi na kuburudisha kwa wakati mmoja. Tunajivunia kuwa chanzo chako cha kuaminika cha habari, tukijitahidi kuleta upeo mpana wa mada kufuatana na maslahi ya wasomaji wetu. Tun

a timu ya waandishi waliobobea ambao wanashughulikia habari zote muhimu na za kusisimua zinazohusiana na burudani, michezo, siasa, na zaidi. Kupitia ukurasa wetu, utapata makala za kina zinazoshughulikia mada mbalimbali, mahojiano na watu maarufu, taarifa za matukio ya kusisimua, na mapitio ya burudani na michezo. Tunajitahidi kuleta habari zinazoburudisha na kuelimisha ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu wenye ladha tofauti. Tafadhali jiunge nasi katika mazungumzo kupitia sehemu ya maoni na ushiriki kwa kushirikiana habari zetu na yaliyomo na marafiki zako. Tuko hapa kukuletea habari sahihi na kuwaunganisha watu pamoja kupitia mawazo na maoni. Tuko hapa kukuletea habari za kuvutia na burudani kwa kila siku yako. Jiunge nasi na uwe sehemu ya safari yetu ya kusisimua na kuelimisha katika ulimwengu wa habari na burudani.

๐Ÿ“ŒPicha hizi zinatoka pale kaunti ya Antu, kaskazini mwa China katika jimbo la Jilin, Xueshanfeihs ni eneo la kitalii kut...
08/10/2024

๐Ÿ“ŒPicha hizi zinatoka pale kaunti ya Antu, kaskazini mwa China katika jimbo la Jilin, Xueshanfeihs ni eneo la kitalii kutokana na mazingira yake hewa nzuri inayopatikana katika eneo hilo.
โฌ‡
Sisi huku Tanzania tunakata miti hadi iitike "Rabeca" tukiambiwa ukikata mti panda mti, masikio hayasikii hata kidogo.
โฌ‡
Wasimamizi wa hifadhi nao baadhi yao hawana uadilifu, wanakula rushwa na kuwarudisha nyuma wenzao wanaosimamia sheria kuonekana ni wanoko sana.
โฌ‡
Tunajitetea kuwa "tukale wapi?" "Tusipochoma mkaa tutapata wapi pesa ya kuendesha familu?" Jiulize, hiyo familia (Watoto) wakikua wao watafaidika na nini k**a unakata na kumaliza miti yote kwa kuchoma mkaa?
โฌ‡
Serikali mnapowak**ata hawa wachoma mkaa na wauza mkaa, mnawapeleka mahak**ani wanahukumiwa au mnawapiga faini mnawaacha waende mkaa mnautaifisha, mnadhani hawa wataenda wapi?
โฌ‡
Kwanini serikali msiweke mpango nzuri kila Halmashauri, kuwakusanya hawa wakata miti, wachoma mikaa na wauza mikaa mkawapa project nyingine ya kuwaingizia kipato kupitia misitu hiyo hiyo na project zingine?
Mfano: Unawaweka kwenye vikundi mnawaanzishia mradi wa kufuga nyuki, wakilinda asali wanawauzia kikundi kingine wanaiongezea thamani asali ile hapo mnakuwa mmewaunganisha na SIDO.
Wengine wanashughulika na mazao mengine yanayozalishwa na nyuki kutengeneza nta nk.
โฌ‡
Ifike wakati tufikirie tofauti, tusione ni fahari kujaza magereza tu, matatizo/changamoto na tabia za watu zibadilishwe na kutengenezwa fursa. Fursa hizo ziwasaidie kujiingizia kipato na kutunza mazingira yetu kwa vizazi vya sasa na vya baadae.
โฌ†
๐Ÿ–ŠGeofrey D.

๐Ÿ”ดUSAHIHI WA TAARIFAUkipewa kichwa cha huyu jamaa unaweza usiamke kesho. Anaitwa Tyrese Gibson miaka 45, ni mwanamuziki w...
03/10/2024

๐Ÿ”ดUSAHIHI WA TAARIFA

Ukipewa kichwa cha huyu jamaa unaweza usiamke kesho. Anaitwa Tyrese Gibson miaka 45, ni mwanamuziki wa R&B na Muigizaji kutokea pale nchini Marekani. Ameigiza filamu nyingi moja wapo ni muendelezo wa filamu za Fast and Furious imezidi kumuweka kwenye vichwa vya habari katika media mbalimbali na kujizolea mkwanza.

Leo nimeona kwenye page za watu kadha wa kadha hapa Bongo zikidai kuwa jamaa amepokonywa mali zake zote na jumba lake na kwamba hatakiwi kufika katika jumba hilo isipokuwa kwa mwaliko tu na pia amepewa ruhusa ya kumuona binti yake wa miaka mitano (5) aitwaye Soraya.

Nimepita katika vyanzo vya habari vinavyoaminika ikiwemo na kote huko hakuna taarifa hiyo ambayo baadhi ya watanzania wenzangu wameichapisha pasipo na kuweka vyanzo vya habari.

Taarifa iliyopo hadi sasa kuhusu Gibson ni ya wiki mbili zilizopita yaani wiki ya tarehe 11 mwezi wa 9 mwaka 2024 ambayo nayo ilipotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amek**atwa alipokuwa amehudhulia kesi inayomkabili ya kutokutoa matunzo k**a alivyoamriwa na mahak**a mwaka 2022. Usahihi wa taarifa hiyo ni kuwa alizuiliwa kwa saa 2 pekee kisha aliachiwa kuendelea na shughuli zake. Kuzuiliwa kwake kunatokana na kutolipa child support ya kiasi cha dola za marekani 75,000 kulingana na nakala za mahak**a ambazo walizipata.

Kushikiliwa kwake kunaanzia mwaka 2022 ambapo aliamriwa na mahak**a kutoa kiasi cha $10,690 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto (child support). Awali mzazi mwenzake, Samantha Lee aliomba kulipwa $20,000 kila mwezi lakini Gibson aliomba apunguziwe na kufikia kiasi hicho cha $ 10,690.

Gibson, na Lee waliachana mwaka 2020 na amekuwa akipuuza kutoa kiasi alichoamriwa na mahak**a na badala yake amekuwa akitoa $2,200 wa ajili ya matunzo ya mtoto, kwa mujibu wa , ambao ndiyo walikuwa wakwanza kuripoti taarifa hiyo. Gibson amekuwa akilipa chini ya asilimia 25 ya kile alicho amriwa mwaka 2022.

Hivyo ifahamike kuwa, taarifa zinazo sema, "Mmesikia alichofanyiwa mwenzenu huko" ikiambatanishwa na picha ya Tyrese Gibson na taarifa inayodai, "...amenyang'wa nyumba, na kila kitu na kupewa masharti makali ili kumuona mwanaye..." SIYO ZA KWELI!

๐Ÿ–ŠGeofrey D.

๐ŸŒน๐‡๐š๐ฉ๐ฉ๐ฒ ๐๐ข๐ซ๐ญ๐ก๐๐š๐ฒ ๐€๐ฎ๐ง๐ญ Tedy Mgaya๐ŸŒนIshi sana Aunt angu๐ŸŽ‚๐Ÿพ๐Ÿฅ‚
25/08/2024

๐ŸŒน๐‡๐š๐ฉ๐ฉ๐ฒ ๐๐ข๐ซ๐ญ๐ก๐๐š๐ฒ ๐€๐ฎ๐ง๐ญ Tedy Mgaya๐ŸŒน

Ishi sana Aunt angu๐ŸŽ‚๐Ÿพ๐Ÿฅ‚

๐Ÿ“ŒNiliamua kupita kwenye page kadhaa ikiwemo Samson Charles , Malisa GJ, East Africa TV, millard ayo ili kujua undani wak...
22/07/2024

๐Ÿ“ŒNiliamua kupita kwenye page kadhaa ikiwemo Samson Charles , Malisa GJ, East Africa TV, millard ayo ili kujua undani wake na hiki ndicho nilichokutana nacho, Boniface Mwaitege Yuko hai.

NB:
Ukiona taarifa usiwahie kupost ili upate Likes na Comment nyingi, thibitisha kwanza ndipo upost itakuongezea credit kuliko kukurupuka....

Aritz Adorrs : โ€œ Kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid C.F. nilimpiga kichwani Kepler Lima(Pepe) kisha Sergio Ramos akanifu...
20/06/2024

Aritz Adorrs : โ€œ Kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid C.F. nilimpiga kichwani Kepler Lima(Pepe) kisha Sergio Ramos akanifuata na kuniuliza, โ€œUnataka kutoka ndani ya uwanja kwa lift au Ambulance?" Nikamuuliza kwanini unaniuliza swali hilo Sergi? Akajibu, โ€œKwasababu Pepe amenituma nikuulize"

Niliogopa na kumfuata kocha na kumuomba anibadilishe (Substitute) kocha akajibu, โ€œTumefika ukomo wa substitution." Kisha nikarudi kwa Sergio Ramos na kumwambia, "Nahitaji kuondoka kwa liftโ€ Sergio Ramos akatabasamu na kumkimbilia Pepe kumwambia nilichosema, dakika chache baadae mchezaji mwenzangu akanipa pass nikawaona Pepe na Sergio Ramos wakinijia kwa kasi, ninachokumbuka ni jinsi nilivyodondoka na nilipoamka nilijikuta nipo hospitali."

"Huo ndiyo ulikuwa mchezo wangu wa mwisho k**a mchezaji. "

โš Pole kwa familia lakini kuna jambo moja la msingi sana lakujifunza.๐Ÿ”ดMadereva wa serikali kila uchwao mnaaswa, mnaelezwa...
19/06/2024

โš Pole kwa familia lakini kuna jambo moja la msingi sana lakujifunza.

๐Ÿ”ดMadereva wa serikali kila uchwao mnaaswa, mnaelezwa, mnaonywa, mnalalamikiwa lakini hamsikii mnakuwa na viburi eti kwasababu unaendesha gari ya Serikali au umembeba kiongozi hivyo unaona ni haki yako kutoheshimu sheria za usalama barabarani!
Maajabu mengine hata hao viongozi wamefanana na madereva wao, nao wamekuwa wakipuuza sheria, wakiwahimiza madereva kufanya makosa.

๐Ÿ”ดKumekuwa na mijadala lukuki kuhusu madereva wa serikali, kumekuwa na malalamiko maelfu kwa maelfu kwa madereva wa gari za serikali. Wananchi wengi wamekuwa wakitoa malalamiko jinsi gani gari za serikali zinavyovunja sheria, zinavyokosakosa wananchi kuwagonga na mwishowe zinasababisha ajali mbaya k**a hii.

๐Ÿ”ดSi madereva wote wa gari za serikali ni kero barabarani, ila baadhi yao. Si mnakumbuka yule dereva wa serikali aliyeingia kwenye 18 za afande Muslim? Aliendesha gari mwendo kasi ndani akiwa amebeba wataalamu fulani, akak**atwa na polisi kikosi cha usalama barabarani.

๐Ÿ”ดVipi kuhusu yule dereva wa gari ya serikali aliyekuwa amelewa chakali, akawa anaendesha gari ya serikali, akamgonga dereva wa bodaboda.

๐Ÿ”ดMnakumbuka pale Arusha miezi miwili iliyopita gari ya serikali imemgonga dereva wa bodaboda na kumburuza?

๐Ÿ”ด Mnakumbuka ajali iliyomuua mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga mkoani Tabora kule Mbeya? Askari polisi walimzuia na kumuelekeza kufuata utaratibu wa kupita eneo husika lakini alipuuza matokeo yake ni ajali iliyowaua Mkurugenzi na dereva.

๐Ÿ”ดNa sasa ni hii iliyochukua uhai wa RAS!

โžกSwali langu ni, kwanini madereva wa gari za serikali mnakuwa na mapuuza?

โžกKwanini viongozi wanaokuwa ndani ya hizo gari hawawazuii madereva kufanya makosa?

โžกJe, madereva wa gari za Serikali wako juu ya sheria?

๐Ÿ“ŒMwisho ifike wakati ieleweke, ajali ya gari inapotojea inaleta madhara makubwa kwa taifa, jamii na familia kwa ujumla. Ajali inapotokea kunakuwepo na uharibifu wa mali ikiwemo gari lenyewe, miundombinu ya barabara na mali nyingine.

๐Ÿ“ŒMadhara mengine ambayo ni makubwa zaidi ni uhai kupotea, nguvu kazi kupotea. Lakini pia familia zinapoteza baba/mama ni majonzi kwa familia.

๐Ÿ–‹Rai yangu kwetu sote madereva, tuwe makini tuwapo barabarani, tufuate sheria za usalama barabarani iwe ni dereva wa serikali au gari binafsi sote tunawajibu wa kutii sheria.
Sote kwa pamoja tunalojukumu la kumlinda mtumiaji mwenzetu wa barabara.

MUNGU AWAPE FARAJA WAFIWA WOTE NA AWATIE NGUVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU...AMEN๐Ÿ™๐Ÿพ

๐Ÿšจ๐”๐’๐€๐‹๐€๐Œ๐€โš ๏ธโšชBajaji na Boda boda ni watu muhimu sana kwenye maisha na shughuli zetu za kila siku.๐Ÿ”ดLakini si kila bodaboda/...
06/05/2024

๐Ÿšจ๐”๐’๐€๐‹๐€๐Œ๐€โš ๏ธ

โšชBajaji na Boda boda ni watu muhimu sana kwenye maisha na shughuli zetu za kila siku.

๐Ÿ”ดLakini si kila bodaboda/bajaji ni mwema.

โšชHakikisha unapotumia usafiri huu, haufiki nyumbani kabisa, ni kheri akakushushia njiani karibu na nyumbani na ukatembea kwa miguu hadi kwako.

๐ŸŸกSi kila dereva bajaji/bodaboda ni mbaya au anatabia mbaya au si mwaminifu, hapana, ila kuchukya tahadhali ni muhimu.

๐Ÿ“Œ๐™๐ข๐ง๐ ๐š๐ญ๐ข๐š ๐ก๐ข๐ฅ๐ข, ๐ฎ๐ญ๐š๐ง๐ข๐ฌ๐ก๐ฎ๐ค๐ฎ๐ซ๐ฎ ๐›๐š๐š๐๐š๐ž!

ยฉ๐†๐ž๐จ๐Ÿ๐ซ๐ž๐ฒ๐ƒ๐ข๐ฌ๐ฆ๐š๐ฌ

๐Ÿ˜ญ๐Œ๐’๐ˆ๐๐€ ๐Œ๐–๐ˆ๐๐†๐ˆ๐๐„ ๐๐Ž๐‹๐‹๐˜๐–๐Ž๐Ž๐ƒ๐Ÿ˜ญ๐Šwa mara nyingine tena Nollywood inaingia katika msiba mzito   baada ya kifo cha Mwigizaji ngu...
11/04/2024

๐Ÿ˜ญ๐Œ๐’๐ˆ๐๐€ ๐Œ๐–๐ˆ๐๐†๐ˆ๐๐„ ๐๐Ž๐‹๐‹๐˜๐–๐Ž๐Ž๐ƒ๐Ÿ˜ญ

๐Šwa mara nyingine tena Nollywood inaingia katika msiba mzito baada ya kifo cha Mwigizaji nguli kutoka nchini Nigeria aitwaye ๐‰ohn ๐aul ๐Ždonwodo maarufu k**a ๐ope ๐‰r.

Kifo cha ๐‘ท๐’๐’‘๐’† ๐‘ฑ๐’“ kimetokea siku ya Jumatano baada ya boti ndogo waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika mto Niger walipokuwa wakielekea Location kurekodi movie iitwayo โ€œThe Other Side of Life" ya kwake ๐€danma ๐„luke ambaye ni producer wa filamu hiyo. Taarifa zinaeleza kuwa, katika boti hiyo kulikuwa na watu wengine 15 akiwemo mwigizaji TC Virus, waliofariki pamoja na Pope ni watatu huku watatu wengine wakiwa hawajulikani walipo.

๐Š๐”๐€๐๐™๐€ ๐Š๐”๐ˆ๐†๐ˆ๐™๐€
Pope Jr aliingia katika ulimwengu wa filamu mwaka 2006 lakini alianza kujulikana mwaka 2007 baada ya kuigiza filamu iliyoitwa Secret Adventure iliyoandaliwa na Tchidi Chekere. Ushiriki wake katika filamu hiyo ambayo aliitendea haki ulimfanya ajihakikishie ulaji ndani ya kiwanda cha filamu nchini humo maarufu k**a Nollywood kwani tangu mwaka 2007, Pope Jr amekwishaigiza filamu zipatazo 150 zikiwemo Bachelor's Eve, Bitter Generation, The Generals, Wrong Initiation, The Cat, Nwocha, Vengeance Bullet.

๐๐€๐€๐ƒ๐€ ๐˜๐€ ๐“๐€๐€๐‘๐ˆ๐…๐€ ๐Š๐”๐’๐€๐Œ๐๐€๐€
Baada ya taarifa za ajali ya boti yao kupata ajali kikosi cha polisi wanamaji kiliwasili katika eneo la tukio wakishirikiana na wavuvi waliweza kufanikiwa kuwaokoa watu kadhaa akiwemo Pope Jr ambaye aliokolewa na kukimbizwa hospitali akiwa katika hali mbaya.

Waigizaji wenzake akiwemo ๐‘egina ๐ƒaniels na mama yake aitwaye ๐‘ita ๐ƒaniels, rais wa shirikisho la waigizaji nchi nijeria โ€œAGNโ€ ๐„meka ๐‘olls na waigizaji wengine walikuwepo hospitali kuhakikisha chochote kinachohitajika kuokoa maisha ya Pope Jr kinapatikana lakini Mungu akampenda zaidi.

๐Œ๐€๐ˆ๐’๐‡๐€ ๐๐ˆ๐๐€๐…๐’๐ˆ
Mwaka 2014 John Paul Odonwodo alipata wakufanana naye hakuwa mwingine bali ni Jennifer Awele ambaye hadi mauti yanamkuta alijuwa amefanikiwa kupata watoto watatu na mkewe.

๐’๐€๐€ ๐‚๐‡๐€๐‚๐‡๐„ ๐Š๐€๐๐‹๐€ ๐˜๐€ ๐Š๐ˆ๐…๐Ž
Katika video ya mwisho aliyopost katika mtandao wa Instagram saa chache kabla ya kupata ajali aliyoiambatanisha na maneno, โ€œ๐‘ฏ๐’Š๐’Š ๐’๐’…๐’Š๐’š๐’ ๐’‰๐’‚๐’•๐’‚๐’“๐’Š ๐’•๐’–๐’๐’‚๐’Š๐’„๐’‰๐’–๐’Œ๐’–๐’‚ ๐’Š๐’๐’Š ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚๐’ƒ๐’–๐’“๐’–๐’…๐’Š๐’”๐’‰๐’‚โ€, Pope Jr alisikika akimueleza mwongoza chombo, โ€œ๐‘ป๐’‚๐’‡๐’‚๐’…๐’‰๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’‚๐’Œ๐’‚ ๐’‘๐’–๐’๐’ˆ๐’–๐’›๐’‚ ๐’Ž๐’˜๐’†๐’๐’…๐’, ๐’†๐’๐’…๐’†๐’”๐’‰๐’‚ ๐’•๐’‚๐’“๐’‚๐’•๐’Š๐’ƒ๐’–, ๐’Ž๐’Š๐’Ž๐’Š ๐’๐’Š ๐’Ž๐’•๐’๐’•๐’ ๐’˜๐’‚ ๐’‘๐’†๐’Œ๐’†๐’† ๐’Œ๐’˜๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’›๐’‚๐’›๐’Š ๐’˜๐’‚๐’๐’ˆ๐’–, ๐’๐’Š๐’๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’•๐’๐’•๐’ ๐’˜๐’‚๐’•๐’‚๐’•๐’– ๐’๐’‚๐’•๐’‚๐’Ž๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚๐’๐’๐’‚ ๐’˜๐’‚๐’Œ๐’Š๐’Œ๐’–๐’˜๐’‚ ๐’๐’‚ ๐’๐’Š๐’˜๐’† ๐’ƒ๐’‚๐’ƒ๐’‚ ๐’ƒ๐’๐’“๐’‚ ๐’Œ๐’˜๐’‚๐’. ๐‘ป๐’‚๐’‡๐’‚๐’…๐’‰๐’‚๐’๐’Š ๐’Œ๐’‚๐’Œ๐’‚ ๐’†๐’๐’…๐’†๐’”๐’‰๐’‚ ๐’•๐’‚๐’“๐’‚๐’•๐’Š๐’ƒ๐’–, ๐’€๐’†๐’”๐’– ๐’๐’Š๐’๐’Š ๐’‰๐’Š๐’Œ๐’Š...โ€

Wapenzi wa filamu, watu maarufu, Waigizaji mbalimbali nchini Nigeria wameendelea kutoa salamu za pole huku wengi wakionesha kush*tushwa na taarifa za msiba huo.

ส™แดกแด€ษดแด€ แด€สŸษชแด›แดแด€, ส™แดกแด€ษดแด€ แด€แดแด‡แด›แดกแด€แด€, แดŠษชษดแด€ สŸแด€แด‹แด‡ สŸษชส™แด€ส€ษชแด‹ษชแดกแด‡, แด€แดษชษด๐Ÿ™






๐ŸšจHawa mashabiki wa Trabzonspor hawatamsahau Bright Osayi-Samuel walipigwa goli 3 mujarabu wakaona wawe mabondia wakamvam...
22/03/2024

๐ŸšจHawa mashabiki wa Trabzonspor hawatamsahau Bright Osayi-Samuel walipigwa goli 3 mujarabu wakaona wawe mabondia wakamvamia Osayi na wenzake, akawakusanya k**a picha inavyoonekana hapo. Next time watawaza mara mbili kabla ya kugeuza uwanja wa soka kuwa ulingo wa ndondi.

11/03/2024

๐Š๐ฎ๐ญ๐จ๐ค๐š ๐ค๐ฐ๐š Malisa GJ

Mtoto Isaac Enock (miezi minne), mkazi wa kijiji cha Kondoa Wilaya ya Kilosa, Morogoro anapigania maisha yake katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Alizaliwa Novemba 2023, akiwa mzima lakini baada ya miezi miwili alianza kupumua kwa shida, kushindwa kunyonya na kutoka jasho sana. Tar 29 Januari 2024 alipelekwa hospitali ya wilaya ya Kilosa lakini hawakuona tatizo.

Alipewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa Morogoro akalazwa kwa siku 3 akifanyiwa vipimo. Majibu yakaonesha kuwa Isaac ana tatizo kwenye moyo na hivyo kupewa rufaa ya JKCI.

Alipofikishwa JKCI alifanyiwa vipimo upya na kugundulika kuwa na Tetralogy of Fallot (TOF), yani matatizo manne ya moyo yaliyounganika pamoja (combination of 4 congenital heart defects).

Matatizo hayo ni;
1. Pulmonary stenosis; yani mshipa mkubwa unaopeleka damu kwenye mapafu kushindwa kufanya kazi.
2. Ventricular septal defect (VSD); yani tundu kwenye moyo.
3. Overriding aorta; yani hitilafu kwenye mshipa mkubwa unaopeleka damu sehemu nyingine za mwili.
4. Hypertrophy of the right ventricle; yani kutanuka kwa chemba ya chini kulia ya moyo.

Isaac anahitaji upasuaji wa awamu mbili. Awamu ya kwanza ni "Temporary Shunt Operation" yani upasuaji wa kuimarisha mshipa mkubwa unaopeleka damu mwilini (aorta) na unaopeleka damu kwenye mapafu (pulmonary artery).

Awamu ya pili atafanyiwa TOF Complete Repair baada ya miezi 4. Upasuaji huu kwa muda mrefu umekua ukifanyika nje ya nchi; lakini kwa sasa unafanyika JKCI.

Kwa sasa Isaac anahitaji kufanyiwa Temporary Shunt Operation ili aweze kuimarika kiafya kabla ya kufanyiwa TOF Complete Repair.

Gharama za awamu ya kwanza ya upasuaji ni TZS 8M lakini familia yake ni duni sana kuweza kumudu gharama hizo. Baba yake ni kibarua kwenye mashamba ya mpunga huko Kilosa. Kutokana na hali yake kiuchumi aliandika barua ustawi wa jamii akapunguziwa hadi 3.5M ambazo hata hivyo ameshindwa kuzilipa.

Ukiguswa kuokoa maisha ya Isaac, tuma mchango wako kwenda M-PESA 0752581983, Tigopesa 0719744954, CRDB 0150633516500 Gifted Heart Foundation.

Address

Makambako
Njombe
59101

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HabariHub posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to HabariHub:

Share