Ufunuo TV

Ufunuo TV TV maalumu kwa Neno la Mungu kwa Watu wote Ulimwenguni

07/07/2024

Bwana Yesu apewe Sifa.

Karibuni Wana wa Ufalme.

Send a message to learn more

Bwana Yesu asifiwe Wapendwa. Kwasasa mutapata mafundisho Kila siku ya neno la MUNGU, kutoka kwa Mwalimu wa Neno la MUNGU...
07/07/2024

Bwana Yesu asifiwe Wapendwa.

Kwasasa mutapata mafundisho Kila siku ya neno la MUNGU, kutoka kwa Mwalimu wa Neno la MUNGU Mwl. "FIDELIS TEGEMEO JOHN"

Swali la Leo linajibiwa hivi, si kweli kwamba Wana wa Esrael hawakuwaoa Waafrica.

1. Yusufu mwana wa yakobo alioa mmisiri akiwa kwa farao.

2. Ibrahimu babu wa Imani alizaa na Hajri mjakazi wa sara. Hajri alikuwa anatoka misiri.

3. Suremani alizaa na malikia wa sheba. Leo hii sheba ni nchi ya Ethiopia.

4. Musa. Mke wa pili wa Musa alikuwa Mwafrica kutoka Kushi. Kushi Leo hii ni nchi ya Sudani. Tena baada ya kumuoa mtu mweusi kutoka Kushi, Miliamu akaanza kueneza uongo Musa amepotoka kuoa mtu mweusi, lakini maneno hayo MUNGU alikasirika na kumpiga ukoma Miliamu.

HESABU 12:1-15.

1 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

2 Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.

3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

4 Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.

5 Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.

6 Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.

7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;

8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

9 Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.

10 Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe k**a theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.

11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.

12 Nakusihi, asiwe k**a mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.

13 Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.

14 Bwana akamwambia Musa, Je! K**a baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.

15 Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.

MUHIMU: Hao ni baadhi tu wapo wengi sana, lakini wayahudi walizaa na waafrica na tena uzao huo ulitoa manabii wakubwa ambao walikuwa chotara waafrica na uyahudi.

Kwa Maswali wasiliana nami.

Simu & Whatsapp: 0785043326.

MUBARIKIWE SANA WANA WA UFALME:

Address

Nyegezi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufunuo TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share