
19/07/2025
Nahodha wa Simba Sc, Mohamed Hussein (Tshabalala) amefunga ukurasa wa utumishi wake klabuni hapo baada ya kuaga rasmi kuwa anaondoka klabu ya Simba kupitia barua kwa Wanasimba.
“Takribani miaka 11 ya Furaha, uzuni, Shangwe, vifijo, nderemo na masikitiko ndani ya Mbuga.
Kwa uaminifu mkubwa, weledi wa kiwango cha juu, Kuvuja jasho kuipigania nembo ya klabu ndio ulikuwa msingi na malengo.
Wahenga walisema kila lenye mwanzo halikosi mwisho na leo nawaaga rasmi.
Haya ni maamuzi yaliyolenga Maendeleo yangu binafsi, maslahi yangu binafsi na weledi wangu uliotukuka.
Nichukue fursa hii kuwashukuru viongozi, benchi la ufundi na operation staffs wote wa klabu ya Simba SC kwa kipindi chote cha kuhudumu ndani ya klabu.
Kipekee niwashukuru mashabiki kwa kuwa nami kipindi chote, k**a mnavyonipenda na mimi nawapenda pia na nina imani mtaendelea kuniunga mkono.
Naishukuru Management Yangu ikiongozwa na Carlos Carlos kwa ushirikiano mkubwa wa kipindi chote.” — ameandika Zimbwe Jr.
Jicho la maisha