28/03/2022                                                                            
                                    
                                                                            
                                            USIYOYAJUA KUHUSU RAIS VLADIMIR PUTIN, HANA MKE HAAMINI MTU 
Rais wa Russia, Vladimir Putin alizaliwa mwaka wa 1952 huko St. Petersburg (wakati huo ikiitwa Leningrad). Baada ya kuhitimu katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Leningrad, Putin alianza taaluma yake katika shirika la kijasusi la Russia (KGB) k**a afisa wa ujasusi mwaka 1975.
Putin alipanda vyeo haraka katika Serikali ya Russia baada ya kujiunga na utawala wa Rais Boris Yeltsin mwaka 1998, na kuwa waziri mkuu mwaka 1999 kabla ya kuwa rais. Putin aliteuliwa tena kuwa waziri mkuu wa Urusi mwaka 2008, na mwaka 2012 alichaguliwa kuwa Rais wa Urusi.
Kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mwaka 1991, alistaafu kutoka KGB akiwa na cheo cha kanali, na akarudi Leningrad k**a mfuasi wa Anatoly Sobchak (1937-2000), mwanasiasa huria. Katika uchaguzi wa mwisho k**a Meya wa Leningrad (1991), Putin alikua mkuu wake wa kitengo cha uhusiano wa mambo ya nje na Naibu Meya wa kwanza (1994).
Baada ya kushindwa kwa Sobchak mwaka 1996, Putin alijiuzulu wadhifa wake na kuhamia Moscow. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Usimamizi katika utawala wa Rais wa Boris Yeltsin, akisimamia uhusiano wa Kremlin na Serikali za Mkoa.
Muda mfupi baadaye, aliteuliwa kuwa mkuu wa Usalama wa Shirikisho, ambalo awali lilikuwa ni tawi la iliyokuwa KGB, na Mkuu wa Baraza la Usalama la Yeltsin.
Agosti 1999 Yeltsin alimfukuza Waziri Mkuu, Sergey Stapashin pamoja na Baraza lake la Mawaziri, na kumpandisha cheo Putin kuchukua nafasi yake.
Desemba 1999 Yeltsin alijiuzulu urais, na kumteua Putin kukaimu nafasi yake hadi uchaguzi rasmi ulipofanyika mapema mwaka 2000. Alichaguliwa tena mwaka wa 2004. Aprili 2005 alifanya ziara ya kihistoria nchini Israeli kwa mazungumzo na Waziri Mkuu Ariel Sharon, na hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi yeyote wa Kremlin.
Kwa sababu ya ukomo wa muda, Putin alilazimishwa kuacha urais mwaka 2008. Lakini alirudi kuhudumu k**a waziri mkuu wa Dmitry Medvedevhadi 2012 alipochaguliwa tena kuwa Rais wa Urusi.
Rais Vladimir Putin ni jasusi hatari Mtaalamu na mbobezi wa 'counterintelligence'
- Yuko single Hana Mke, aliachana na Mkewe Lyudmila Shkrebneva mwaka 2014 wakiwa na Watoto wawili, Maria na Katerina
Putin ana watoto Wawili, wote ni MABINTI. Binti yake Mkubwa anaitwa Maria(35) ni Daktari Bingwa wa Mifumo ya Homoni kwa watoto (pediatric endocrinologist) na mdogo wake anaitwa Katerina(33) ni Mruka sarakasi (acrobatic dancer).
:
Walikua siri kwa miaka mingi, wamefahamika miaka ya 2010's, Imekuwa k**a desturi ya Majasusi ama Viongozi wengi wakubwa duniani kuficha sana Historia za watoto wao.
- Ni Mtaalamu wa Martial Arts : Anashikilia mkanda mweusi wa Kyokushin. Pia yupo vizuri kwenye Judo na Sambo.
- Ni Rafiki mkubwa wa Roman Abrahmovich, Mmiliki wa klabu ya Chelsea Abrahmovich, ni mmoja ya Watu waliomsaidia Putin kuchukua madaraka Urusi na ni Mmoja Wafadhili wake muhimu.
Putin haamini mtu yeyote linapokuja suala la usalama hata mak**anda na viongozi wake waandamizi akikutana nao hukaa nao mbali mara zote hutumia meza ndefu mno ambayo huwatenga kwa umbali usiopungua mita tano. Huyo ndio Vladimir Putin. 
Baada ya kuzidiwa mkakati wa kimapambano ardhini nchini Ukraine vikosi vyake vinarusha makombora ovyo  kwenye mashule, hospitali na makazi ya watu na kuua raia wasio na hatia ikiwemo watoto. Anaendelea kukosa uungwaji mkono kitaifa na kimataifa jambo linalohatarisha hatima ya uongozi wake ikiwemo kuwepo tetesi za waandamizi wake kufikiria kumpindua. 
Kungi online news