TimesMajira

TimesMajira Kivuli Business Care Limited (KBC) is a Media House specializing in print media (newspapers) for the

09/12/2022

WADAU WA ELIMU NA VIONGOZI WA DINI WAKEMEA VIKALI UNYANYASAJI WA KIJINSIA

09/12/2022

UFUNGAJI WA MAONESHO YA SABA YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

09/12/2022

UFUNGAJI WA MAONESHO YA SABA YA BIDHAA ZA VIWANDA VYA TANZANIA

09/12/2022

Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) imewataka wazalishaji kuhakikisha bidhaa wanazozalisha ndani zinakidhi viwango lakini pia zinavutia wanunuzi hali itakayopelekea kuokoa matumizi ya fedha za kigeni, kuvutia wawekezaji nchini, kuongeza ajira kwa watanzania na kumlinda mlaji.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania, William Erio wakati wa maonesho ya saba ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yaliyoenda sambamba na kauli mbiu inayosema 'Nunua bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania', katika uwanja wa maonesho wa Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es salaam

"Kwa kufanya hivyo watafanya bidhaa za Tanzania kuwa nyingi na hata fedha za kigeni ambazo serikali inatumia katika kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi zikatumika kwa matumizi mengine ambayo hayapatikani hapa nchini k**a teknolojia yake ni kubwa bado haijafika na hivyo kuokoa matumizi ya fedha za kigeni na kuongeza ajira kwa watanzania kwasababu viwanda hivi lazima viajiri watu watakaofanya kazi"

Erio amesema Katika shughuli ya uzalishaji, kuna njia ya kupata mtaji kwa urahisi na teknolojia mpya inayoambatana na mtaji huo ambapo unaweza kupata kwa kuungana na kampuni nyingine na kuongeza uzalishaji ulionao lakini pia kuwashirikisha FCC ili mawazo hayo yaweze kupitishwa na kupelekea kufikia lengo la kutanua soko.

"Katika kufanya biashara unaweza ukahitaji nyongeza ya mtaji, au aina mpya ya teknolojia ambayo itakuwezesha biashara yako iwe nzuri zaidi ni lazima wakakope benki, unaweza ukapata mtaji mpya na teknolojia mpya kwa kuungana na kampuni nyingine ambapo hiyo ni kazi yetu FCC kuhakikisha kwamba katika mazingira k**a hayo mtu akipata muwekezaji anataka kupanua biashara yake au kuleta teknolojia anaweza akaja FCC tukamuwezesha kwa kupitisha mawazo yake na kumuwezesha kufikia hatua hiyo"

Pia Erio amesema wamekuwa wakitoa elimu husika kwa kuwafikia wazalishaji wakiwemo watu wenye ulemavu kwa kufanya ziara mbalimbali, kuwapa semina na kuwahamasisha kushiriki katika maonesho mbalimbali nchini.

08/12/2022

BENKI YA NMB "MASTABATA KOTEKOTE" YAENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI

NMB Tanzania

08/12/2022

MAHAFALI YA 46 YA TAASISI YA USTAWI WA JAMII YAFANA

08/12/2022

QATAR KULINOGA, WASHINDI WA "WAKISHUA TWENZETU QATAR NA HISENSE" WATUA DAR.

Tigo Tanzania

08/12/2022

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Tanzania(IAAT),Sayi Daudi alimuomba Kamishna huyo pindi sheria ya bima kwa wote itakapopitishwa mawakala wote waruhusiwe kuuza bima hiyo hasa ya afya Kwa umma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi.

Pia Daudi alitoa maombi mengine kwenye mamlaka hiyo kuwa
wapunguziwe gharama za usajili kutoka sh500,000 hadi kufika sh 250,000 na
mawakala hao wanatumia mifumo ya smartpolicy,vusha na bimapap wanaomba isajiliwe kwa wingi na iwe huru ili waweze kutumia walau mifumo miwili inapotokea umekorofisha utumike mwingine.

"Mpaka kufikia June 30 mwaka huu tulikuwa tumesajili wanachama 890 nchi nzima hivyo kuanzia Julai mwaka huu tumesajili mawakala wapya 160 Hadi sasa idadi ya wanachama imefikia 1050,"amesema Daudi.

08/12/2022

Mawakala wa bima Tanzania wametakiwa kuchangamkia fursa wakati tukielekea kuwa na bima ya afya kwa wote ili waongeze wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Akizungumza hayo leo Jumatano,Kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania,Baghayo Saqware alipokuwa akizindua mpango wa bima ya pole na mazishi, alisema matarajio ya serikali kuelekea kuwa na bima kwa wote mwaka 2023 hivyo mawakala hao wajiandae kuwa wauzaji wa bima hiyo.

Saqware amesema wakijidhatiti Kwa kuboresha huduma zao na kutengeneza mifumo ili kuwapata wateja wa bima hiyo serikali itahitaji wauzaji wawe wengi ili waweze kuwafuata wananchi hadi vijijini.

"Kuna fursa zitatokea mwaka 2023 ikiwemo bima ya afya kwa wote na bima za lazima k**a za vyombo vya majini wao k**a watoa huduma wachangamkie ili waongeze wigo wa upatikanaji wa huduma ya bima kwa wananchi,"amesema Saqware.

08/12/2022

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga ameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaovunja haki za binadamu lakini pia jamii kuwajibika kulinda haki za binadamu.

Aidha Henga amesema Juhudi madhubuti zinahitajika kupunguza masuala ya mauaji ikiwa ni pamoja na kuboresha masuala ya upepelezi na mahak**a lakini pia kuongeza uelewa kwa umma.

"Wao k**a asasi za kiraia waongeze juhudi za kuongeza uelewa kwa umma juu ya utaratibu za kisheria na masuala ya haki za binadamu"

Henga ameongeza kwamba "Haki ya kuwa huru dhidi ya ukatili, ukatili wa watoto umekuwa mkubwa sana na mbaya zaidi ukatili huo unafanywa na watu wa karibu, akiwemo baba mdogo, babu, baba mzazi, mjomba n.k , hivyo tunatakiwa kuwalinda watoto"

Legal and Human Rights Centre

Address

INDIA Street
Sea View
022

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TimesMajira posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TimesMajira:

Share