17/01/2026
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, linamshikilia Seke Mabirika Sesila, (45) mkazi wa kitongoji cha Tinda,kata ya Mwamabanza, wilaya ya Magu,kwa tuhuma za mauaji ya mke wake aitwaye Rahel Samwel (39) mkulima na mkazi wa kitongoji cha Tinda ,kata ya Mwamabanza, aliyeuawa kwa kushambuliwa kwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake.
Akitoa taarifa hiyo K**anda wa Polisi mkoani humo, Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo lilitokea Januari 15, 2025 baada ya kutokea kwa ugomvi wa kifamilia baina yao.
"Mtuhumiwa alimshambulia mke wake ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi miwili kwa mateke na ngumi sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni hali iliyosababisha kupoteza nguvu na hatimae kufariki dunia", amesema
βοΈ Melkizedeck Anthony.