09/12/2025
Mlinzi wa kati wa Simba SC Abdulrazack Hamza amekamilisha matibabu ya upasuaji wa goti uliofanyika nchini Morocco.
Nyota huyo aliyefanya vyema msimu uliopita akiwa na kikosi hicho alikuwa na jeraha hilo alilocheza nalo kwa muda mrefu.
Hamza amefanyiwa upasuaji huo Disemba mosi mwaka huu kufuatia kupata majeraha katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliofanyika Septemba 16 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Upasuaji huo umefanyika katika Kliniki ya Zerktouni ambayo pia mlinda mlango wa Simba SC, Moussa Camara alifanyiwa upasuaji wake hapo mwezi uliopita.
Sasa ni rasmi mlinzi huyo atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi nane kuendelea kuuguza jeraha hilo.