11/03/2025
Na: Yosia Emannuel
HAMISI MOHAMED Maarufu kwa jina la Kimondo, ni mlewavu wa Miguu aliyekulia kwenye familia ya wakulima na wafugaji, Katika Tarafa ya Ndago wilayani Iramba mkoani Singida.
Ngano za Wasemi husema kuwa "Mungu akikupa ukilema anakupa na mwendo", Licha ya Ulemavu alionao Mr. Kimondo, Mungu amemjaalia kipawa cha ubunifu wa zana mbalimbali za Chuma kupitia Uhunzi, ambao unamsaidia kuingiza kipato cha kila siku, na kuendesha familia yake ya watoto nane.
Ulemavu wa miguu Umekuwa ni Changamoto Iliyompa fursa na Upekee katika Bunifu zake, ukilinganisha na wabunifu wengine, kwani anaeleza kuwa changamoto ya Ulemavu alionao ulimpa Fursa ya kubuni na kuunda Ndege inayotumia Upepo.
"Nilikuwa nasimamia mifugo mbugani, eneo ambalo lilikuwa na matope sana, Ilinipa tabu kutembea kwenye matope, hivyo ilinifanya nibuni NDEGE Inayotumia upepo AIRPLANE ✈️ ilí niwe naruka matope na kutua kwenye nchi kavu kwa uharaka bila kuhangaika sana" Ameeleza Mr. Kimondo”
Mbunifu huyu hakuishia hapo, bali katika makala hii anaieleza kwamba, amewahi pia kubuni baiskeli za walemavu, na kuwasaidia walemavu wengi wilayani Iramba, Na sasa Amebuni zaidi ya pikipiki tatu za miguu mitatu zinazo wasaidia watu wenye ulemavu.
Changamoto kubwa anayopitia katika shughuli zake ni kukosa mtaji wa kutosha kwaajili ya kununulia vifaa chuma pamoja na mtambo wa kufua vyuma kwaajili ya ubunifu,
Mbunifu huyu Anatueleza kuwa amekata tamaa kufuatilia mikopo ya Asilimia 10, inayotolewa na halmashauri kwaajili ya walemavu, kwasababu ya mizunguko mingi na Masharti magumu ya mikopo.
Mr. Kimondo (jina lake Maarufu) Bado anaamini kwamba anabunifu nyingi anazoweza kuzifanya na kuwasaidia wengi zaidi. anawaomba watanzania na Serikali kumshika mkono, ili aweze kupata mtaji wa kununua zana chuma, ambazo zitamsaidia kubuni zana mbalimbali, za kilimo pamoja na Usafiri kwa walemavu.
UNAWEZA KUWASILIANA NAYE MOJA KWA MOJA AU KUMCHANGIA CHOCHOTE KUPITIA NAMBA YA SIMU YA VODACOM 0749277227, Namba ya Usajili wa Line M-PESA ni MAGRETH MKUMBO.
Na: Yosia Emannuel HAMISI MOHAMED Maarufu kwa jina la Kimondo, ni mlewavu wa Miguu aliyekulia kwenye familia ya wakulima na wafugaji, Katika Tarafa ya Ndag...