05/09/2021
*Wanawake ni Waalimu wa jamii – Mama Zuhra*
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zuhra Kassim Ali, amesema jitihada zinazooneshwa na wanawake wa kislamu hapa Zanzibar ni ishara kuwa jamii ya Wazanzibar wanaunga mkono jitihada za Serikali za kuleta maendeleo na ustawi wa jamii nchini na zitasaidia kuijenga jamii iliyo bora.
Mama Zuhra, ameyasema hayo leo huko Jumbi wilaya ya Magharibi ‘B’ Unguja, alipotoa salamu kwa wanawake wa kiislamu wa Madrasa ya Almujitahidina iliyopo Jumbi Uwandani, katika sherehe maalum zilizoandaliwa na madrasa hiyo za kuukaribisha mwaka mpya wa kiisalam wa 1443 Hijiria.
Amesema juhudi hizo za wanawake katika masuala mbali mbali ni muhimu sana katika kuchangia na kukuza jitihada za kuendeleza uislamu Zanzibar.
Aidha Mama Zuhra amesema kwamba amevutiwa sana na jitihada za wanawake wa madrasa hiyo za kujikwamua na utegemezi kwa kufanya shughuli mbali mbali za uzalishaji mali na maendeleo yao kwa lengo la kuondokana na umasikini.
Sambamba na kuunga mkono jitihada hizo, ameeleza kwamba ni muhimu kuendelezwa kwa juhudi kubwa, kwani zitasaidia kuwanyanyua kiuchumi wanawake na kuondokana na changamoto mbali mbali zinazowakabili katika kuendeleza maisha yao.
“Wanawake wa madrasa hii mumedhihirisha kwamba wanawake wa Zanzibar wanauwezo mkubwa wa kuisaidia jamii kuondokana na matatizo mbali mbali yakiwemo ya kifamilia,kiuchumi na kuijenga jamii iliyo bora".
Amesema pia madrsa hiyo tayari imeonesha kupata mafanikio ya kuibua vipaji mbali mbali k**a vile usomaji wa Quraan na hukumu zake, uoshaji maiti na mambo mengine mema, jambo ambalo ni muhimu katika harakati za kuendeleza mbele dini ya kiislamu hapa Zanzibar.
Aidha Mama Zuhra ameridhia ombi la ulezi wa madrasa hio na kuwataka watambue kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inathamini sana michango yao katika kuijenga jamii yenye amani na utulivu.
Pamoja na hayo Mama Zuhra ameahidi kushirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili madrasa hio ikiwemo ukarabati wa mabanda ya kusomea, umeme na kuongezewa mtaji wa fedha kwaajili ya kuendeleza shughuli za uzalishaji mali kwalengo la kujikimu.
Mapema kiongozi wa Madrasa h