Swahili Bollywood Mix

Swahili Bollywood Mix Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Swahili Bollywood Mix, Digital creator, Stone Town.

Mkongwe wa sinema za Bollywood, Aamir Khan, amewashangaza mashabiki zake baada ya kushea siri nzito kuhusu ndoa yake ya ...
21/04/2026

Mkongwe wa sinema za Bollywood, Aamir Khan, amewashangaza mashabiki zake baada ya kushea siri nzito kuhusu ndoa yake ya kwanza na Reena Dutta. Katika mahojiano na podikasti ya Raj Shamani, Aamir amesimulia jinsi walivyofunga pingu za maisha kwa siri kubwa na walitumia gharama nafuu.

Aamir alieleza kuwa mapenzi yake kwa Reena yalikuwa ya moto moto kiasi kwamba hakutaka kupoteza muda baada ya kufikisha umri wa kisheria wa kuoa. โ€œTulioana siku ileile ilipowezekana kisheria,โ€ alisema Aamir. Alitimiza umri wa miaka 21 mnamo Machi 1986 na alifunga ndoa Aprili 18, 1986, akiwa na Reena aliyekuwa na umri wa miaka 19 wakati huo.

Tofauti na harusi za kifahari za mastaa wa sasa, ndoa ya Aamir ilikuwa ya kipekee. Alieleza kuwa walipanda basi namba 211 kuelekea ofisi ya msajili wa ndoa. Gharama nzima ya sherehe hiyo, ikiwemo ada ya usajili na nauli, haikuzidi Rupia 10 za Kihindi.

Licha ya kuwa mke na mume, wawili hao walilazimika kuishi maisha ya siri kwa muda wa miaka miwili. Walichukua uamuzi huo ili kulinda kipaji cha Aamir kilichokuwa kikichipukia na kuepuka migogoro ya kifamilia kutokana na tofauti zao za kidini (Aamir akiwa Muislamu na Reena akiwa Mhindu). Kila mmoja alirudi kuishi kwa wazazi wake kana kwamba hakuna kilichotokea, huku marafiki wachache tu waliokuwa mashahidi ndio wakijua siri hiyo.

Ingawa safari yao ya ndoa ilifikia tamati mwaka 2002 baada ya miaka 16, Aamir amesisitiza kuwa Reena bado ni nguzo muhimu katika maisha yake. Alieleza kuwa heshima na urafiki walionao leo unatokana na msingi imara wa upendo walioujenga tangu wakiwa vijana wadogo wasio na kitu.

06/04/2026

Kumbe Akshay Kumar alikopi halafu hamsemi๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Unajuwa kwenye filamu ya Aankhen (1993), yule nyani alilipwa pesa ndefu kuliko waigizaji wakuu Chunky Panday na Govinda....
05/04/2026

Unajuwa kwenye filamu ya Aankhen (1993), yule nyani alilipwa pesa ndefu kuliko waigizaji wakuu Chunky Panday na Govinda. Chunky amethibitisha hilo wakati akifanya mahojiano na show ya Kapil Sharma (The Great Indian Kapil Show) mnamo Desemba 2024. Alisema

"Nyani alilipwa pesa nyingi sana kuliko mimi na Govinda kwenye filamu ya Aankhen"

Sasa jiulizeโ€ฆ ๐Ÿค”
K**a ungekuwa wewe kwenye nafasi yake, ungekubali kulipwa kidogo huku nyani anakula mshahara mkubwa kuliko wewe? ๐Ÿ˜…๐Ÿ‘‡

Tuambie maoni yako!

Muigizaji Sushmita Sen aliwahi kufunguka kwamba mapenzi yake kwa Salman Khan yalianza zamani sana, hata kabla hajapata u...
04/04/2026

Muigizaji Sushmita Sen aliwahi kufunguka kwamba mapenzi yake kwa Salman Khan yalianza zamani sana, hata kabla hajapata umaarufu. Alieleza kuwa alipokuwa bado yupo shuleni, alikuwa akitumia pesa yote ya matumizi aliyokuwa akipewa, na alikuwa akikununua picha za Salman na kuzipamba chumbani kwake. Alimpenda sana kiasi kwamba wazazi wake walikuwa wakimtishia kuziondoa picha hizo k**a hatakamilisha kazi zake za shule. Miaka kadhaa baadaye, aliishia kufanya naye kazi pamoja na kuwa marafiki wa karibu!

K**a wewe ni mfuatiliaji wa movie, tuambie - Sushmita na Salman walikutana kwenye movie gani?

Staa wa Bollywood, Kajol Devgan, ameweka wazi msimamo wake wa kutounga mkono mpango wowote wa kutengeneza upya (remake) ...
03/04/2026

Staa wa Bollywood, Kajol Devgan, ameweka wazi msimamo wake wa kutounga mkono mpango wowote wa kutengeneza upya (remake) filamu ya Dilwale Dulhania Le Jayenge (DDLJ) ya mwaka 1995.

Akizungumza katika mahojiano na shirika la habari la Indo-Asian News Service (IANS), Kajol ameeleza filamu hiyo ni moja ya kazi yake bora ambayo haiwezi kurudiwa na mwigizaji yeyote katika kizazi cha sasa.

Kajol ameeleza kuwa mafanikio ya DDLJ yalitokana na mchanganyiko wa mazingira, hisia, na wakati maalum wa miaka ya tisini ambao haupo tena katika ulimwengu wa sasa wa kidijitali.

Ikumbukwe kuwa filamu ya Dilwale Dulhania Le Jayenge iliigizwa na Shah Rukh Khan k**a Raj Malhotra pamoja na mrembo Kajol Devgan chini ya Director Aditya Chopra

FAHAMU HAYA๐Ÿ‘‡

โœ”๏ธFilamu ya Dilwale Dulhania Le Jayenge, inashikilia rekodi ya kuwa filamu iliyoonyeshwa kwa muda mrefu sana katika kumbi za sinema nchini India (zaidi ya miaka 25).

โœ”๏ธWakati inatoka, iliweka rekodi ya kuwa filamu iliyopata tuzo nyingi zaidi za Filmfare (10) kwa wakati mmoja, ikiwemo Picha Bora, Muigizaji Bora wa Kiume (SRK), na Muigizaji Bora wa K**e (Kajol). Pia ilipata tuzo ya taifa (National Film Award) kupitia kipengele cha Best Popular Film Providing Wholesome Entertainment

โœ”๏ธDilwale Dulhania Le Jayenge inatajwa k**a moja ya filamu zenye mafanikio makubwa zaidi ya kifedha nchini India ikiwa na kiwango cha All-Time Blockbuster.

โœ”๏ธDilwale Dulhania Le Jayenge ilikuwa filamu ya pili katika historia ya India kuvuka mapato ya shilingi bilioni 27.97 (crore 100) duniani kote kwa thamani ya mwaka 1995.

โœ”๏ธDilwale Dulhania Le Jayenge inakadiriwa kuwa k**a ingepigwa mahesabu kwa mfumuko wa bei wa sasa, mapato yake yangezidi shilingi bilioni 139.84 (500 crore).

โœ”๏ธDilwale Dulhania Le Jayenge ni moja ya filamu tatu tu za Kihindi zilizojumuishwa katika kitabu cha 1001 Movies You Must See Before You.

โœ”๏ธDilwale Dulhania Le Jayenge ilishika nafasi ya 12 katika orodha ya British Film Institute (BFI) ya filamu bora zaidi za India za wakati wote.

K**a ungekuwa producer, ungewekeza kwenye kurudia Dilwale Dulhania Le Jayen ?

Leo wacha tuone Couple โค๏ธ gani inakubalika pale Bollywood ๐Ÿ˜๐Ÿ˜
31/03/2026

Leo wacha tuone Couple โค๏ธ gani inakubalika pale Bollywood ๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Mnamo Machi 2024, muigizaji maarufu wa Uturuki, Hande Erรงel anayefahamika sana k**a Hayat wa kwenye tamthilia ya Ask Laf...
31/03/2026

Mnamo Machi 2024, muigizaji maarufu wa Uturuki, Hande Erรงel anayefahamika sana k**a Hayat wa kwenye tamthilia ya Ask Laftan Anlamaz, alifika nchini India kwa mara ya kwanza kuhudhuria mkutano wa FICCI Frames 2024 mjini Mumbai.

Katika mahojiano yake na vyombo vya habari nchini humo, Hande aliulizwa kuhusu mtazamo wake juu ya tasnia ya filamu ya India (Bollywood). Bila kusita, mrembo huyo amewataja mastaa wawili wakubwa ambao ni ndoto yake kufanya nao kazi:

๐Ÿ•บ Hrithik Roshan (Greek God wa Bollywood)
๐Ÿ’ƒ Deepika Padukone (Queen of Bollywood)

Hande amendelea kusema kuwa anavutiwa sana na utamaduni wa India, densi zao, na uaminifu wa watu wa nchi hiyo.

Pia alikiri kuwa hakuwa anajua k**a ana mashabiki wengi kiasi hicho nchini India na amependa sana chakula cha Biryani! ๐Ÿ›โœจ

Vipi k**a Hande na Hrithik wakikutana kwenye filamu moja ya mapenzi au action? Itakuwaje wakuu? ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

Staa wa muziki wa kimataifa kutoka Nigeria, Rema, amefunguka kuhusu mapokezi makubwa aliyoyapata nchini India, akiwataja...
30/03/2026

Staa wa muziki wa kimataifa kutoka Nigeria, Rema, amefunguka kuhusu mapokezi makubwa aliyoyapata nchini India, akiwataja raia wa nchi hiyo kuwa miongoni mwa watu wakarimu zaidi duniani. Akizungumzia uzoefu wake wa ziara yake nchini humo, mwimbaji huyo wa wimbo uliovunja rekodi wa Calm Down amesema:

"Watu nchini India ni waajabu, ni wakarimu sana, wenye msaada, na wenye kupokea wageni vizuri. Nilihisi kana kwamba niko nyumbani."

Rema aliandika historia mwezi Mei 2023 kwa kuwa msanii wa kwanza wa Afrobeats kufanya ziara rasmi ya kimuziki nchini India (The Calm Down India Tour) iliyohusisha miji mitatu mikubwa: New Delhi, Mumbai, na Hyderabad.

Uhusiano wa Rema na taifa hilo ulikua zaidi mwezi Julai 2024, ambapo inaripotiwa alilipwa takriban Dola milioni 3 (zaidi ya Shilingi bilioni 8 za Kitanzania) kutumbuiza kwenye harusi ya mtoto wa bilionea namba moja Asia, Anant Ambani, iliyofanyika jijini Mumbai.

Muigizaji nguli wa filamu nchini India, Suniel Shetty, amefunguka sababu ya kusahaulika kwake kwenye tasnia ya filamu kw...
30/03/2026

Muigizaji nguli wa filamu nchini India, Suniel Shetty, amefunguka sababu ya kusahaulika kwake kwenye tasnia ya filamu kwa takriban miaka saba. Alisema wazi kuwa: "I messed up, that's why people forgot me for a while" (Nilikosea, ndiyo maana watu walinisahau kwa muda).

Kwanini Alisema Hivyo?
Suniel Shetty, alitamba sana miaka ya 90, ameweka wazi kuwa anguko lake halikusababishwa na mtu mwingine, bali na maamuzi yake mwenyewe. Alieleza kuwa kuna kipindi alijisahau na kuanza kuigiza filamu ambazo yeye mwenyewe anaziita takataka (trash films). Aliamini kuwa kuonekana kwenye filamu nyingi ndiyo njia ya kulifanya jina lake liwe maarufu, kumbe alikuwa anaharibu brand yake.

Sababu Tatu za Anguko Lake๐Ÿ‘‡

โœ”๏ธKufanya Kazi Chini ya Kiwango: Alianza kuchagua hadithi (scripts) mbovu ambazo hazikuwa na mvuto kwa mashabiki.

โœ”๏ธKukataa Mabadiliko: Wakati teknolojia na ladha ya watazamaji ikibadilika, yeye alibaki na mfumo ule ule wa kizamani wa Action Hero.

โœ”๏ธKupoteza Thamani Sokoni: Baada ya kutoa mfululizo wa filamu zilizofeli (flops), watayarishaji na mashabiki wakaanza kumpuuza.

Kurudi kwake (The Comeback):
Badala ya kulalamika, Shetty aliamua kukaa pembeni kuanzia mwaka 2014. Alitumia muda huo kufanya mazoezi ya mwili (fitness) na kujitathmini k**a shabiki. Aligundua kuwa ili urudi kwenye ubora, lazima ukubali kuwa umezingua. Leo hii, amerudi akiwa na mwonekano mpya na uigizaji wa kisasa zaidi.

K**A UNGEKUWA MSHAURI WA SUNIEL SHETTY 2014, UNGEMSHAURI KITU GANI?

Filamu ya Dhurandhar 2: The Revenge ya staa Ranveer Singh imekuwa gumzo kwenye masoko ya ndani pamoja na kimataifa. Just...
30/03/2026

Filamu ya Dhurandhar 2: The Revenge ya staa Ranveer Singh imekuwa gumzo kwenye masoko ya ndani pamoja na kimataifa. Just imagine, kwenye soko la Worldwide imekusanya takriban shilingi Bilioni 371.55 (โ‚น1,365 Crore) ndani ya siku 11 tu, na inakuwa ndio filamu ya kwanza ya Kihindi kufikia kiasi hicho kwa siku chache. Kasi hio ya kimbunga imeanza kuiweka hatarini rekodi ya muda mrefu ya filamu ya Dangal (2016) ya staa Aamir Khan, ambayo imeshikilia rekodi ya kuwa filamu iliyoingiza pesa nyingi kuliko filamu yoyote pale India kwa soko la Worldwide. Tazama takwimu zilivyo๐Ÿ‘‡

โœ”๏ธFILAMU ZA BOLLYWOOD ZILIZOINGIZA PESA NYINGI KWA SOKO LA WORLDWIDE ๐ŸŒŽ

1) Dangal - 2070.30 cr - Bilioni 563.54๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
2) Dhurandhar 2-1365 cr - Bilioni 371.55๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
3) Dhurandhar - 1356.58 cr - Bilioni 369.26๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
4) Jawan- 1151.73 cr - Bilioni 313.50๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
5) Pathaan -1050.30 cr - Bilioni 285.89๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
6) Bajrangi Bhaijaan - 969.6 cr - Bilioni 263.92๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
7) Animal - 917.82 cr - Bilioni 249.83๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
8) Secret Superstar - 95.70 cr - Bilioni 246.53๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
9) Stree 2- 884.45 cr - Bilioni 240.75๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
10) Chhaava -827.06 cr - Bilioni 225.12๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
11) PK - 769.89 cr - Bilioni 209.56๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
12) Gadar 2 - 691.08 cr - Bilioni 188.11๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
13) Sultan - 614.49 cr - Bilioni 167.26๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
14) Sanju - 586.85 cr - Bilioni 159.74๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
15) Saiyaara - 581.50 cr - Bilioni 158.28๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
16) Padmaavat - 571 cr - Bilioni 155.43๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

FILAMU ZA INDIA NZIMA ZILIZOINGIZA PESA NYINGI KWA SOKO LA WORLDWIDE ๐ŸŒŽ

1) Dangal - 2070.30 cr - Bilioni 563.54๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
2) Pushpa 2 - 1877.10 cr - Bilioni 510.95๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
3) Baahubali 2 - 1810 cr - Bilioni 492.68๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
4) RRR - 1387 cr - Bilioni 377.54๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
5) Dhurandhar 2- 1365 cr - Bilioni 371.55๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
6) Dhurandhar - 1356.58 cr - Bilioni 369.26๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
7) KGF Chapter 2-1230 cr - Bilioni 334.81๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
8) Jawan - 1151.73 cr - Bilioni 313.50๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
9) Kalki 2898 AD - 1140 cr - Bilioni 310.31๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
10) Pathaan - 1050.30 cr - Bilioni 285.89๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
11) Bajrangi Bhaijaan - 969.06 cr - Bilioni 263.78๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
12) Animal - 917.82 cr - Bilioni 249.83๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
13) Secret Superstar - 905.70 cr - Bilioni 246.53๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
14) Kantara: Chapter 1- 892 cr - Bilioni 242.80๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
15) Stree 2 - 884,45 cr - Bilioni 240.75๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
16) Chhaava - 827.06 cr - Bilioni 225.12๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Vipi Ranveer Singh ndio mfalme mpya wa masoko au tumuangalie tu kwanza๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Maoni yako ni yepi ?

Kati ya Katrina Kaif ๐Ÿ†š Aishwarya Rai๐ŸŒ๐Ÿ’–
30/03/2026

Kati ya Katrina Kaif ๐Ÿ†š Aishwarya Rai๐ŸŒ๐Ÿ’–

Muigizaji kutoka India, Randeep Hooda, ameweka wazi hisia zake za kusikitishwa na namna tasnia ya filamu ya Bollywood il...
30/03/2026

Muigizaji kutoka India, Randeep Hooda, ameweka wazi hisia zake za kusikitishwa na namna tasnia ya filamu ya Bollywood ilivyoshindwa kumsapoti wakati alipopata mafanikio makubwa ya kimataifa.

Randeep, ambaye alicheza k**a Saju Rav kwenye filamu maarufu ya Netflix ya Extraction (2020) akiwa na staa wa Hollywood Chris Hemsworth, anasema kuwa licha ya kazi hiyo kuwa kubwa na kusumbuwa mitaani Duniani kote, hakupewa pongezi wala ushirikiano wowote na mastaa wenzake wa nyumbani.

Randeep alisema, filamu hiyo ilihitaji maandalizi mazito ya kimwili na kiufundi, jambo ambalo lilimfanya asifiwe sana na wataalamu wa filamu kutoka Hollywood na hata wale wa tasnia ya filamu ya Kusini mwa India (South Cinema). Hata hivyo, ndani ya Bollywood, walikaa kimya k**a vile hakuna jambo kubwa lililotokea.

KWA WALE WALIOTAZAMA JAAT BASI MWAMBA WANAMJUWA NANI๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜

Sources๐Ÿ‘‰ Hindustan Times, Pinkvilla, pamoja na uchambuzi wa kina kutoka jarida la Outlook India.

Address

Stone Town

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Swahili Bollywood Mix posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share