Upcoming Journalist

Upcoming Journalist News Anchor+Sports Pundit+Journalist

21/05/2026
15/05/2026

Hii ni elimu kubwa mno kwa Watu wanaothamini Uhai wao na familia zao .

Tunapaswa kuiishi hii elimu,Nadhani majanga mbalimbali yanayotokana na Moto hasa wa majumbani tutayaepuka.

Asante sana Afande kwa Elimu Bora
Asanteni Sana Jeshi letu pendwa la nami nitakuwa barozi wa walimu huu🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
.....Ulikuwa unaijua Elimu huu?

11/05/2026

Celebrating my 2nd year on Facebook. Thank you for your continuing support. I could never have made it without you. 🙏🤗🎉

11/05/2026

wapi Tunaelekea Ndugu zangu,Hii siyo sawa hata kidogo 🫪🫪🫪

Huu ujinga siyo wa kupuuzwa 😭😭😭😭

Ni bora wangefanya haya wakiwa ndani ya jengo flani isije public lakini walikuwa public na k**a teknolojia ilivyo wameletwa mjini zaidi na bado wanafurahia 😭😭😭😭

Katika kipindi ambacho tunapaswa kulinda na kuheshimu Tamaduni na maadili ya jamii zetu ni hiki kipindi ambacho teknolojia inakuwa na kuenea kwa kasi

Mamlaka tafadhali fanyeni jambo sisi Watanzania hatuna maadili ya namna hii😭😭😭

Mama yangu Mheshimiwa tafadhali mama

09/05/2026

TAHARUKI: NYOTA WANNE WA AZAM FC WAKIMBIZWA HOSPITALINI KWA DHANA YA KUPEWA SUMU

Hali ya taharuki imetanda ndani ya klabu ya Azam FC kufuatia ripoti za baadhi ya wachezaji wake tegemeo kuugua ghafla baada ya mchezo wa hivi karibuni dhidi ya TRA United ya Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mwanahabari mkongwe na mdau wa soka nchini, Jemedari Said, mshambuliaji wa klabu hiyo, Ashraf Kibeku, amelazwa katika Hospitali ya Saifee jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu ya dharura.

Inasadikika kuwa Kibeku pamoja na wachezaji wengine watatu walikumbwa na matatizo ya kiafya yanayodhaniwa kusababishwa na kuvuta hewa yenye sumu au kutumia chakula/kinywaji chenye viashiria vya sumu kabla au baada ya mchezo huo.

Wachezaji wengine waliotajwa kuathirika zaidi na tukio hilo ni pamoja na:
Feisal Salum 'Fei Toto'
Pascal Msindo
Lusajo Mwaikenda

Hadi sasa, uongozi wa Azam FC haujatoa taarifa rasmi ya kitabibu kuthibitisha chanzo cha tatizo hilo, huku mashabiki na wadau wa soka wakisubiri kwa hamu kujua hali za nyota hao ambao ni nguzo muhimu katika kikosi hicho na timu ya Taifa.

UEFA CHAMPIONS LEAGUE NUSU FAINALI Vikosi Vya Timu Zote Mbili Vinavyoanza katika Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ...
06/05/2026

UEFA CHAMPIONS LEAGUE NUSU FAINALI

Vikosi Vya Timu Zote Mbili Vinavyoanza katika Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya Nusu fainali mkondo wa pili, kati ya wenyeji Bayern Munich dhidi ya wageni wao PSG

Ikumbukwe katika mchezo wa mkondo wa Kwanza PSG waliibuka na ushindi wa mabao 5-4.

Nani kutinga Fainali?

NDOA YA PEDRO NA YANGA YAFIKA MWISHO Uongozi wa Klabu ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wao Pedro Go...
06/05/2026

NDOA YA PEDRO NA YANGA YAFIKA MWISHO

Uongozi wa Klabu ya Yanga umetangaza rasmi kuachana na aliyekuwa kocha wao Pedro Goncalves raia wa Angola.

Yanga wamefanya uamuzi huo ikiwa zimesalia mechi 9 Pekee kwa msimu kutamatika huku Yanga wakiwa ni Vinara.

Bila Shaka Mmeanza kutuelewa yale tunayoyasema kuhusu ubora na mbinu za makocha wa timu zenu.

Je ni sahihi kwa Yanga kuachana na Pedro?

LIGI KUU TANZANIA NBC FULL TIME KMC 0-1 YANGA ✅ Klabu ya wananchi Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa bao moja kwa ...
06/05/2026

LIGI KUU TANZANIA NBC

FULL TIME
KMC 0-1 YANGA

✅ Klabu ya wananchi Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi wa bao moja kwa Bila dhidi ya wenyeji wao klabu ya KMC Iliyopo nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi kuu.

✅Bao Pekee la ushindi limefungwa na Mchezaji kinda raia wa Uganda Allan Okelo.

Umevutiwa na kiwango cha Nani?

Asanteni sana Baba na Mama Kwa Juhudi zenu za kunileta Duniani.Asanteni sana Ndugu,Jamaa na Marafiki kwa kuendelea kuish...
02/05/2026

Asanteni sana Baba na Mama Kwa Juhudi zenu za kunileta Duniani.

Asanteni sana Ndugu,Jamaa na Marafiki kwa kuendelea kuishi nami pamoja na kuniamini.

Asanteni sana Mwenyezi Mungu kwa Neema na Rehema zako juu Yangu.

Happy Birthday To Me 🎂🎂🎂

Namba inayopokea ni ileile.

TOFAUTI YA LIGI YA MUUNGANO NA KOMBE LA MUUNGANO🏆.✅Ligi ya Muungano ilianzishwa mwaka 1982 ikiwa ni shindano kuu la soka...
01/05/2026

TOFAUTI YA LIGI YA MUUNGANO NA KOMBE LA MUUNGANO🏆.

✅Ligi ya Muungano ilianzishwa mwaka 1982 ikiwa ni shindano kuu la soka nchini lililounganisha timu bora kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

✅Lengo lake kuu lilikuwa kumpata bingwa mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye angeiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF). Ilikuwa ikichezwa kwa mfumo wa ligi na pointi, ikishirikisha timu nyingi zilizofanya vizuri kwenye ligi zao mama.

✅Ligi hii ilikufa rasmi mwaka 2003 kutokana na sababu za kiufundi na mabadiliko ya kisheria ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Sababu kubwa ilikuwa hitaji la Zanzibar kutambulika kimichezo ili timu zake zishiriki mashindano ya kimataifa moja kwa moja. Aidha, gharama kubwa za usafiri kwa timu kuvuka bahari mara kwa mara na muingiliano wa ratiba za ligi za ndani vilichangia kufutwa kwake.

✅Kombe la Muungano lina maana tofauti, kwani ni mashindano ya mwaliko ya muda mfupi yanayochezwa kwa mfumo wa mtoano (nusu fainali na fainali). Ingawa mashindano ya aina hii yamekuwa yakifanyika mara chache tangu miaka ya 1990, yalirudishwa rasmi kwa nguvu na mfumo wa kisasa mwaka 2024 wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano. Tofauti na ligi, shindano hili halitoi mwakilishi wa kwenda CAF, bali hutoa zawadi za fedha na heshima.

✅Malengo ya Kombe la Muungano ni kuimarisha mshik**ano, undugu, na kuenzi amani kati ya watu wa Tanzania Bara na Zanzibar kupitia sherehe za Aprili 26. Wakati Ligi ya Muungano ilikuwa na lengo la kitaalamu la kupata bingwa wa nchi, Kombe la Muungano lina lengo la kijamii na kiserikali la kudumisha tunu za taifa na kutoa burudani maalum wakati wa maadhimisho ya kitaifa.

Punguzeni ujuaji Bwana 🫪🫪🫪🫪

NB:
1.Yanga ametwaa ubingwa wa Ligi ya Muungano mara 6 huku Simba wakitwaa Ubingwa Huu mara 5.

2.Simba wametwaa Ubingwa wa Kombe La Muungano mara 2,huku Yanga wakitwaa Ubingwa Huu mara 1 Pekee.

Ulilijua hili?

Address

Sumbawanga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Upcoming Journalist posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share