Radio UHAI FM

Radio UHAI FM Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Radio UHAI FM, Radio Station, 4518, Tabora.

Redio Uhai ni redio ya Kikristo inayopatikana mjini Tabora,Tanzania ikiwa na lengo la kuelemisha jamii kupitia mafundisho ya Neno la Mungu na mfundisho mengine yenye lengo la kuifanya jamii iishi katika maisha ya upendo na Amani.

Kutoka Israel, Habari Njema zilianzia kuenea duniani. Leo, tunaendelea na utume huo kupitia Radio Uhai.Unapoiunga mkono ...
03/07/2026

Kutoka Israel, Habari Njema zilianzia kuenea duniani. Leo, tunaendelea na utume huo kupitia Radio Uhai.

Unapoiunga mkono Radio Uhai, unachangia kupeleka ujumbe wa wokovu kwa watu wengi zaidi.

Asante kwa kuwa sehemu ya kazi ya Mungu. 🙏📻

26/06/2026

Mkoa wa Tabora umetangazwa kushika nafasi ya pili Matokeo ya Mtihani wa Mock wa Darasa la Saba Mwaka 2026 Kanda ya Taaluma ya TASIDO inayounganisha mikoa ya Tabora, Singida, Iringa na Dodoma.

Akitoa taarifa hiyo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Elias Luvanda amesema Mkoa wa Tabora umefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kupata wastani wa asilimia 134.25, sawa na daraja C katika mtihani huo wa majaribio.

Luvanda ametoa wito kwa shule kutumia takwimu za matokeo kupanga afua za ufundishaji, ujifunzaji kuongeza ufatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi na kusimamia kwa karibu maeneo yanayohitaji msukumo zaidi husussani somo Kingereza na Hisabati kwani ufaulu wake umekuwa chini ya kiwango.

25/06/2026

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa huo Mariam Muhaji, kuwachukulia hatua watumishi wa idara ya afya wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu waliosababisha kuharibika kwa dawa za binadamu zenye thamani ya shilingi milioni 238.1, hali iliyosababisha baadhi ya wananchi kukosa huduma.

Sendiga ametoa agizo hilo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu kuhusu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ambapo licha ya halmashauri hiyo kupata hati safi, kulikuwa na zaidi ya hoja 20 za kufanyiwa kazi.

25/06/2026

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema vyombo vya usalama vimejipanga kikamilifu kulinda amani ya nchi, huku akiwahakikishia wananchi kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu.

Katambi ameyasema hayo wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya awali katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chogo kilichopo wilayani Handeni, mkoani Tanga.

25/06/2026

Serikali itaendelea kuhamasisha ufugaji wa kwenye vizimba kwa kuwaunganisha wanawake na taasisi za kifedha ili waweze kupata mitaji ya kuweza kutekeleza shughuli hiyo

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Lucy Mwakyembe wakati wa kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma.

23/06/2026

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime, amesema jeshi hilo limejifunza thamani ya upendo na ushirikiano uliopo kati ya askari polisi na wananchi, akieleza kuwa mahusiano hayo yamekuwa nguzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya kulinda amani na usalama nchini.

Misime ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Jeshi la Polisi katika misa ya kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi, SACP Richard Abwao, aliyefariki dunia Juni 20, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Amesema mchango na uhusiano mzuri alioujenga marehemu Abwao na wananchi utaendelea kuwa kumbukumbu muhimu ndani ya Jeshi la Polisi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshik**ano na ushirikiano kati ya jeshi hilo na jamii.

23/06/2026

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amesema mkoa huo utaendelea kuwa tulivu na salama, huku wananchi wakiendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi bila changamoto yoyote.

RC Chacha ameyasema hayo wakati akitoa salamu za mkoa katika misa ya kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, aliyefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili.

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa mkoani humo, huku akiwataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kulinda usalama wa mkoa.

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika Prof. Mohamed Janabi amesema mpango wa PEN-PLUS k**a mkakati muhim...
23/06/2026

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika Prof. Mohamed Janabi amesema mpango wa PEN-PLUS k**a mkakati muhimu wa kukabiliana na ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza barani Afrika.

Prof. Janabi amebainisha kuwa hatua hiyo ni msingi wa kuokoa maisha na kupunguza mzigo mkubwa unaoikabili sekta ya afya katika nchi zinazoendelea.

Akiongea Juni 23, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kimataifa wa PEN-PLUS unaorushwa kupitia TBC1, Prof. Janabi amesema magonjwa yasiyoambukiza k**a vile kisukari, shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, figo na saratani yamekuwa changamoto kubwa ya kiafya barani Afrika, na hivyo yanahitaji mkakati madhubuti unaowalenga wananchi katika ngazi ya huduma za msingi.

"Mpango wa PEN-PLUS unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwa kuzipeleka karibu zaidi na wananchi kupitia hospitali za wilaya na vituo vya afya, badala ya wagonjwa kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu katika hospitali kubwa za rufaa", amesema Prof. Janabi.

Amefafanua kuwa, hatua hiyo itasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na kuchelewa kupata matibabu pamoja na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya.

Serikali imeendelea kuimarisha usimamizi wa ajira za wageni nchini kwa lengo la kuhakikisha ajira hizo zinatolewa kwa ku...
23/06/2026

Serikali imeendelea kuimarisha usimamizi wa ajira za wageni nchini kwa lengo la kuhakikisha ajira hizo zinatolewa kwa kuzingatia sheria na wageni hao wanaoajiriwa wanamiliki vibali halali.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Dkt. Evaline Munisi amesema hayo Juni 23, 2026 Bungeni, Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mheshimiwa John John Nchimbi, Mbunge wa Nyasa, ambaye amehoji Je, nini kauli ya Serikali juu ya Wataalam wa kigeni wanaokaa muda mchache na kupatiwa Business Visa ambayo haitambuliwi na Idara ya Kazi.

Dkt. Munisi amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Ajira za Wageni, Sura ya 436, vibali vya kazi hutolewa kwa raia wa kigeni wenye mahusiano ya ajira na kampuni au taasisi zinazowaajiri nchini.

Aidha Dkt. Munisi ameonya vitendo vya baadhi ya watu (vishoka) wanaotumia mbinu zisizo halali kuwaleta wageni nchini kwa ajili ya kufanya kazi kinyume cha taratibu, pamoja na kuwawezesha kuendelea kufanya kazi baada ya mikataba yao kuisha kwa kuwatoa nje ya nchi na kurejea tena kwa kutumia pasi nyingine za kuingia nchini. Ameongeza kuwa, Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote au taasisi itakayobainika kukiuka sheria na taratibu za ajira za wageni.

23/06/2026

MHASHAMU JOSAPHAT BUDUDU - ASKOFU MSAIDIZI JIMBO KUU KATOLIKI TABORA AKITOA SALAMU ZA KANISA KWA NIABA YA MUADHAMA PROTASE KADINALI RUGAMBWA KATIKA MISA YA KUMUAGA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA TABORA SACP RICHARD ABWAO.

SACP Abwao alifariki dunia Juni 20, 2026 wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tiafa ya Muhimbili.

Address

4518
Tabora

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Radio UHAI FM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Radio UHAI FM:

Shortcuts

Share

Category