SimuliziMax

SimuliziMax GodstarFlix has a broad library of highlight films, narratives, TV shows, and so on!

NYUMBA JUU YA KABURISEHEMU YA TANOIlipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 04“Unamkumbuka Zena?” nilimuuliza, alionekana kutafaka...
24/10/2025

NYUMBA JUU YA KABURI
SEHEMU YA TANO

Ilipoishia Nyumba Juu Ya Kaburi 04

“Unamkumbuka Zena?” nilimuuliza, alionekana kutafakari kidogo kisha akaniuliza “Yule rafiki yako?”

“Ndiyo!”

“Kimetokea nini?” aliniuliza kwa shahuku kubwa sana, sura ya Mama yangu haikua na hatia lakini nilijiuliza maswali mengi, nilijiuliza k**a kweli hafahamu chochote vipi kuhusu jana Usiku walipotoka kwenye lile shimo yeye na Baba, wana uhusiano gani na Mwanamke anayelia kwenye ile stoo? . Endelea

SEHEMU YA NNE

“Amefariki Mama” nilisema kwa sauti ya kilio. Mama alishtuka sana kuliko kawaida, alishtuka k**a vile alimfahamu Zena kwa muda mrefu sana, alishika kifua chake hadi nilishtuka

“Mama‼” nilimwita sababu namna alivyoipokea taarifa alikua k**a amepandwa na presha. Alinitazama

“Pole Binti yangu, pokea rambirambi zangu” alisema kwa sauti ya upole sana kisha alisimama. Nilikua namtazama Mama yangu k**a vile ilikua ndiyo mara ya kwanza namwona, alivyobadilika ghafla alizidi kunipa mawazo zaidi.

Simu yangu ilianza kuita tena, pochi yangu ilikua karibu na Mama yangu. Akanipatia Pochi, niliona ni bora niitoe simu niipokee, ilikua ni Namba ngeni. Kilichokua akilini mwangu niliwaza huwenda napewa ratiba za mazishi ya Zena, taratibu niliipokea na kuiweka sikioni bila kusema chochote, niliisikia sauti ya kiume ikiniuliza

“Wewe ni Celin?” moyo wangu ulifanya paaa k**a nimewagiwa na maji, nilisimama “Eeh Ni Mimi!”

“Mimi ni Msamalia mwema, nimemsaidia rafiki yako Caren alikua amepata ajali mbaya sana jana Usiku. Yupo hapa Hospitalini, namba hii nimeikuta kwenye simu yake ndogo nikaona nikueleze k**a unaweza kuja hapa Hospitali ya Jiji” Moyo wangu ulianza kunienda mbio, niliyakumbuka maneno ya Yule Bibi wa ajabu kua nitapoteza niwapendao kwa Mpigo.

Nguvu ziliniisha, nilijikuta nikiidondosha simu sakafuni kisha niliketi kitini k**a mzigo. Macho yangu niliyaelekezea chini, chozi la ajabu lilinitoka. Nilijikuta nina hatia kubwa sana kwa kumshirikisha Caren kwenye hili jambo. Upepo ulianza taratibu huku ukipeperusha pazia, Mama yangu alinisogelea kwa utaratibu sana akaniuliza

“Kuna nini Celin?” nilimeza mate, nilikua k**a Zezeta. Nilinyanyua macho yangu taratibu yakiwa yamejawa na uzito wa chozi lililoganda machoni pangu. Nilimtazama Mama yangu k**a Mtu niliyepooza mwili mzima nikamwambia

“Caren‼” Mama alinitikisa kunirudisha kwenye ufahamu wangu lakini juhudi zake hazikufua dafu, uono ulinikimbia. Kila kitu nilikiona kipo mbali, hata pumzi zangu zilianza kunisaliti taratibu, niliona giza huku nikihisi ubaridi mwilini mwangu. Nilipoteza fahamu mikononi mwa Mama yangu.

****

Nilianza kusikia sauti inayofanana na kengele, sauti ilizagaa kichwa kizima. Ghafla nilishtuka, nilizinduka kutoka Usingizini. Mwili ulikua unauma, nilikua mchovu sana. Niliangaza huku na kule, niligundua nilikua kwenye chumba cha Hospitali, nilikua kitandani. Macho yangu yalikutana na macho ya Baba yangu pamoja na Mama yangu.

Mmoja aliketi upande wa kulia na mwingine aliketi upande wa kushoto, wote walionekana kunisubiria niamke. Nilipotaka kujitingisha Baba yangu alinizuia

“Taratibu Celin” alisema kwa sauti ya kujali sana. Hakuna kilichokua kimbebadilika kichwani kwangu. Nilijiuliza k**a nilikua nawafahamu vyema wazazi wangu, nilitikisa kichwa kwa mbali kua nilikua sijawafahamu vizuri wazazi wangu. Hapo hapo niliikumbuka sababu ya Mimi kuwepo Hospitali, ni simu ile niliyopigiwa kuhusu Caren

Nilihema kwa uchovu, halafu nikamtazama Mama maana yeye ndiye aliyekua na Mimi wakati napoteza fahamu.

Mama yangu aliyasoma Mawazo yangu akawa wa kwanza kusema.

“Celin‼” aliniita Mama, niliiona sura yake ilivyojaa upole na unyongefu uliopitiliza, alituma ujumbe kwa sura yake nikajua fika kua Caren alikua amefariki kutokana na ile ajali, Mama yangu alinitazama kwa jicho la kunipa pole. Alikua akipepesa macho yake, aligeuza shingo na kumtazama Baba yangu.

Baba naye aligeuza shingo yake na kunitazama, alikua na sura ile ile aliyonayo Mama yangu. Sura zao zilikua zimejaa huzuni na huruma. Baba alinishika mkono wangu uliokua una sindano iliyotumika kunipatia maji mwilini.

“Celin, pole sana. Umepoteza marafiki wawili ndani ya siku mbili” alisema Baba kwa sauti ya Upole sana, sura yake ilijaa huruma sana. Hawakuonekana k**a wana hatia lakini kwanini walikua kwenye lile shimo kule stoo, kuna uhusiano gani kati yao na yule Mwanamke anayelia. Swali hili lilihitaji majibu ya haraka, siyo rahisi wao wakanipatia Majibu.

Chozi lilianza kunidondoka, macho yangu yalianza kuwasha taratibu huku chozi likidondoka taratibu. Zena na Caren walikua marafiki wazuri kwangu lakini kila kitu kiliharibika baada ya Wazazi wangu kununua nyumba Mjini.

“Celin Binti yangu, najua unavyojisikia. Kupoteza uwapendao kunaumiza sana” alisema Mama yangu akinitazama kwa sura ile ile. Niliitikia kwa kutumia kichwa changu, sauti haikutoka kabisa. Nilijihisi ni mwenye hatia, Caren alikufa kwasababu yangu k**a ningemzuia asiondoke Usiku ule basi asingepata ajali iliyopelekea kifo chake. Nililia sana lakini sikuwa na uwezo wa kurudisha wakati nyuma.

Mchana wa siku hiyo niliruhusiwa kutoka Hospitalini, nilirudishwa nyumbani na Wazazi wangu. Mwili ulikua na uchovu sana, sikuweza kwenda Kumzika Zena maana alizikwa nikiwa Hospitali, hata Sikuwahi kwenda kuuaga mwili wa Caren ambao ulisafirishwa mara moja kuelekea Mji wa Wazazi wake ambako ndiko wanakozikia ndugu zao.

Nilibakia nikiwa mpweke kuliko wakati wowote kwenye Maisha yangu. Mama yangu alinitazama kwa ukaribu sana kwa siku mbili hadi alipothibitisha kua akili yangu ilianza kutulia.

Sikupata majibu ya maswali yangu hata pale niliporudi tena kule stoo sikuliona lile shimo, sauti ya Mwanamke anayeimba nayo ilitoweka kabisa

**

Zilipita siku kadhaa, nilianza tena kwenda chuo. Maisha yaliendelea bila Zena na Caren, Wanachuo wenzangu walinipa pole kwa kuondokewa na marafiki wawili niliowapenda.

Usiku mmoja nikiwa nimelala chumbani kwangu, nilianza kupata njozi ya ajabu sana. Niliota nikiwa ninalia halafu pembeni yangu kuna Mtu aliyejifinika shuka gubi gubi akiwa hatikisiki. Nililia sana, chozi lilinitoka huku nikiwa nimejawa na uchungu sana, njozi hii ilikua ikitokea

ndani ya chumba kimoja chenye kitanda cha Hospitali, Mtu aliye juu ya Kitanda alikua amefunikwa shuka jeupe.

Nilikua ninalia huku nikisema

“Usiniache nitabaki na Nani Mimi, usiende nakuomba rudi” Sijui nilikua namlilia Nani, ghafla nilishtuka kutoka Usingizini,niliketi nikiwa nina pumua haraka haraka. Chumba changu kilikua giza kidogo, nilisimama baadaye na kuwasha taa. Japo nilipata ndoto ya kutisha lakini Usingizi ulikua mwingi machoni pangu

Nilijivuta ili nielekee chini kupata maji ya kunywa, nilijifunga vizuri nguo yangu ya kulalia, wakati nauelekea Mlango nilianza kusikia sauti ya Mwanamke mmoja, ilikua ni sauti ile ile ya Mwanamke anayeimba lakini safari hii alikua akilia, nilishtuka sana. Nilipigwa na Butwaa huku nikisikia vyema kua ilikua ikitokea nje ya Mlango wa chumba changu.

Hata mate hayakuweza kupita kooni kwa jinsi ambavyo nilikua nimejawa na hofu, nilitamani kugumia kuwaita Wazazi wangu lakini sikuweza, butwaa iliyokua imeniingia akilini ilinifanya nitulie kimya nikisikiliza ile sauti. Wakati naendelea kuisikiliza ile sauti nilianza kuhisi ilikua ni sauti ya Mtu ninaye mfahamu

“Mamaaa‼” nilipata jibu, ilikua ni sauti ya Mama yangu Mzazi. Alikua akilia kisha alianza kuniita jina langu. Hofu ilizidi kuniingia, nilisimama nikiwa ninaangalia sana mlangoni. Nilitamani kumwita Mama na kumuuliza analia nini lakini nilipokumbuka nilichokiona Usiku ule nikiwa na Caren niliishiwa nguvu kabisa.

Aliendelea kulia huku akiniita kwa jina langu hali iliyoizidi kunichanganya, mwendo wa dakika tano tu kisha sauti ya Kilio iliondoka Mlangoni kwangu, nikawa naisikia ikishuka chini kupitia ngazi. Chozi lilinilenga sababu sikujua anayelia k**a alikua ni Mama yamgu kweli na k**a ni Mama yangu basi ndiye anayeleta Mauzauza.

Baada ya sekunde kadhaa ile sauti ilitoweka, palikua kimya sana. Sikupata Hata lepe la Usingizi, nilikesha nikiwa macho. Asubuhi mapema niliamka na kujiandaa kisha niliondoka nyumbani bila hata kuwaaga wazazi wangu, nilimpigia simu yule Dalali ili nimuulize maswali kadhaa, nilikua na uhakika hata yeye alikua anajua ni nyumba ya aina gani aliwauzia Wazazi wangu.

Wakati natoka niliitazama sana nyumba ya yule Mzee jirani, ilikua tulivu sana. Majani makavu yalikua yameanguka sana uwani kwake kuashiria kua palikua hapakaliwi na Mtu yeyote yule

Nilimpigia simu kwa namba ngeni, nilikua na uhakika k**a angelijuwa ni Mimi asingelinipa ushirikiano wowote ule. Nilimwambia kua nahitaji chumba cha kupanga, akanitajia mahali alipo huku akinisistiza kuwa niende hapo akanioneshe chumba kizuri. K**a kawaida yangu nilikua napendelea sana treni sababu ya kukwepa usumbufu.

Baada ya kufika eneo ambalo tulikubaliana tukutane, yeye sikumkuta hapo. Niliangaza huku na kule lakini sikufanikiwa kumwona, niliketi mahali nikimsubiria huku nikijaribu kumpigia simu lakini simu yake ilikua haipokelewi kwa zaidi ya dakika tano, mwanzo niliona ni jambo la kawaida lakini baadaye nilipata hisia ya tofauti.

Nusu saa nzima simu yake ilikua haipokelewi kisha baadaye ilizimwa kabisa. Mahali alipokua amenielekeza palikua ni Kijiwe cha kahawa, hapo ndipo anapopatikana kwani hata mara ya kwanza nilikutana naye hapo. Nilikata shauri la kuendelea kumsubiria hapo, nilinyanyuka na kuuvaa mkoba wangu ili niondoke

Mara akaja Mwanaume mmoja aliyekua akiendesha Pikipiki kwa kasi sana, japo alikua haji upande wangu lakini mwendo wake Ulinifanya niwe macho kumtazama. Aliegeshe Pikipiki kando kidogo ya kundi la Wanaume walioizunguka meza ya kahawa kisha akaketi huku akisikitika k**a Mtu aliyepoteza Umakini wake.

Nilinogewa na kuwatazama. Nilisimama nikiwa sikwepeshi macho yangu huku masikio yangu yakiwa k**a antena, walianza kumuuliza kwanini alikua katika ile hali ya kuchanganikiwa, akawa anajisonya-sonya tu huku akishikilia kichwa chake, walianza kumzingatia hata kwa wale walioanza kuhisi ulikua ni utani walianza kuweka Umakini huku wakizidi kumuuliza

“Sheby jamani‼” alianza kusema huku akihema sana.

“Sheby amefanya nini?” aliuliza mmoja wao akiwa anamtikisa bega, walionekana kumjua huyo Sheby na pengine alikua ni Mtu wao wa karibu.

“Sheby eeeee haaaaa‼” alitoa sauti kubwa iliyoambatana na kilio

“Sheby amefanya nini?” aliuliza mwingine, shahuku ikazidi kuwa kubwa, siyo kwao tu hata kwangu. Taratibu nilianza kupiga hatua ndogo za kuhebu ili nisikie neno.

“Amekufaa‼ ajali jamani aaaah Maisha hayaaa‼!” yule Mwanaume alizidi kuendelea kulia, Watu walisikitika sana kusikia taarifa za kifo cha huyo Mtu, papo hapo akili yangu ikakaa sawa‼ Yes, Dalali niliyewasiliana naye anaitwa Sheby. Nilihisi mwili k**a unatengana na roho yangu Jamani, nilikua na tumaini la kupata majibu ya maswali yangu kwa huyo Sheby halafu ghafla nasikia taarifa ya kifo chake.

Niliishiwa nguvu, nikasogea na kuketi juu ya gogo moja. Ndiyo maana simu zangu zilikua hazipokelewi, nilipata mfadhahiko mkubwa sana. Chozi lilikua likinimwagika, nilijuwa kua kuna

jambo lisilo la kawaida linaloondoa uhai wa Watu wasio na hatia, moyo wangu ulivunjika vipande vipande hata ile nguvu niliyokuja nayo ilipungua kabisa.

Nilitazama juu huku chozi likizidi kunibubujika kutoka machoni kuteremka hadi mashavuni kisha kwenye gauni langu, nilihisi Dunia ikizunguka. Nilikosa majibu ya maswali yangu yote, Uchungu ulipanda kutoka kifuani niliuhusi ukija hadi puani na kunipa maumivu makali sana. Hali ya mafua ya ghafla ilianza pale pale nikiwa bado kichwa changu kimeelekea juu.

Imani ya moyo wangu iliniambia kua Mungu alikua angani akinitazama kila hatua lakini hakutaka kunisaidia, nilisema ndani ya Moyo wangu.

“Eeh Mungu, nitapoteza wangapi? Hii ni ndoto, niamshe basi nikutane na wapendwa wangu” niliumia sana ndani ya moyo wangu, Mungu aliniachia mizigo yote niibebe mwenyewe katika wakati mgumu ambao kila niliyemshilisha alikufa kifo cha ghafla. Nilipoteza Watu watatu, mmoja ni dalali niliyeamini alikua akiyajua mazingira ya nyumba yetu na wengine ni marafiki zangu wawili niliowapenda k**a nilivyozipenda mboni za macho yangu.

Ghafla nilisikia sauti kando yangu, nilishtuka. Ilikua ni sauti ya kiume iliyoanza kwa utaratibu sana kisha kuniachia tabasamu la mwongeaji.

“Pole, haijalishi unapitia nini kwenye Maisha yako. Mungu atashinda na wewe” niligeuka haraka kumtazama aliyeongea, alikua upande wangu wa kulia, ni Mwanaume mwenye ndevu nyingi, mtanashati aliyenizidi Umri lakini alikua rika langu.

Nilisogea pembeni haraka kwa hofu maana sikutaka kumwamini Mtu yeyote yule.

“Usiogope Celin‼” Mungu wangu, alinifahamu kwa jina. Hii siyo tu ilinishtua pia iliniacha na Butwaa la ajabu sana, nikamkumbuka yule Bibi wa Ajabu ambaye alinisemesha kwenye treni na kuanzia hapo kila kitu kiliharibika.

“Tafadhali kaa mbali na Mimi, hunijui sikujui. Jina langu siyo Celin” nilisimama kisha nilipaza sauti yangu, kila mmoja aliye jirani na sisi alitutazama kwa Mshangao na maswali mengi. Yule Mwanaume wala hakujali, aliendelea kutabasamu na kunidhihirishia kua alikua Mtu wa ajabu k**a yule Bibi.

Niliondoka hapo haraka huku akiniita kwa jina langu akidai napaswa kumsikiliza, sikutaka hata kugeuka nyuma, niliyaziba masikio yangu ili hata kumbukumbu ya Sauti yake isibakie masikioni mwangu.

Nilipofika barabarani nilisimamisha Taxi ya njano kisha haraka nikaingia na kuketi siti ya nyuma kisha nikamuamuru dereva aondoe gari anipeleke chuoni, hapo chozi lilikua likinibubujika. Bado sauti yake ilikua inasikika masikioni mwangu. Maneno ya yule Mwanaume yalikua yakijirudia.

“Endesha haraka” nilisema kwa sauti ya juu ili dereva aongeze mwendo, nilikua nimegubikwa na woga wa ajabu, hofu na Mashaka vilikua vimenitawala kwa kiasi kikubwa sana. Nililia k**a

Mtoto mdogo, sikujua nilikosea kuichagua ile nyumba au kuna mahali familia yangu ilifanya kosa na sasa tunaadhibiwa.

Dereva aliongeza mwendo k**a ambavyo nilikua nimemwambia. Nilikua nimejiinamia nikiwa nimeziba masikio yangu, taratibu ile sauti ilianza kupotea masikioni mwangu. Zilipita dakika kadhaa ambazo zilitosha kwa dereva kukaribia chuoni. Nilijihisi nafuu sana, kisha nilitoa kitambaa na kujifuta chozi kisha nilifuta pua zangu.

Niliponyanyua Sura yangu nitazame nje nijuwe k**a tulikua tunakaribia chuoni au laa, nilipigwa na Butwaa nyingine. Nje ya gari palikua na Msitu mkubwa sana, halafu gari lilikua likitembea kwa mwendo wa kawaida.

Nilipaza sauti yangu “ Wewe dereva umenileta wapi huku?” nilisema huku nikijaribu kufungua mlango lakini ulikua umefungwa. Hofu niliyoiacha ilianza kunivaa upya halafu nikaisikia sauti ile ile ya yule Mwanaume niliyemkimbia akisema

“Haijalishi unapitia nini, kumbuka maneno yangu. Utashinda” Masikini, yule dereva alikua ni yule Mwanaume niliyemkimbia, aliwezaje kuingia ndani ya gari sijui, nitamkimbia vipi sijui na kwanini anajua kila kitu kuhusu Mimi pia sijui.

Nilikua ninatetemeka sana. Kisha lile gari likachepuka kutoka barabara kuu na kuingia barabara ya vumbi iliyo kimya sana, hapakua na yeyote.

“Wewe ni Nani?” nilimuuliza nikiwa ninalia, nilijua haiwezekani tena kumkimbia. Kwa namna alivyo siyo rahisi pia kupambana naye. Alisimamisha gari kisha aligeuka na kunitazama, sura yake ilionesha alikua na jambo kubwa analohitaji kuniambia.

Alinionesha sura ambayo haikua na hatia, wala hakuonesha k**a alikua na nia ya kunifanyia jambo baya, kisha kwa sauti ya taratibu aliniambia

“Usiniogope Celin, nahitaji Msaada wako. Nitakusaidia pi, tusaidiane” kauli hii ilianza kunipa tumaini la kuishi tena, k**a alihitaji msaada wangu asingeliweza kunidhuru lakini haraka haraka akiwa ananiangalia nilijiuliza alihitaji Msaada gani kutoka kwangu wakati yeye anaonekana kua ni Mtu wa ajabu ajabu k**a yule Bibi.

Nilibabaika kumjibu, sauti ilitoka kwa wasiwasi tena isiyo na nguvu. “Nikusaidie nini? Tafadhali usidhuru Maisha yangu” nilisema huku nikiwa ninalia, niliweka mikono yangu kifuani kwangu kwa isharaka ya kumwomba ahurumie Maisha yangu, alikuwa akinitazama nusu bega huku mwili wake wote ukitazama mbele.

“Ningekua na nia ya kuyadhuru Maisha yako ningefanya hivyo muda mrefu, nina ombi moja tu kwako Celin” Maneno ya yule yalianza kunipa tumaini zaidi na zaidi kua pengine nitapata nafasi nyingine ya kuishi, alionesha wazi kua alikua akinifwatilia kwa muda mrefu sana.

“Nitakusaidia nini Mimi Kaka yangu?” nilimuuliza, angalau swali hili lilitoka huku nikiwa nimetuliza kilio changu.

Alikunja midomo yake, ishara hii iliniambia ndani yangu kua alihitaji kuzungumza jambo zito sana, alitafakari huku akinitazama akiendelea kukunja midomo yake. Halafu akaniambia “Nataka umtoe Dada yangu ndani ya nyumba yenu”

“Dada yako?”

“Ndiyo!”

“Kivipi, ni yupi mbona sisi tunaishi watatu, Mimi na Wazazi wangu?” nilimuuliza huku moyo wangu ukiamini kua nilikua karibu kugundua siri fulani ya nyumba yetu. Alishusha pumzi zake kisha akaniambia

“Teremka kwenye gari, nitakueleza zaidi. Najua una maswali mengi sana” alisema kisha alifungua mlango wa gari kisha aliteremka na kusimama mbele ya gari akiegemea ‘Boneti’

Nilikua ninamtazama kwa makini nikiwa bado nina jishauri k**a nitaweza kumwamini Mtu nisiyemjua, lakini niliuvaa ujasiri wa ghafla kisha niliufungua mlango kirahisi sana, mlango uliokua Mgumu hapo awali, safari hii ulifunguka nilipoutekenya.

Sekunde kadhaa nilikua nikiivuta hewa ya jua kali lililokua likiwaka nje, niliyatazama mazingira tuliyopo. Niliona miti mingi iliyofungana, tulikua msituni japo kwa mbali nilisikia sauti ya magari yakitembea kwa kasi. Upepo wa taratibu ulikua ukiendelea na kufanya eneo hilo kua na hali mbili tofauti. Jua kali lakini pia upepo uliopoza joto kali

Taratibu nilitembea kuelekea mbele ya gari kumsikiliza yule Mwanaume, alikua mnene kiasi na pia alikua na ndevu nyingi mfupi wa wastani, alikua ananukia manukato makali sana. Nilitembea taratibu huku nikijikwaa jiwe dogo lililonipa mwendo zaidi hadi nilisogea kabisa karibu yake, akanipa pole huku akigeuka na kunitazama nikitembea taratibu hadi nilipofika mbele yake.

“Usiwe na wasiwasi Celin, usiogope sababu nusura ya Maisha yenu yapo mikononi mwako” niliyafinya macho yangu kwa mshangao mkubwa sana, moyo ulilipuka ghafla na kuanza kwenda mbio

“Unamaanisha nini?” nilimuuliza nikiwa na mhemko wa alichoniambia, tayari nilikua nimepoteza marafiki zangu wawili.

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya SITA

NYUMBA JUU YA KABURI SEHEMU YA NNEIlipoishia Sehemu Ya 3 Nyumba Juu Ya KaburiHata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha...
28/09/2025

NYUMBA JUU YA KABURI
SEHEMU YA NNE

Ilipoishia Sehemu Ya 3 Nyumba Juu Ya Kaburi

Hata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha nikaisikia sauti ya Caren

“Shii‼ ni Mimi” aliongea kwa sauti ya kunong’oneza. Aliniachia, hapo hapo kabla sijamuuliza alifikaje, sote tulimwona Yule Mzee akiwa ameshikilia tochi, alikua akichungulia pale mlangoni nilipotaka kuingilia, kwa namna nilivyomwona ni k**a alihisi uwepo wa Mtu. Alimulika tochi huku na kule lakini hakufanikiwa kutuona kisha aliufunga mlango wa Nyumba yake.

Hapo tuliachia pumzi ndefu maana tulikua tumezibana kuhofia asije akatushtukia. Endelea

SEHEMU YA NNE

“Unafanya nini hapa?” nilimuuliza Caren, sikutegemea angefika pale maana nilimpigia simu lakini hakushika simu yangu. Nilimuuliza kwa sauti ya chini sana, akanijibu

“Tutoke hapa Celin, turudi nyumbani kwenu tafadhali” ilionekana mpango wangu umeshindwa kufanya kazi usiku huu, basi taratibu tuliondoka. Tulilipanda lile geti tukatua upande wa pili kisha tulirudi nyumbani.

Tuliingia hadi chumbani kwangu, Nilikua na maswali mengi kwake. Alinitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaniambia

“Celin nashindwa kukuelewa, umenitumia ujumbe na kunieleza mahali ulipo ndiyo maana nilikuja, unaniuliza nimefikaje?” Nilitikisa kichwa changu, maneno ya Caren yalikua k**a yamejaa mzaha hivi

“Mimi?” nilimuuliza huku nikiwa najipiga kifuani.

“Caren, nilipiga simu yako hukushika. Sikutuma ujumbe wowote ule” Caren alitikisa kichwa chake akionesha wazi kua alikua akimaanisha alichoniambia, kisha alitoa simu yake na kunionesha ujumbe ambao alidai nilimtumia, ni kweli namba yangu ilionesha kumtumia ujumbe Caren. Macho yalinitoka, niliyapepesa huku nikihakiki. Funda zito la mate lilikua likipita kooni kwangu

“Caren, hali inaweza kua mbaya zaidi. Haya ni maajabu ya Dunia, sijakutumia ujumbe k**a huu. Nina hisia kuwa kuna mchezo wa kichawi unafanyika” nilisema.

“Wakati nakupigia simu nilisikia kitu cha ajabu sana chumba cha chini, hii nyumba inaweza kua na mizimu Caren. Unaweza ukaniamnini?”

“Celin, k**a unahisi hivyo ni bora ukawaambia Wazazi wako kabla mambo hayajawa mabaya zaidi. Sisi hatuwezi kupambana na hizo nguvu” alisema Caren, sura yake ilijaa hofu na woga sana, nilimuelewa. Nilimshika mkono nikamwambia huku nikimtazama usoni

“Baba yangu ana presha, sitaki kumtia matatizoni zaidi. Pesa yote ya kustaafu ameinunua hii nyumba. Nikimwambia ninaweza nikampoteza Caren, tafadhali tutafute ufumbuzi” nilimsistiza Caren, yeye alikua ndiye Mtu pekee niliyemueleza kuhusu nyumba hii mpya na mauza uza yake. Alitikisa kichwa akiitikia japo alikua na woga

“Tunaweza kwenda chini? Nilisikia sauti ya Mwanamke akiimba kutokea stoo, pengine tunaweza kupata majibu huko” Bado nilikua nimejawa na shahuku sana. Caren aliitikia kwa

kutumia kichwa huku jasho likimtiririka, basi tuliongozana kushuka ngazi taratibu hadi tulipofika chini, palikua giza sababu taa zote zilizimwa.

Pumzi za Caren zilikua juu sana, alikua akihema k**a Mtu aliyetoka kukimbia, hofu ilimjaa sana. Nikamwambia

“Usiogope Caren, hakuna tulichokosea hatustahili kuadhibiwa. Twende” nilisema, Binafsi nilikua na Ujasiri sana, sikutaka tuwashe taa sababu sikutaka Mama anikute tena pale pale aliponikuta na kuniuliza maswali. Miili yetu ilianza kusisimka kadili tulivyoisogelea stoo.

Hatua kadhaa mbele tulianza kusikia tena sauti ya Yule Mwanamke akiimba, ilikua ni sauti nyororo sana ikitokea stoo. Hatukuelewa alikua akiimba nyimbo gani wala lugha aliyoitumia kuimba hatukuijua. Hofu ilianza kuniingia lakini ilikua ni lazima nipate majibu ili kuwaokoa niwapendao.

Tulisimama tukiendelea kumsikia akiimba, ilionekana alikua ametulia sana, sauti yake ilikua ya taratibu iliyojaa upweke fulani ndani yake. Miili ilizidi kusisimka, hadi tunafika mlango wa stoo tulikua na miili mizito ambayo tuliisukuma kwenda mbele, msisimko ulikua wa ajabu sana ambao sikuwahi kuuhisi kabla yake.

Palikua na mwanga hafifu sana kutokea nje kupitia dirishani pale kwenye korido, taa ya nje ndiyo iliyokua ikiendelea kutupatia uelekeo. Niliuvuta mkono wangu huku nikisema liwalo na liwe, japo mkono ulikua mzito lakini nilifanikiwa kutekenya kitasa, mlango ukafunguka.

Pakawa kimya sana, hatukuisikia tena ile sauti ya Mwanamke akiimba, wala ile hali ya kusisimka mwili ilikua imetoweka, ni k**a tulikua tumevuka kizingiti kizito mbele yetu, nilikua wa kwanza kuingia stoo kisha nilipapasia na kuwasha taa, mwanga wa taa ukakita kila kona ya chumba cha stoo. Humo tulihifadhi baadhi ya vitu ambavyo hatuvitumii tena, vilikua vimetokea Kijijini na vingine tulivikuta baada ya kuhamia.

Chumba cha stoo kilikua kikubwa sana, kilikua na hewa, eneo kubwa la kuhifadhi vitu zaidi na zaidi. Caren naye aliingia akiwa anaogopa, nilianza kutafuta mahali ambapo ile sauti ilitokea, hapakua na yeyote ndani ya kile chumba.

“Si uliisikia sauti Caren?” nilimuuliza, alimeza mate kwanza kisha alinijibu akiwa bado anaendelea kuogopa

“Ndio ilitokea humu, Celin….” Caren alinionesha kitu nyuma yangu, palikua na kitu kilichonifanya nigeuke kwa haraka sana. Palikua Na shimo ambalo wakati tunaingia hatukuliona, istoshe hata wakati tunaweka vitu stoo hatukuliona.

Shimo hilo lilikua k**a njia ya kushuka chini, tulisogea na kuchungulia, palikua na ngazi za kuelekea chini. Nilimtazama Caren, macho yetu yaligongana, tulikua na maswali mengi sana yasiyo na majibu.

Mara tulisikia vishindo vya miguu ikipanda kutoka chini kuja juu, shimo lilikua na giza. Mimi na Caren tukajificha nyuma ya p**a huku macho yetu yakikodolea shimo lile Kuona ni Nani aliyekua akitokea humo, tulijawa na hofu kiasi kwamba tulikua tukitetemeka. Macho yetu yalikua eneo hilo tena kwa shahuku kubwa sana.

Kila hatua ilizidi kutupatia hamu ya kuona ni Nani aliyekua akitoka ndani ya shimo hilo, nilichokua nafikiria ni kumwona Mwanamke anayelia ambaye sauti yake niliisikia zaidi ya mara moja. Moyo wangu ulizidi kupiga kwa hofu na wasiwasi usio na ukomo, hali hiyo ilikua kwa Caren pia, yeye alikua akitetemeka kabisa.

Ghafla palikua kimya, hazikusikika tena zile hatua. Mimi na Caren tulitazamana kwa mshangao mkubwa sana, bado macho yetu yalikua yakitazama eneo lile lenye shimo. Mara tuliona Kichwa, kisha mwili, Mungu wangu alikua ni Baba yangu tena akiwa uchi wa Mnyama k**a alivyozaliwa, alifuatiwa na Mama yangu ambaye naye alikua k**a Baba yangu.

Mshangao mkubwa uliniingia, cha ajabu ambacho kilizidi kunishangaza ni namna walivyo, walikua Uchi lakini walikua wamefumba macho yao k**a watu wanaotembea wakiwa Usingizini. Hawakutazama popote kisha waliongoza kuondoka ndani ya chumba, halafu pale shimoni palijifunga.

Nilimziba mdomo Caren maana alikaribia kupiga kelele za hofu, nilimtaka akae kimya kisha nilimwambia tuwafuatilie wazazi wangu. Taratibu tulianza kiwafuata kwa nyuma, hatua kwa hatua hadi walipoingia chumbani na kufunga mlango

Walituacha na maswali mengi yaliyokosa majibu, tulirudi chumbani kwangu. Sikutaka kuamini hasa nilichokiona, Caren alinifuata niliposimama kisha aliniuliza

“Ina maana wazazi wako wanalijua hili jambo na wameamua kukaa kimya, au ni washirika?” aliniuliza swali lililozidi kunipa maumivu sana, chozi lilinidondoka nikifikiria Nilichokiona, nilitamani iwe ndoto niamke lakini lilikua tukio la kweli lililoniacha na maswali mengi sana kichwani, nilifikiria namna ambavyo Mama alinizuia nilipokua nafuatilia sauti ya Mwanamke anayeimba.

Uchungu ulikishika kifua changu, jasho lilinitoka huku chozi likinibubujika, sikujua nimpe jibu gani Caren, tulimpoteza Ziada katika mazingira ya kutatanisha. Nani ana majibu ya maswali yetu? Ni yule Mzee wa nyumba jirani, yule Bibi wa ajabu au Wazazi wangu?

“Celin, siwezi kubakia hapa naondoka. Nina hisia mbaya sana juu ya wazazi wako, tulicho kishuhudia hakikua kitu cha kawaida” alisema Caren. Nilimuelewa, hata k**a ningekua kwenye nafasi yake ningefanya hivyo hivyo lakini Mimi siwezi kuikimbia nyumba yetu. Niliishia kumtazama Caren akiwa anatokwa na machozi alichukua mkoba wake na kuishia zake, nilizisikia hatua zake akishusha ngazi.

Sikuweza kumzuia, moyoni mwake aliamini wazazi wangu walikua wachawi na hata mzizi wa kifo cha Zena ulitokana na Nyumba yetu, kuwaona wazazi wangu katika hali ile aliamini kua

kuna jambo walikua wanalijua na waliamua kulificha. Nilibakia nikiwa nimeketi kitandani nikiwa ninalia

Nilikua na usiku usiosahaulika Maishani mwangu, kila nilivyowafikiria wazazi wangu chozi lilikua likinibubujika bila kupumzika. Nilifuta chozi kila dakika hadi kulipopambazuka, asubuhi ilinikuta nikiwa nimeketi kwenye kochi chumbani kwangu.

Simu yangu ilikua ikiita sana, tena iliita mfululizo lakini sikutaka kujua nani anapiga wala sikua na mpango wa kuipokea, niliiacha iite hadi ilipokata yenyewe. Hisia za Usiku ziliendelea kunitesa, mara nilisikia mlango ukigongwa

Sikuitikia wito wa hodi hiyo, niliishia kuutazama mlango. Kisha ulisukumwa na kufunguka, nilikumbuka mlango sikuufunga. Mama yangu alikua amesimama mlangoni akinitazama, chozi lilianza kunilenga lakini sikutaka kuliruhusu lidondoke, Mama alisogea karibu nami, akaketi kitandani huku akionekana kunishangaa

“Hujaniona?” aliniuliza, nilimtazama Mama kisha nilimjibu

“Samahani Mama, kichwa changu hakipo sawa. Shikamoo” nilisema, sikutaka kumuuliza chochote kuhusu Usiku uliopita.

“Marahaba Celin, kimetokea nini?” Swali hili nusura chozi linidondoke, nilihisi Mama yangu alikua akiuliza jambo analolifahamu. Niliumia ndani yangu sababu ni Mama yangu Mzazi, nilipepesa kope za macho yangu k**a Mtu anayekaribia kulia

“Sio sawa Mama, nahisi nipo kwemye Dunia iliyojaa siri, isiyo na huruma kabisa. Sijui kwanini siambiwi ukweli Mimi” Kusema ule ukweli nilijikuta nikidondosha chozi langu, Zena alijaa mawazoni, Mama alinishika bega akaniuliza

“Kimetokea nini Celin, niambie Mimi ni Mama yako?” aliongea kwa kusisitiza huku sura yake ikionesha kutokua na hatia, alionesha kutofahamu chochote kile. Niliziweka nywele zangu vizuri maana zilivurugika kutokana na purukushani za Usiku, chozi liliendelea kunibubujika nikamtazama Mama huku nikiwa ninafuta chozi langu

“Unamkumbuka Zena?” nilimuuliza, alionekana kutafakari kidogo kisha akaniuliza “Yule rafiki yako?”

“Ndiyo!”

“Kimetokea nini?” aliniuliza kwa shahuku kubwa sana, sura ya Mama yangu haikua na hatia lakini nilijiuliza maswali mengi, nilijiuliza k**a kweli hafahamu chochote vipi kuhusu jana Usiku walipotoka kwenye lile shimo yeye na Baba, wana uhusiano gani na Mwanamke anayelia kwenye ile stoo?

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya TANO

NYUMBA JUU YA KABURISEHEMU YA TATUIlipoishia Nyumba Juu KaburiTulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wem...
27/09/2025

NYUMBA JUU YA KABURI
SEHEMU YA TATU

Ilipoishia Nyumba Juu Kaburi

Tulipishana Mwaka mmoja wa kuingia chuoni, alinitendea wema kila nyakati. Hata wakati ambao alipaswa kufurahi alinipa furaha yake na kisha yeye alibakiwa na huzuni yangu. Nilimwona akiwa anafunguliwa kutoka juu ya feni akiwa amevalia gauni lake jekundu.

Hakika maneno ya yule Bibi yalianza kutimia, nilimpoteza mmoja nimpendaye. Nilijiegemeza ukutani nikilia kwa kwikwi nikiushuhudia mwili wa Zena ukiondolewa na Askari Polisi waliokua hapo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa. Endelea

SEHEMU YA TATU

Mimi na Caren tulibakia chumbani kwa Zena tukilia, haikua rahisi kuamini kua Zena alikua amekufa kikatili sana kwa kujinyonga. Mara simu yangu ilianza kuita kutoka kwenye mkoba wangu niliokua nimeutupia pembeni, nilishtuka sana. Niliacha kulia nikauvuta mkoba kisha nikaitoa simu yangu ambayo bado ilikua ikiendelea kuita

Moyo ulinipiga ‘Paaa‼’ nilipoona ni Mama yangu ndiye aliyekua akinipigia. Sikutaka kusikia taarifa nyingine mbaya. Niliiacha simu iite hadi ilipo acha kuita, niliirudisha kwenye mkoba mara moja halafu fikra zangu zikawa nyumbani kwetu.

Maneno ya yule Bibi yalikua na nguvu ya kunizunguka kichwani, nilihisi nyumbani kwetu hapako salama. Niliumia ndani ya moyo wangu huku nikiitupa miguu yangu sakafuni.

Sikujua ni Nani alikua anafuata baada ya Zena, yule Bibi ni Nani na kwanini haya mauzauza yameanza baada ya kuhamia kwenye ile nyumba. Maswali haya yote nilijua ni Nani anapaswa kuyajibu. Ni yule Mzee wa nyumba jirani, huwenda anafahamu jambo fulani la kutisha kuhusu nyumba yetu.

Nilinyanyuka kutoka sakafuni, nikamtazama Caren aliyekua amelegea kutokana na kukosa nguvu kwa kile kilichotokea, tulimpoteza rafiki mzuri sana katika mazingira ya kutatanisha. Nilimwambia Caren

“Nataka kupata majibu ya haya yote Caren, siwezi kuruhusu hii hali iendelee” sauti yangu ilitoka kwa hisia kali ya maumivu, nilifuta chozi langu. Caren naye alisimama. Tulikua wawili tu ndani ya kile chumba cha Zena.

“Ukweli upi, ni kuhusu yule Bibi au kifo cha Zena?” aliniuliza, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha nilimwambia

“Vyote kwa pamoja, jina la Zena lilikua kwenye ile Barua uliyopewa na yule Bibi wa ajabu. Sijui, lakini nahisi kuna shida sehemu” Umakini wa Caren uliongezeka, akanitazama kwa shahuku akaniuliza

“Shida Sehemu?”

“Ndiyo, baada ya kuhamia kwenye ile nyumba nilianza kupata hisia ya ajabu. Sitaki kuwaambia Wazazi wangu kuhusu hilo lakini nahisi kuna Mtu anajua jambo kuhusu ile nyumba, Caren nisikilize Mimi” nilisema kisha nilimshika mabega Caren ili nimueleze zaidi. Nilimfanya Caren kua Mshirika wangu

“Kuna Mzee nyumba jirani nina wasiwasi anajua jambo, ile nyumba sio ya kawaida kabisa. Sitaki Wazazi wangu wajuwe sababu watachanganikiwa. Tunaweza kuutafuta ukweli?” nilimuuliza, alinitazama kwa tafakari fupi kisha aliniambia

“K**a hisia zako zinakwambia hivyo Celin, sina chaguo” nilimkumbatia Caren, angalau nilipata Mtu anayeweza kunielewa.

Nilirudi nyumbani jioni, hofu na mashaka viliendelea kunitafuna hadi nafika nyumbani. Niliogopa kukuta Watu wengi pale nyumbani, niliogopa kusikia sauti ya Kilio, niliogopa kupoteza Mtu mwingine. Nilipofika getini kwetu, nilisimama kidogo huku macho yangu yakielekea nyumbani kwa yule Mzee.

Palikua kimya, hapakua na dalili ya Mtu. Nilijiweka sawa kiakili ili Wazazi wangu wasigundue lolote, sikutaka wajuwe kuhusu kifo cha Zena wala jambo lolote lile lenye utata. Nilipoingia Bustanini niliitazama sana nyumba yetu, nafsi yangu iliniambia kuna jambo lisilo kawaida kuihusu hii nyumba lakini sikua na ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Nilipata amani nilipowakuta Wazazi wangu wakiwa wameketi sebleni wanaangalia taarifa ya Habari, angalau moyo wangu ulipata kupumzika.

Niliwasalimia kisha nilipandisha ngazi nikaelekea chumbani kwangu. Nilisimama kando ya dirisha nikiitazama nyumba ya yule Mzee, bado ilikua kimya. Palikua na majani mengi sakafuni kuashiria kua eneo hilo halikufanyiwa usafi kwa muda mrefu.

Baada ya kusimama kwa muda kidogo nilirudi na kuketi kitandani nikiwa nakumbuka matukio ya siku nzima, chozi lilinitoka tena. Kusema ukweli kifo cha Zena kiliniumiza sana, kuna namna nilijiona Mimi ni Mkosaji. Basi nilijiegesha kidogo, nikajikuta nikipitiwa na Usingizi.

Nilishtuka, bado palikua na giza. Mwili ulikua umechoka sana, hisia ya kua nililala muda mrefu ilinijia. Nilijinyoosha kidogo kabla ya kuchukua simu na kuangalia saa

Niliona ilikua ni saa 7:11 Usiku, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani kisha nikasogea pale dirishani na kuangalia nyumbani kwa yule Mzee. Bado palikua kimya, hapakua na dalili yoyote ile, Mbwa walikua wakibweka sana.

Nilifungua mlango taratibu kisha kwa mwendo wa kuchoka nilishusha ngazi, taa zilikua tayari zimezimwa kuashiria kua Wazazi wangu walikua wameshalala, swali pekee nililojiuliza

“Inawezekanaje Wazazi wangu walale bila kuniamsha?” Sikupata jibu la haraka, nilitembea taratibu baada ya kufika sebleni kisha niliwasha taa, kisha nililielekea friji nikachukua maji ya Baridi na kuyanywa. Angalau niliusikia mwili wangu ukiwa umepoa

Nilifikiria kuwagongea mlango wazazi wangu lakini niliona nitawasumbua, badala yake niliketi kwenye sofa. Bado taswira ya kifo cha Zena ilikua ikiendelea kunisak**a.

Nikiwa hapo nilianza kuhisi mwili wangu ukisisimka sana k**a vile nilikua napandwa na sisimizi, kichwa kilianza kua kizito huku nikianza kuisikia sauti fulani ya ajabu. Nilisikia sauti ya kugonga, ilisikika ikigongwa kwa utaratibu sana

“Mh‼ hii sauti inatokea wapi?” nilijiuliza, nilisimama taratibu huku sauti ya kochi ikisikika wakati nanyanyuka. Niliisikilizia vizuri ile sauti niligundua ilikua ikitokea kwenye chumba kimoja pale eneo la chini.

Chumba hicho tulihifadhia baadhi ya vitu ambavyo hatuvitumii mara kwa mara, mfano wa stoo hivi. Woga ulianza kunijia kisha nilianza kusikia sauti ya Mwanamke akiimba, sikujua alikua akiimba nyimbo gani lakini sauti ilikua ikitoka mule mule chumbani.

Ilikua ni sauti laini inayoimba kwa umaridadi sana, mapigo ya moyo wangu yaliongezeka sana, yalikua yakidunda k**a ngoma. Hata pumzi ziliongezeka, woga ulinishika sana, mwili uliendelea kusisimka kwa kasi huku nikihisi k**a nina hali ya kuchanganikiwa. Nilipiga hatua za taratibu sana kuelekea nilipoisikia sauti ile, korido ilikua tupu isipokua Mimi pekee.

Nilimeza funda zito la mate ili kujipa utulivu ambao kwa hali ilivyo ulihitajika sana, hatua zangu zilikua za kusuasua sana huku nikitembea k**a Mtu nsiye na uhakika wa kufika ninapohitaji. Nilizidi kutembea taratibu sana kuuelekea mlango, mara nilisikia sauti nyuma yangu

“Celin?” ilikua ni sauti ya Mama yangu aliyeonekana kusimama kwa sekunde kadhaa akinitazama kwa kunishangaa, uso wake haukuwa na hofu k**a wangu, jasho lilikua likinitoka. Kwa mara nyingine tena nilijiapiza kua siwezi kumweleza chochote kile Mama yangu.

“Mamaa‼” nilimwita kwa sauti ya msh*tuko kidogo, sikutegemea angekua akinitazama. Mkononi alikua ameshikilia glasi yenye maji ya Baridi. Taratibu alisogea akionesha kuwa alikua na maswali ya kuniuliza, aliponifikia aliniuliza

“Kuna nini mbona unaonekana k**a ni Mtu unayevizia Usiku huu?” swali la Mama lilinifanya nigundue kuwa alikua hajasikia chochote kile. Ile sauti haikusikika tena

“Hakuna Mama, sio kitu” nilisema kisha nilitaka kuondoka lakini Mama akanisimamisha

“Kuna jambo unanificha Celin, nakujua nje na ndani, wewe ni Binti yangu ukisema ukweli najua na ukisema uwongo vile vile najua. Nieleze, ulikua unavizia nini?” nilimshika Mama bega nikamwambia

“Mama usijali, hakuna jambo lolote lile. Nipo sawa” nilisema kisha nilipandisha ngazi nikarejea chumbani, nilijuwa nyuma yangu Mama alikua na maswali mengi ambayo sikutaka kuendelea kuyasikia. Nilipofika Chumbani, haraka nilichukua simu yangu na kumpigia Caren lakini hakuipokea

Niliitupa simu kitandani, kisha nilisogea dirishani. Niliitazama tena nyumba ya yule Mzee, niliamini alikua na majibu mengi ya maswali yangu, nilisimama kwa dakika k**a tatu hivi kisha

nilikata tamaa, nikataka kufunga dirisha lakini ghafla nilihisi k**a kuna Mtu amesimama dirishani kwenye nyumba ya yule Mzee akinitazama.

Nikishtuka sana, nyumba yake ilikua ya kawaida sio ya ghorofa. Dirisha moja lilikua likiwaka taa, hapo ndipo nilipomwona Mtu akinitazama. Ilionesha wazi kua alikua anajua kua nina tabia ya kuichunguza nyumba hiyo, nikajificha kidogo na kuanza kuchunguza kwa siri.

Nilishtuka sana, niliyemwona akinitazama alikua ni yule Bibi niliyepanda naye kwenye Treni, ndiye aliyenitamkia maneno ya ajabu na ndiye aliyempa Caren bahasha yenye karatasi yenye jina la Zena. Kwa namna yoyote ndiye anayehusika na kifo cha Zena, moyo ulilipuka mithiri ya Volkano nikiwa nimejibanza, niliipa mgongo nyumba ya yule Mzee

Mapigo ya moyo wangu yaliongezeka kasi, nilifumba macho ili kuvuta nguvu ya kirejea kumtazama tena, nilipopeleka tena macho yangu yule Bibi hakuwepo, isipokua ile taa iliyokua ikiwaka kwa mwanga mkali ilikua ikiangaza.

Japo nilikua mwoga sana Maishani mwangu lakini nilipata ujasiri wa kutaka kuelewa zaidi, nilipata wazo la kwenda kwenye ile nyumba. Usiku ulizidi kuwa mwingi, sikutaka Mtu yeyote yule ajuwe kuwa ninatoka. Nilichukua koti langu kisha nikalivaa, nilivuta pumzi nikiwa nimesimama tayari kwa ajili ya kuelekea nyumbani kwa yule Mzee.

Simu yangu ilinidokeza kua ilikua imeshapata saa Nane kasoro za Usiku. Nilijiambia kuwa liwalo na liwe lakini ni lazima niujuwe mzizi wa yote, nisingeliweza kukubali kupoteza wapendwa wangu, nilifungua mlango taratibu huku nikiisikia sauti ya Baba yangu akikoroma.

Sikua na shaka yoyote kua alikua amelala, hofu yangu ilikua kwa Mama yangu. Nilihakikisha nakua makini sana, nilizichunga hatua zangu za taratibu hadi nilipofika chini, kisha nilifungua mlango ambao ulinitii bila kupiga kelele zozote zile, nilipiga hatua za haraka baada ya kutoka nje hadi nilipoondoka ndani ya Uzio wa nyumba yetu.

Nyumba ya jirani, mbwa alikuwa akiendelea kubweka tena alibweka kwa kasi sana, sauti ya Bundi ilikua ikiendelea kusikika pia, ulikua ni Usiku mwingi kiasi kwamba hapakua na yeyote nje isipokua Mimi na shahuku yangu. Upepo wa hapa na pale ulikua ukiendelea kuvuma taratibu, ulifanya hali ya Ubaridi iongezeke.

Nilipofika nje kabisa, niliitazama nyumba yetu. Akili na nafsi yangu viliniambia haikua nyumba ya kawaida, basi nilishupaza shingo yangu kuelekea nyumbani kwa yule Mzee, nilikua na uhakika wa kupata Majibu ya maswali yangu usiku huu. Taratibu niliendelea kupiga hatua

Nilipofika mbele ya nyumba ya yule Mzee nilisimama kwanza huku nikijiuliza mara mbili mbili k**a nilikua tayari kufanya nilichokua nataka kukifanya. Nilijiambia ndani yangu kwa sauti isiyo na mawimbi ya nje

“Ni lazima niwe jasiri, vinginevyo naweza kupoteza kila nikipendacho” ilikua ni sauti iliyojaa ujasiri mwingi ndani yangu. Macho yangu yaliendelea kuitazama ile nyumba kisha nilisukuma

geti, halikua geti kubwa, geti dogo lililozungushiwa na uzio wa Miti fulani yenye miiba ndogo ndogo

Urefu wa geti iliishia kifuani pangu, nilipolisukuma nilipokelewa na sauti ya Bawaba za geti hilo ambazo zilipiga kelele fulani ya maumivu ya kufunguliwa mithiri ya nyumba isiyo kaliwa na yeyote yule. Sauti hii ilinipa maswali mengi, nilichukua simu na kuwasha tochi nione k**a hisia zangu zilikua sahihi.

Macho yangu yalishuhudia kile ambacho nafsi yangu iliniambia, geti lilizungukwa na kutu, Bawaba zilifichwa na kutu. Hapana shaka geti hili halikufunguliwa kwa muda mrefu, sasa nilijiuliza nikiwa nimesimama pale pale getini.

“Inawezekanaje? Ina maana walio ndani wanapitia wapi k**a geti hili halifunguliwi?” Lilikua swali la kwanza la Msingi, bado nilikua njia panda. Sikutaka kurudi nyuma, niliazimia ni lazima niichunguze nyumba pamoja na wanaoishi ndani ya hii nyumba.

Nilipiga hatua za kunyata, nikafanikiwa kufika mlango mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba hii. Nilipofika hapa niliwaza kidogo, jibu nililolipata ni kulielekea dirisha lile ambalo nilimwona yule Bibi wa ajabu, basi taratibu nilianza kutembea kwa mwendo wa kunyata hadi nilipolifikia dirisha.

Bado palikua panawaka taa, taratibu nilianza kuchungulia ndani, sikumwona yeyote yule lakini mazingira yote yaliniambia kua ndani ya nyumba palikua na Mtu au Watu k**a ambavyo nilimwona yule Bibi nikiwa chumbani kwangu.

Nilisimama hapo kwa dakika kadhaa, palikua kimya sana. Bado upepo wa taratibu ulikua ukiendelea, nilipata wazo la kuuelekea mlango hivyo nilirudi hadi mlangoni. Nilisimama kwa sekunde kadhaa, kisha nilijaribu kutekenya kitasa cha mlango

Cha ajabu, Mlango ulifunguka kirahisi sana. Baada ya kufungua mlango niliweza kuangaza kwa ndani ya nyumba hiyo, nilikutana na sebule inayowaka taa kali, palikua na Kochi moja jekundu lililo chakaa sana, niliona sahani juu ya meza, nilimuona paka akiwa ameketi kando ya meza.

Paka huyo alikua ametulizana sana, alikua akinitazama kwa macho yake makali ya kung’aa. Uwepo wa Paka ilikua ni ishara nyingine kua nyumba hii inakaliwa na Mtu, paka hawezi ishi mahali ambapo hakuna chakula. Nilishusha pumzi zangu huku moyo ukiendelea kunigonga sana.

Bado kichwa changu kiliendelea kugonga kwa maswali yasiyo na majibu ya Uhakika, wazo la kuingia ndani ya nyumba hiyo lilinijia, moyo haukuacha kudunda kwa nguvu, kijasho chembamba kilikua kinanitoka, nilipoanza kupiga hatua niliingiwa na Ubaridi, kwa nguvu sana nilivutwa nje na kuzibwa mdomo wangu kisha nikasogezwa pembeni, nikafichwa nyuma ya Ua moja.

Hata nilipojaribu kufurukuta sikuweza kisha nikaisikia sauti ya Caren

“Shii‼ ni Mimi” aliongea kwa sauti ya kunong’oneza. Aliniachia, hapo hapo kabla sijamuuliza alifikaje, sote tulimwona Yule Mzee akiwa ameshikilia tochi, alikua akichungulia pale mlangoni nilipotaka kuingilia, kwa namna nilivyomwona ni k**a alihisi uwepo wa Mtu. Alimulika tochi huku na kule lakini hakufanikiwa kutuona kisha aliufunga mlango wa Nyumba yake.

Hapo tuliachia pumzi ndefu maana tulikua tumezibana kuhofia asije akatushtukia.

Nini Kitaendelea? Usikose Sehemu Ya NNE

Address

Tanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SimuliziMax posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to SimuliziMax:

Share

GODSTAR ONLINE |GODSTAR MEDIA & COMPANY |GODSTAR_TZ |GODSTAR INC

Naitwa Godfrey Godstar ni muandishi na ni mtunzi wa hadithi lakini pia ni Graphics Designer na mfanya biashara unaweza wasiliana nami kupitia simu namba 0627200512, AHSANTE.