28/04/2025
AFYA TIPS:
JE! WAJUA MINYOO KUZIDI TUMBONI NDIO CHANZO CHA MATATIZO YAKO MENGI KIAFYA.
Na.
Stewart Meena
Hebu kwanza jiulize ni lini ilikuwa mara yako ya mwisho kunywa dawa za minyoo? Au kumpa mtoto wako dawa za minyoo?
Inawezekana kabisa sababu kuu ya changamoto hizo za kiafya unazozipitia zikawa zimesababishwa na MINYOO tu iliyoko ndani ya mwili wako.
Unapokuwa na minyoo mingi tumboni, ule mfumo wako wa mmengβenyo wa chakula unakuwa hautendi kazi sawa sawa ndio maana changamoto nyingi huwa zinajitokeza.
Mtu yeyote anapaswa kunywa dawa ya minyoo, , watu wazima, mama wajawazito-ikishauriwa na daktari pekee.
INATAKIWA KUNYWA DAWA HII KWA MUDA GANI!? π€
Miezi6 hadi mwaka1 kwa watu wazima na watoto na hii ni mahususi ikiwa unaishi kwenye mazingira hatarishi yanayosababishwa na maji machafu, kula nyama za kuchoma na ambazo hazijaiva vizuri, kula bila kunawa mikono kwa maji safi na sabuni au vitakasa mikono nk.
KIPI HUTOKEA K**A USIPOKUNYWA DAWA ZA MINYOO NA WADUDU WA TUMBO kwa muda mrefu!?
-uchovu kupita kiasi mara kwa mara
Kuumwa na tumbo mara kwa mara
Kupungukiwa damu (Anemia)
Ngozi kuparara, kutoka vipele (skin infections)
Kupungua uzito, tumbo kujaa gesi, meno kusuguana usiku.
Kuhara mara kwa mara na kwa watoto kudumaa, na kutokuimarika kiakili.
MAMBO YA KUEPUKA:
Safisha mikono kabla ya kula, usile matunda ambayo hayakuoshwa na maji safi ikiwemo na mbogamboga.
Punguza kutembea peku maeneo hatarishi yenye bakteria,
Usinywe maji machafu, usile nyama ambazo hazikuiva vizuri na samaki.
Mwisho usicheze muda mrefu na wanyama wafugwao k**a paka na mbwa( π π )
TIBA ZA MINYOO NA WADUDU WA TUMBO: (πͺ± π)
Kuna dawa za mitishamba na kuna dawa za mahosipitalini... "wataalamu wanazifahamu" waone kwa ushauri na matibabu.
Dawa zitolewazo hospitali kutibu minyoo ni pamoja na: , , (kwa tapeworms, flukes!)
Baadhi ya minyoo huweza kukuwa sentimita (centimetre) 30 hadi 180, au hata mita3 k**a ilivyo minyoo aina ya tegu nk. Ambao hawa hukuwa kuanzia mita3 hadi 6.
Source:
At WeCure Pharmacy, (Zambia)
π Call or WhatsApp Us on: +260779115205