UTUME FM RADIO 97.3MHz

UTUME FM RADIO 97.3MHz Utume Fm Radio, North Eastern Diocese- Evangelical Lutheran Church Tanzania. Box 10 Lushoto Tanga, E-mail [email protected] - Lushoto – Tumaini Hostel.

MOTTO OF THE RADIO
‘TUNAKUFIKIA ULIPO’ TUSIKILIZE LIVE KUPITIA http://onlineradiobox.com/tz/utume973/player/... TUAMBIE UNATUSIKILIZA KUTOKA WAPI

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amepiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi k...
27/11/2024

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amepiga kura kwa ajili ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa katika Kituo cha kupigia kura cha Uwalu kilichopo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga tarehe 27 Novemba, 2024.

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Zephania Sumaye amesema zoezi la upigaji kura katika Halmashauri ya Lushoto lina...
27/11/2024

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga Zephania Sumaye amesema zoezi la upigaji kura katika Halmashauri ya Lushoto linaendelea vizuri huku wananchi wakiendelea kusisitizwa kujitokeza katika vituo vya kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka.

Sumaye ameyasema hayo mapema leo mara baada ya kuzindua zoezi la upigaji kura katika kituo cha kupigia kura kilichopo katika Kitongoji cha Chakechake na kuongeza kuwa hali ya usalama ni shwari na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza hivyo kila mwananchi aliyejiandikisha ajitokeze akapige kura katika kituo alichojiandikisha.

Ameongeza kuwa k**ati ya ulinzi na usalama imejipanga vizuri kuimarisha ulinzi ambapo hata kubali kuona matukio yoyote yanayoashiria uvunjifu wa amani huku akiwataka wananchi wote mara baada ya kupiga kura kuondoka katika mazingira ya vituo vya kupigia kura.

Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashari ya Wilaya ya Lushoto Ikupa Harsoni Mwasioge amesema kuwa katika Kitongoji hicho cha Chake Chake vipo vituo vya kupigia kura vilivyoongezwa ili kupunguza umbali kwa wapiga kura ambapo katika kitongoji hicho kina jumla ya vitu 30 hivyo wananchi waendelee kujitokeza katika zoezi hilo.

Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza katika zoezi hilo wamesema kuwa zoezi la kupiga kura linaendelea vizuri licha ya kuwepo changamoto ndogo ya utafutaji wa majina lakini wanashukuru uwepo wa wasimamizi kuwasaidia katika kutafuta majina yao na kupiga kura

Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, amesema idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini ...
26/11/2024

Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, amesema idadi ya vifo vilivyotokana na kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo Jijini Dar es salaam imefikia 29 hadi kufikia leo November 26,2024 huku akisema lipo pia zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kwa kutumia teknolojia ya vinasaba(DNA) na wakishathibitisha watatoa taarifa.

Akiongea mchana huu Kariakoo, Makoba amesema "Mpaka kufikia muda huu ambao tunazungumza kwa bahati mbaya namba ya marehemu ambao tumethibitisha ni 29, kwahiyo namba imeongezeka kidogo tunaendelea kuwaombea wenzetu wapumzike kwa amani"

"Lipo zoezi linaloendelea la kutambua miili mingine kutumia teknolojia ya vinasaba (DNA) na wenyewe tutatoa taarifa tukishathibitisha Ndugu pamoja na miili ya wenzetu, kwa upande wa majeruhi idadi ipo palepale"

Siku moja kabla Watanzania hawajaenda kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, Halmashauri ya wilaya ya Lusho...
26/11/2024

Siku moja kabla Watanzania hawajaenda kupiga kura kuchagua viongozi wa serikali za mitaa, Halmashauri ya wilaya ya Lushoto imepewa kibali cha kuongeza vituo vya kupigia kura 64 kutoka 941 vya awali hadi 1005.
Hayo yameelezwa na Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Lushoto, Ikupa Mwasyoge leo Jumanne Novemba 26,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake, akisema ongezeko hilo ni kuwarahisishia wapiga kura hasa wenye changamoto za mahitaji maalumu kutekeleza zoezi hilo la kikatiba kwa urahisi na wakati.

Nao baadhi ya wananchi pamoja na wasimamizi wa vituo vya uchaguzi wamepongeza hatua ya kuongozwa vituo hivyo na kuwataka wananchi wenye sifa kujitokeza kuchagua viongozi wanaowataka

Jumla ya Vyama vinne vimeidhinishwa kusimamisha wagombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa katika Halmashauri ya wilaya ya Lushoto ambavyo ACT WAZALENDO, CUF, CCM na CHADEMA.
dc .safiel

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda leo Novemba 26, 2024 akiwa kwenye soko la Kilombero amezindua  kampeni  ya usafi ka...
26/11/2024

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Paul Makonda leo Novemba 26, 2024 akiwa kwenye soko la Kilombero amezindua kampeni ya usafi katika jiji la Arusha huku akisisitiza uwajibikaji kwa kila mwananchi kuhakikisha wanatunza mazingira kwani atakayek**atwa kwa kutupa taka faini shilingi milioni moja.

“Kwa hiyo nawaombeni msitupe taka ovyo hakikisheni taka inawekwa sehemu sahihi, usipotii sheria kwa mujibu wa sheria ya Jiji watakuk**ata utalipishwa milioni moja. Kwa nini tuingie kwenye ugomvi kwa jambo tunaloweza,” amesema Makonda.

Aidha Makonda amewakumbusha wananchi hao kwenda kupiga kura siku ya Jumatano Novemba 27, 2024 ili kuwapata viongozi wanaowataka, na baada ya kupiga kura warudi makwao kuendelea kutafuta pesa kwani mkoa wa Arusha ni mkoa wa kutafuta pesa

Askofu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mchungaji DKT. Msafiri Joseph Mbilu ...
23/10/2024

Askofu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mchungaji DKT. Msafiri Joseph Mbilu amewasihi wanawake kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika jamii na Kanisa kwaajili ya kujikwamua kiuchumi ili kuondokaa na umasikini.

Askofu Mbilu ameyasema hayo leo Oktoba 23, 2024 katika ufunguzi wa Kongamano kubwa la wanawake ukanda wa Afrika linalofanyika katika chuo cha KOTETI kilichopo Magamba wilayani Lushoto linalodhaminiwa na fungamano la kimisioni la United Evangelical Mission (UEM) lenye lengo la kuwajengea uwezo wanawake kujishughulisha katika kazi mbalimbali zitakazowafanya wajikwamue kiuchumi.

Aidha, Askofu Mbilu amesema njia moja wapo ya kupingana na umaskini ni kufanya kazi kwa bidii hivyo ni vyema kuwajengea wanawake uwezo wa kufanya kazi mbalimbali zitakazowasaidia kimaisha kwani ukimuwezesha mwanamke ni sawa na kuiwezesha jamii nzima.

Naye mwenyekiti wa kongamano hilo katika ukanda wa Afrika DKT. Mary Mbilu amesema kuwa baada ya kupata mafuzo hayo k**a washiriki watawashirikisha wanawake wengine katika ngazi ya kanisa na jamii ili kila mwanamke awe na uwezo na ujuzi wa kupata fursa zitakazomsaidia kimaisha.

Nao baadhi ya wanawake waliohudhuria Kongamano hilo wameushukuru uongozi wa UEM kwa kuandaa Kongamano hilo litakalowajengea uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali zitakazowafanya kutokuwa tegemezi katika familia.

Viongozi wa Dini mbalimbali kupitia k**ati ya Amani wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wamekutana hii leo Octoba 15, 2024 il...
15/10/2024

Viongozi wa Dini mbalimbali kupitia k**ati ya Amani wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wamekutana hii leo Octoba 15, 2024 ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu amani katika jamii hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika Novemba 27, 2024 na kuhamasisha jamii kushiriki Uchaguzi huo.

Mgeni rasmi katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Sumaye ameipongeza k**ati hiyo kwa kusadifu madhumuni ya uwepo wake na kuwaeleza kuwa ipo haja ya kukaa pamoja ili kuona namna bora ya kutekeleza mipango mikakati iliyonayo ikiwemo suala la kupambana na ushoga.

Awali mwenyekiti wa Kamati ya Amani Wilaya ya Lushoto ambae pia Msaidizi wa Askofu KKKT-DKMs Mch. Michael Kanju amesema kuwa uwezeshwaji katika masuala ya kifedha ili kuweza kuzifikia jamii za maeneo ya ndani zaidi na kukosa ofisi imekuwa ni changamoto kubwa inayoikabili k**ati hiyo katika kufikia malengo yake.

Nae Katibu wa Kamati hiyo ambae pia ni katibu wa BAKWATA wilaya ya Lushoto, Mohamed Said Baruti ameiomba serikali kusaidia mchakato wa kushusha majukumu ya k**ati hiyo hadi kufikia ngazi ya tarafa na kata ili iweze kufahamika hatua itakayo ondoa mtazamo hasi kwa baadhi ya watu kuhusu k**ati hiyo.

Ili kukabiliana na changamoto ya kukosa ofisi Mkuu wa wilaya alimuomba Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Lushoto Ali Daffa kuona uwezekano wa kulitafutia ufumbuzi ambapo aliahidi kufanyia kazi kwa kushirikiana na ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Lushoto na kuhusu kuishusha k**ati ngazi ya chini Dc Sumaye ameahidi kulitekeleza baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa kukamilika.

Mlezi wa Kamati ya Amani wilaya ya Lushoto Askofu wa Kanisa la kiinjili la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKT-DKMs) Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambae aliwasihi viongozi hao kuendelea kushik**ana ili kuwaletea wananchi amani ya kweli itakayo saidia kusukuma ajenda ya maendeleo kwa taifa na wananchi wake hususani kipindi hiki cha uchaguzi.

Kamati ya Amani wilaya ya Lushoto inaundwa na viongozi wa dini mbalimbali ambapo kwa pamoja wanashirikiana kuhakikisha kunakuwepo na haki, upendo, amani na umoja kwa dini zote Tanzania na wananchi wake.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu,amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanz...
14/10/2024

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu,amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha Watanzania kuendelea kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapigakura huku akiwataka Watanzania wote kutumia muda uliobaki kuendelea kujitokeza katika Vituo mbalimbali vya kujiandikisha kwa kuwa ni wajibu kushiriki katika kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi.

Askofu Dkt Mbilu ametoa witu huo leo tarehe 14/10/2024 mara baada ya kujiandikisha kwenye daftari la Wapigakura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kituo cha kujiandikisha cha Uwalu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga na kuwasihi Watanzania wote kuendelea kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili kutimiza haki yao ya kimsingi ya kikatiba ya yakupiga kura wakati utakapofika.

Sambamba na hayo ikiwa leo pia ni kumbukizi ya miaka 25 ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Askofu Dkt.Mbilu ameongeza kwa kusema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi ni vema viongozi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kujitenga na vitendo vya rushwa kwani kwakufanya hivyo watakuwa wamemuenzi Baba wa Taifa ambaye alikimea waziwazi vitendo vya rushwa kwani mtu anayetumia rushwa kupata uongozi huyo hafai kwa sababu anafanya hivyo kwa manufaa binafsi badala ya wananchi wanaompa kura.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Zephania Steven Sumaye amesema kuwa uelewa kwa wanachi juu ya kujiandikisha iliwapate sifa ya kupiga kura wakati utakapofika umeendelea kuwa mkubwa Wilayani Lushoto huku akiwataka wananchi kuendelea kujitokeza huku akiwashukuru viongozi wa Dini ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha waumini na wananchi.

Mkuu huyo wa Wilaya kipekee amemshukuru Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluthuri Tanzania Dayosisi ya Kaskazi Mashariki Dkt.Msafiri Joseph Mbilu, kujitokeza kujiandisha na kuwahimiza watanzania katika zoezi zima la kujiandikisha.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu, amewapongeza Washarika wa Usharika Mombo kwa n...
12/10/2024

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dkt Msafiri Joseph Mbilu, amewapongeza Washarika wa Usharika Mombo kwa namna wanavyoendelea kujitoa katika kumtumikia Mungu katika kuchangia ulipaji wa deni la Dayosisi pamoja na ujenzi wa Kanisa jipya na la kisasa linaloendelea kujengwa katika Usharika huo.

Ameyasema hayo wakati akitoa salamu zake katika Ibada ya Kipaimara iliyofanyika tarehe 12/10/2024 katika Jimbo la Tambarale Usharika wa Mombo na kuongeza kuwa amefarijika kuona Washarika wa Usharika wa Mombo wanavyojitoa katika kuchangia ulipaji wa deni la Dayosisi na anaamini kwa namna ambavyo kila mmoja anajitoa siku moja deni hilo litakwisha huku akiwasihi kila mmoja kuendelee kujitoa kwa moyo.

Amewasihi Washarika hao kuendelea kujitoa ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo kwani kwa kufanya hivyo watabarikiwa na Mungu.Pia Askofu Dkt Mbilu ameunga mkono ujenzi wa Kanisa hilo kwa kutoa kiasi cha Tsh 200,000/=

Wakati akihubiri katika Ibada hiyo, Askofu Dkt Mbilu amewataka waumini kuendelea kuweka Imani yao kwa Mungu huku wakiendelea kumtegemea Mungu katika maisha yao kwani kwa kufanya hivyo hiyo ndiyo Imani ya kweli na wasikubali kuyumbishwa na mafundisho potofu ambayo yameibuka kwa wingi katika nyakati hizi.

Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Mbilu amewataka Washarika kuendelea kuliombea Taifa la Tanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa linapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku akiwataka Washarika hao kujitokeza katika kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura,Wenye sifa za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wafanye hivyo na siku ya kupiga kura watu wajitokeze kwa wingi ili wakachague viongozi wazuri.

Nao Vijana waliobarikiwa katika Ibada hiyo wakitoa itikio baada ya kubarikiwa kupitia Risala yao wamemshukuru Askofu Dkt. Mbilu pamoja na wote waliohusika kuwafundisha neno la Mungu kwa usahihi huku wakiahidi kuishika imani ya Kristo bila kuyumbishwa na mafundisho yoyote potofu pamoja na kuyafanyia kazi yote waliojifunza kwa kipindi cha miaka miwili.

Jumla ya Vijana 92 walibarikiwa katika Ibada hiyo huku wawili kati yao wakibatizwa. Vijana hao walitoa kiasi cha Tsh 450,000/= kwaajili ya kuunga mkono juhudi za kulipa

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mheshimiwa  Zephania Sumaye leo Oktoba 11, 2024 amezindua zoezi la Kujiandikisha kwenye Daftar...
11/10/2024

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mheshimiwa Zephania Sumaye leo Oktoba 11, 2024 amezindua zoezi la Kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura litakalofanyika kwa muda wa siku 10 hadi Oktoba 20,2024 na kutumia fursa hiyo kujiandikisha katika kituo cha Chakechake kilichopo Kata na tarafa ya Lushoto wilayani hapo.

Mhe. Sumaye ametumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kutumia haki yao ya msingi kwa kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha katika zoezi hili muhimu na kuwatoa hofu juu ya uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu wenye nia ovu kuwa zoezi la kujiandikisha litasababisha kura kuibiwa.

Dc Sumaye ametoa wito pia kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa na kuombea mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuwahimiza waumini wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba 27, 2024 .

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Lushoto Mh.Shabani Shekilindi amewapongeza wakazi wa kata ya Lushoto kwa kujitokeza kwa wingi katika siku ya kwanza ya kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura hatua itakayowawezesha kupate nafasi ya kuchagua viongozi wazalendo watakao tumikia taifa kwa uadilifu.

Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza mapema leo katika kituo cha kujiandikisha cha Chakechake akiwemo Yohana Msigiti na Pehasisi Ikuni wamesema kwa kutambua kuwa ni haki yao ya kikatiba wamejitokeza kujiandikisha ili waweze kushiriki katika uchaguzi huku wakimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Lushoto kwa kuwaongoza katika zoezi hilo muhimu.

Kauli mbiu ya uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka 2024 inasema" Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi".

Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 15 Kujeruhiwa baada ya basi Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea J...
03/10/2024

Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 15 Kujeruhiwa baada ya basi Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha kupata ajali ya kuacha njia na Kupinduka katika eneo la Maili kumi, barabara ya Segera-Korogwe mkoani Tanga

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea Octoba 3, 2024 majira ya saa 7 na nusu usiku, ambapo basi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Julias Mushi (43) mkazi wa Arusha.

Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa madereva kufuata Sheria za barabarani nyakati zote kwa kuchukua tahadhari na kuheshimu sheria za usalama Barabarani kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho wa Safari

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Mch. Dkt. Msafiri Joseph ...
28/09/2024

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameiomba Serikali kuongeza jitihada katika uchunguzi wanaoufanya ili kuwabaini mapema na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote wa vitendo vya utekaji na mauwaji ya watu hapa nchini.

Askofu Dkt. Mbilu ametoa wito huo leo 28-9-2024 wakati akitoa salamu kwa waumini wa KKKT-DKMs katika ibada ya Kustaafu kwa heshima Mchungaji Ezekiel Andrea Mwarabu iliyofanyika katika Usharika wa Hale Jimbo la Tambarare na kukazia kuwa hakuna mtu mwenye haki ya kutenda ukatili kwa mwingine ikiwemo mauwaji.

Amesema kwa msaada wa Mungu na maombi Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itafanikiwa kuwabaini na kuwak**ata wale wote waliohusika katika matukio hayo.

Katika hatua nyingine amewakumbusha watumishi wa KKKT-DKMs kuendelea kutumika kwa uaminifu na kutenda haki katika wajibu wao k**a walivyoapa wakati wa kuingizwa kazini jambo litakalowaongoza kuwa na mwisho mwema na kustaafu kwa heshima k**a ilivyokuwa kwa Mch.Mstaafu Ezekiel Mwarabu aliyetumikia Kanisa kwa miaka 29 na wachungaji wengine walio kutangulia.

Amesema pamoja na kutumika madhabauni lakini pia watumishi katika Kanisa wanapaswa kujishughulisha na shughuli nyingine halali za kiuchumi zitakazo saidia boresha hali zao za maosha bila kuharibu wito mkuu wa kumtumikia Mungu.

Ibada hii ya Kustaafu kwa Mchungaji Ezekiel Andrea Mwarabu pia ilihudhuriwa na Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Mlondakweli Kanju, Katibu Mkuu wa KKKT-DKMs Mwl. Julius Madiga, Wakuu wa Majimbo, Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi na Washarika wawakilishi kutoka Majimbo matano yanayounda Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Address

Lushoto
Tanga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when UTUME FM RADIO 97.3MHz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to UTUME FM RADIO 97.3MHz:

Share