13/01/2023
Ni k**a vile kifo kilikuwa kikimuita Gunze Luhangija, Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) aliyejinyonga, kwani si mara ya kwanza kujaribu kujiua kwa kunywa sumu lakini amekuwa akiokolewa.
Inaelezwa Gunze alikuwa akirusha makombola yake kwa Mwanamke huyo pichani, akimuomba wawe wapenzi lakini haikuwa rahisi kukubaliwa na mrembo huyo kutokana na sababu zake binafsi, na ilipofika siku ya tarehe 26/12/2022, yaani siku ya Boxing Day, Gunze alimzawadia Mwanamke huyo iPhone 14 yenye thamani ya milioni tatu na ushee....k**a zawaidi ikiwa imeambatana na ombi la kumtaka amkubalie wawe wapenzi lakini baadae Mwanamke huyo alimkataa, ndipo Gunze akaamua kuchukua maamuzi magumu ya kujiua.
Baadhi ya marafiki zake wamefunguka haya
"Huyu kijana hapa chuo katusononesha sana wana Mwanza, siku ya Boxing Day alimnunulia Demu (Mpenzi) wake iPhone 14 (simu) na baada ya siku chache demu akamkataa kwamba kapata mtu mwingine.....dogo akaamua kujitundika"- walieleza Marafiki zake.
RIP
Follow ukurasa Wetu wa Instagram 👇
https://www.instagram.com/mudumohtz