12/06/2026
MATANGAZO YA MUBASHARA YAGEUKA KUWA MOJA TUKIO LA KUCHEKESHA KATIKA UPDATE ZA KOMBE LA DUNIA.
Mwandishi mmoja wa habari kutoka Korea Kusini π°π· alikuwa mubashara kwenye televisheni ya MBC, akiwa makini kabisa na majukumu yake... lakini ghafla shabiki mmoja wa Mexico alitokea pembeni yake na kubadilisha kila kitu.
Shabiki huyo alimshika mkono kwa furaha kubwa, huku mwandishi akionekana kutokuwa na raha lakini akijitahidi kubaki kawaida mbele ya kamera.
Akiwa anaendelea na matangazo hayo ya Mubashara huku akionekana kwamba angeweza kumaliza matangazo yake bila tatizo licha ya uwepo wa shabiki huyo pembeni yake.
Ghafla yule shabiki alimgeukia na kumbusu shavuni akiwa bado anaendelea na matangazo hayo ya mubashara hewani!π
Ndiyo... ni wazi kabisa kwamba hakutarajia jambo hilo kutokea hivyo ilimbidi atabasamu..