MaraMoja News

MaraMoja News KWA HABARI NA MATUKIO YA PAPO KWA APO UTAYAPATA HAPA UKWELI BILA KUPINDISHA
©COPYRIGHT MaraMoja Company Ltd

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya Askari Polisi aitwaye Roland Mollel amba...
16/04/2026

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu sita kwa tuhuma za mauaji ya Askari Polisi aitwaye Roland Mollel ambaye ni mkazi wa Arusha yaliyotokea Aprili 15, 2026 muda wa usiku.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa tukio hilo lilitokea huko katika mtaa wa Mlimani, kata ya Muriet Jijini Arusha.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa Askari huyo wakati akiendelea na shughuli zake binafsi baada ya kazi, kulitokea taharuki iliyotokana na kusambaa maneno ya kundi la
watu wakidai katika eneo lao kuna wezi wameonekana.

Ameendelea kufafanua kuwa wakati hayo
yakiendelea, marehemu akiwa anapita na mtu mwingine ambaye inadaiwa ni dereva
bodaboda wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki, kundi hilo lilianza
kuwashambulia huku wakiwakimbiza.

Aidha, amebainisha kuwa wanaendelea na msako wa kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao wamehusika na pia wanakamilusha uchunguzi wa tukio hilo.

Jeshi la Polisi mkoani humo limetoa wito kwa baadhi ya wananchi wanaoendekeza tabia za kuchukua sheria mkononi kwa kuongozwa na mihemko kuacha kwani watambue wakifanya hivyo ni kuvunja sheria pamoja na kusababisha madhara kwa watu ambao hawana hatia.

16/04/2026

 : Baada ya kukaribishwa kwa vifijo na nderemo na maelfu ya waumini waliojitokeza katika Mji Mkuu Yaounde, Papa Leo amew...
16/04/2026

: Baada ya kukaribishwa kwa vifijo na nderemo na maelfu ya waumini waliojitokeza katika Mji Mkuu Yaounde, Papa Leo amewahutubia viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa muda mrefu wa Cameroon Paul Biya akiwataka viongozi wa nchi hiyo kuzisuta nafsi zao, kuvunja minyororo ya ufisadi na kuheshimu haki za binadamu.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo ametoa wito kwa Serikali ya Cameroon kupambana dhidi ya ufisadi.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema viongozi wanapaswa kuwa madaraja na sio chanzo cha migawanyiko.

MaraMoja News

 : Mahakama ya Ikolo Wilaya ya Kyela imewahukumu Evance Mwakajumba (36) na Gwakisa Mwakajumba (17) wote wakazi wa Ngonga...
16/04/2026

: Mahakama ya Ikolo Wilaya ya Kyela imewahukumu Evance Mwakajumba (36) na Gwakisa Mwakajumba (17) wote wakazi wa Ngonga Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya kifungo cha miezi (5) jela kwa kosa la shambulio la kudhuru mwili walilolifanya kwa Godbless Mwandemelela baada ya kuzusha kwamba watuhumiwa wameguswa na mhanga kisha nyeti zao kupotea hivyo kujichukulia sheria mkononi kwa kumshambulia mlalamikaji huyo.

Hukumu hiyo imetolewa na Mhe.Hakim Kazungu RM Aprili 14, 2026 katika Mahakama ya Mwanzo Ikolo. Imeelezwa kuwa Wash*takiwa walitenda makosa hayo Aprili 6, 2026 baada ya kumtuhumu mlalamikaji kuwa anajihusisha na vitendo vya kishirikina kwa kugusa watu na kupoteza nyeti zao.

Wash*takiwa wametiwa hatiani kwa mujibu wa kifungu cha 241 cha sheria ya kanuni za adhabu sura ya 16 marejeo ya 2023.

  Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama cha@actwazalendo_official  Janeth Rithe, anaendelea kufanyiwa mahojiano usiku...
20/06/2025

Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama cha@actwazalendo_official Janeth Rithe, anaendelea kufanyiwa mahojiano usiku huu katika kituo cha polisi cha Central Dar es Salaam, baada ya kujisalimisha mapema hii leo Juni 20, 2025.

Imeelezwa kuwa, awali maafisa wa polisi walifika zilipo ofisi za chama hicho Magomeni Dar es Salaam, lakini hawakumkuta na kuacha ujumbe, ambapo baadaye alitii wito huo na kujisalimisha mwenyewe.

OJANTO VINTAGE ENTERPRISEHuduma Zetu za Kipekee Zinazokidhi Mahitaji Yako.Ojanto Vintage Enterprise inajivunia kutoa hud...
03/10/2024

OJANTO VINTAGE ENTERPRISE

Huduma Zetu za Kipekee Zinazokidhi Mahitaji Yako.

Ojanto Vintage Enterprise inajivunia kutoa huduma bora na za kuaminika katika maeneo yafuatayo:

Usafi wa Majumbani na Ofisini: Tunahakikisha maeneo yako yanakuwa safi na yenye mazingira bora ya kuishi au kufanya kazi.

Usafirishaji wa Mizigo: Huduma salama na ya haraka kwa usafirishaji wa mizigo, popote unapohitaji.

Kukodisha Magari: Tunatoa magari ya aina mbalimbali kwa mahitaji yako, iwe ya muda mfupi au mrefu.

Madereva kwa Kukodisha: Tunakupatia madereva wenye ujuzi kwa mahitaji yako ya usafiri binafsi au biashara.

Mahali tunapopatikana: Tabata Aroma, Opposite Maghorofa ya NSSF.

Wasiliana nasi leo:

Simu: +255 617 154 183

Barua pepe: [email protected]

Ojanto Vintage Enterprise – Huduma za Kuaminika Kwa Kila Mtu!

🔴AJALI▪️Watu 5 Wafariki,2O Wajeruhiwa Katika Ajali MorogoroWatu watano wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari...
05/06/2023

🔴AJALI

▪️Watu 5 Wafariki,2O Wajeruhiwa Katika Ajali Morogoro

Watu watano wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa baada ya gari walilokua wakisafiria Toyota Coaster yenye namba za usajili T .938 DVQ Lilikua linatokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam kugongana na lori la mzigo lenye namba za usajili T. 693 DMF katika eneo la Iyovi Wilaya ya Kilosa barabara kuu ya Morogoro – Iringa .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Coaster ambaye jila lake halijafahamika kwa kutaka kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari .

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya St Kizito Mikumi dokta Steven Mbilinyi amekili kupokea kwa miili ya watu watano waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

“Tumepokea miili ya watu watano, wanaume watatu na wanawake wawili na majeruhi 20 kati yao 10 wametibiwa na tumewaruhusu na 9 wanaendelea kupatiwa matibabu na mmoja amepelekwa hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro kwa matibabu zaidi.” amsema Mganga Mfawidhi.

  Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki, ...
12/05/2023

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, amefariki dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki, Dar es Salaam.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa alipata changamoto ya kifua na kupelekwa alfajiri ya leo Hospitalini hapo na baadaye kufariki.

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Philip Mpango akimpokea Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris alipowasili katika Uwan...
29/03/2023

Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Philip Mpango akimpokea Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Machi 2023 kuanza ziara nchini Tanzania

(Picha Ofisi ya Makamu wa Rais)

  Mchezo umesimama kwa muda katika dimba la Mkapa, kutokana na tatizo la taa za uwanja kupungua nguvu.Mpaka sasa:Tanzani...
28/03/2023

Mchezo umesimama kwa muda katika dimba la Mkapa, kutokana na tatizo la taa za uwanja kupungua nguvu.

Mpaka sasa:

Tanzania 0-0 Uganda

Address

Tukuyu

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MaraMoja News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MaraMoja News:

Share