JayMero

JayMero Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from JayMero, Digital creator, Ubungo.

08/06/2026

Siku sita kabla ya Kombe la Dunia kuanza mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa N'Golo Kanté ambaye ana asili ya Ufaransa alifika mahak**ani kuomba talaka huku akitaka mali zigawanywe kwa usawa wa asilimia 50 kwa 50.
Kwa mujibu wa simulizi hiyo mwanamke huyo ana watoto watatu ambao si wa Kanté na aliamini kuwa sheria za talaka nchini Ufaransa zingempa haki ya kupata nusu ya mali zilizopatikana wakati wa ndoa.
Hata hivyo baada ya uchunguzi wa kina kufanyika ilidaiwa kuwa Kanté hakuwa na mali zilizosajiliwa chini ya jina lake binafsi. Taarifa hizo zinaeleza kuwa sehemu kubwa ya utajiri wake ilikuwa imeandikishwa kwa watoto wake pamoja na ndugu wa karibu kutoka Mali ambako familia yake inatoka.

07/06/2026

𝗪𝗮𝘁𝘂 𝘀𝗶𝗼 𝘄𝗲𝗺𝗮 𝗸𝗮𝗯𝗶𝘀𝗮😂😂

Mbinu za Diamond Formation (pia huitwa rhombus au diamond/wedge katika baadhi ya muktadha) ni mpangilio wa ulinzi unaotu...
07/06/2026

Mbinu za Diamond Formation (pia huitwa rhombus au diamond/wedge katika baadhi ya muktadha) ni mpangilio wa ulinzi unaotumika sana katika ulinzi wa karibu wa VIP (bodyguard), polisi na mbinu za kijeshi za vitengo vidogo. Mpangilio huu huwaweka walinzi kuzunguka mtu mkuu (principal) ili kutoa ulinzi wa digrii 360 huku wakiruhusu harakati.
Dhana kuu katika ulinzi wa karibu wa VIP
Katika ulinzi wa watendaji au viongozi diamond formation huwaweka mawakala wa usalama katika sehemu nne kuu za almasi (au rhombus) inayozunguka mtu anayelindwa:
• Principal (Mtu Mkuu): Mara nyingi huwekwa karibu na katikati au kidogo mbele, mara nyingi akiwa na “body man” au bodyguard wa karibu.
• Point/Lead (Mbele): Mlinzi aliye mbele huangalia vitisho, kusafisha njia, na kuwa mwangalizi wa mbele.
• Left Flank na Right Flank (Upande wa Kushoto na Kulia): Walinzi wa pembeni hufunika vitisho vya kando na kudumisha umbali.
• Rear Security (Ulinzi wa Nyuma): Mlinzi wa nyuma hufunika sehemu ya nyuma na vitisho vinavyoweza kutokea nyuma.
Timu kubwa (k.m. watu 6–8+) huongeza tabaka za ziada k**a ulinzi wa nje au almasi ya pili.
Mpangilio huu ni dynamic walinzi hubadilisha umbali kulingana na eneo wingi wa watu kiwango cha tishio na kasi ya kutembea. Unaweza kuwa “tight” (karibu sana katika maeneo hatari) au “loose” (umeenea zaidi katika maeneo wazi).
Faida Muhimu
• Ulinzi wa pande zote (360°): Tofauti na mstari au safu moja hulinda dhidi ya vitisho kutoka kila upande.
• Kubadilika na uwezo wa kusonga: Rahisi kubadilisha kuwa miundo mingi wedge au V) au kujibu tukio haraka.
• Ufahamu wa hali: Kila mlinzi ana sekta maalum ya kuwajibika (mbele, pande, nyuma), hivyo kupunguza sehemu zisizoonekana.
• Mwitikio wa haraka: Inasaidia kuondoa mtu mkuu au kujibu shambulio huku akimlinda.
• Kinga ya kisaikolojia: Inionekana kuwa na mpangilio na kitaalamu, hivyo inaweza kuwakatisha tamaa washambuliaji.
Jinsi Inavyofanya Kazi
1. Kusonga: Timu husonga pamoja na mtu mkuu, wakidumisha mawasiliano na kuonana.
2. Sekta za Uwajibikaji: Kila nafasi inachunguza eneo lake kila wakati.

06/06/2026

Vip kwako ulishachangia damu ili upewe biskuti..😂😂

Zifahamu aina Mbalimbali ambazo zinatumika duniani kutengeneza kipato ambazo unapaswa kuzielewa kwa kina jinsi zinavyo f...
06/06/2026

Zifahamu aina Mbalimbali ambazo zinatumika duniani kutengeneza kipato ambazo unapaswa kuzielewa kwa kina jinsi zinavyo fanya kazi Kisha kuchagua Vipaumbele vyako kati ya aina hizi zitakazo Kuwa bora kutumika k**a njia ya kukufikisha katika kilele chako cha mafanikio.

Ni muhimu uweke malengo yako mapema ya vipato utakavyo Kuwa navyo maishani mwako.
Ili uanze mapema kujijengea uzoefu ujuzi pamoja na Maamuzi ya Kuanza. Aina hizo ni k**a ifuatavyo.
a, Earned income (Kipato kazi)
b, Profit income (kipato faida)
c, Interst income (kipato Kodi)
d, Divided income (Kipato gawio)
e, Rental income (Kipato Kodi)
f, Capital gains income (Kipato ongezeko la Thamani)
g, Royalty income (Kipato kutokana na ujuzi, ubunifu, uwezo, kipaji)

Hebu Sasa tuanze kuangalia aina Moja baada ya nyingine Kwa undani Zaidi.

A. EARNED INCOME (Kipato Kazi)
Hii ni aina ya Kipato Maarufu Sana Kwa wàtu wengi katika aina hii unatengeneza Fedha Kwa kuwekeza muda wako katika Kufanya Kazi mahali Fulani hasa Ajira au kibarua. Ili uweze kupata mshahara au ujira.

Na hii ni njia iliyo zoeleka na kutumiwa na wàtu wengi sana, ni aina nzuri ya kutengeneza Kipato hata Kwa mhusika atakaye tumia sehemu ya Kipato hiki kujenga vyanzo vingine vya mapato, Kitu ambacho ni kigumu sana Kwa wàtu walio wengi, wanakwama na kupelekea miaka mingi Kuwa palepale walipo.
Ni kwasababu wamekuwa wakitegemea njia hii k**a ndio chanzo pekee cha Kufikia malengo yao ya kifedha.
Kitu ambacho sio cha kweli na hatari sana kwani mara Nyingi pesa huwa kidogo makato yake makubwa pia mara chache sana mshahara kuongezeka ni watu wachache sana wanaofanikiwa kifedha Kwa Kutumia njia hii pekee k**a chanzo cha mapato.

B: PROFIT INCOME (Kipato Faida)
Hii ni aina ya Kipato ambayo unatumia pesa kuuza bidhaa au kutoa huduma Kwa pesa zaidi ya gharama za udhalishaji unaweza kuwa Katika uuzaji wa jumla rejareja usambazaji ama kuwa mzalishaji mwenyewe.

Hapa ninazungumzia kujishughulisha na biashara ya Kutoa huduma au bidhaa Fulani Katika soko lengo Kubwa likiwa ni kupata Faida.

Itaendelea➡➡➡➡

06/06/2026

Watu mnapenda kujiamulia mambo

06/06/2026

Ila dah😂

06/06/2026

Ishu ni deeep 😃

Hakuzaliwa kwenye maisha ya kifahari..Akiwa mtoto alikulia katika familia yenye changamoto nyingi na hali duni ya kimais...
06/06/2026

Hakuzaliwa kwenye maisha ya kifahari..
Akiwa mtoto alikulia katika familia yenye changamoto nyingi na hali duni ya kimaisha😰

Wakati mwingine alilazimika kupambana na hali ngumu sana na kuwafanya watu wengi waone kuwa ndoto zake za kuwa mchezaji mkubwa wa soka hazitatimia.

Badala ya kukata tamaa aliamua kufanya mazoezi kwa bidii kubwa kuliko wenzake,kila siku aliamka mapema sana.

Na kufanya mazoezi binafsi kabla ya muda wa kufanya mazoezi na wenzake kwa pamoja.

Alijitoa sana kwa moyo wake wote kwenye mchezo wa soka,akavumilia maumivu,lawama na changamoto nyingi
Huyu si mwingine ni Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro.

Leo hii ni miongoni mwa wachezaji walioandika historia kubwa zaidi katika mchezo wa soka duniani.

Good morning

Address

Ubungo

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JayMero posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share