Mbabu Yanga news & Apdate

  • Home
  • Mbabu Yanga news & Apdate

Mbabu Yanga news & Apdate Yanga daima mbele nyuma mwiko Like and comment my page

02/11/2024
2024/25   Group Stage Draw: ☑️
07/10/2024

2024/25 Group Stage Draw: ☑️

With Jonas mkude – I just got recognized as one of their top fans! 🎉
12/06/2024

With Jonas mkude – I just got recognized as one of their top fans! 🎉

KUNA mechi unatamani uendelee kuangalia siku kutwa. Yaani hata wacheze wiki nzima bado hautoichoka. Haijalishi unashabik...
02/06/2024

KUNA mechi unatamani uendelee kuangalia siku kutwa. Yaani hata wacheze wiki nzima bado hautoichoka. Haijalishi unashabikia mojawapo ya timu zinazocheza au la. Mechi bora ya Msimu imepatikana siku ya mwisho ya Msimu. Azam FC vs Yanga ni nyota ya hadhi tano. Kila shabiki wa Mpira angetamani kila siku timu yake icheze k**a hivi. Bonge moja la Fainali.

HONGERA sana Yanga kwa kutwaa Mara tatu mfululizo .

02/04/2024

🚨 Kikosi cha Yanga SC kilichoondoka leo Alfajiri kuwafata Mamelodi Sundowns 🇿🇦

Goalkeepers ;

01 ◉ Djigui Diarra 🇲🇱
02 ◉ Aboutwalib Mshery 🇹🇿
03 ◉ Metacha Mnata 🇹🇿

Centre-defenders ;

04 ◉ Bakari Mwamnyeto 🇹🇿
05 ◉ Ibrahim Bacca 🇹🇿
06 ◉ Gift Fred 🇺🇬
07 ◉ Dickson Job 🇹🇿

Wing-backs ;

08 ◉ Yao Attohoula Kouassi 🇨🇮
09 ◉ Nickson Kibabage 🇹🇿
10 ◉ Joyce Lomalisa 🇨🇩
11 ◉ Kibwana Shomari 🇹🇿

Centre-Midfielders

12 ◉ Khalid Aucho 🇺🇬
13 ◉ Zawadi Mauya 🇹🇿
14 ◉ Salum Abubakar 🇹🇿
15 ◉ Jonas Mkude 🇹🇿
16 ◉ Mudathir Yahya 🇹🇿

Attacking-Midfielders

17 ◉ Maxi Nzengeli 🇨🇩
18 ◉ Pacome Peodoh Zouzoua 🇨🇮
19 ◉ Stephane Aziz Ki 🇧🇫
20 ◉ Augustine Okrah 🇬🇭
21 ◉ Mahlatse Skudu Makudubela 🇿🇦
22 ◉ Farid M***a 🇹🇿
23 ◉ Denis Nkane 🇹🇿

Strikers ;

24 ◉ Clement Mzize 🇹🇿
25 ◉ Joseph Guede 🇨🇮
26 ◉ Kennedy Musonda 🇿🇲

⏩Kikiwa Jijini Cairo, Misri, Kikosi Cha Timu ya Wananchi Kinaendelea Na Mazoezi Kujiandaa Na Mchezo wa Ligi ya Mabingwa ...
01/03/2024

⏩Kikiwa Jijini Cairo, Misri, Kikosi Cha Timu ya Wananchi Kinaendelea Na Mazoezi Kujiandaa Na Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Dhidi ya Al Ahly wa Kukamilisha Hatua Ya Makundi

... 🔪 𝙆𝙄𝘾𝙃𝘼𝙆𝘼 𝙆𝙄𝙈𝙀𝙁𝙔𝙀𝙆𝙒𝘼Binafsi sikuona ulazima wa klabu ya Simba SC kuizungumzia Yanga SC mbele ya wanahabari na kupost...
26/02/2024

... 🔪 𝙆𝙄𝘾𝙃𝘼𝙆𝘼 𝙆𝙄𝙈𝙀𝙁𝙔𝙀𝙆𝙒𝘼

Binafsi sikuona ulazima wa klabu ya Simba SC kuizungumzia Yanga SC mbele ya wanahabari na kupost kwenye kurasa zao rasmi...
.. Badala yake wangezungumzia mambo yanayohusu Simba SC pekee kuelekea mechi muhimu ya kufuzu robo fainali dhidi ya Jwaneng kwa sababu kauli hizi zinawatoa mashabiki wa Simba, wanahabari na wadau katika lengo mama la mkutano huo na kuanza kujadili Yanga SC... Agenda ya mkutano ilikuwa Jwaneng, mashabiki kujitokeze lakini kwa sasa katika platform zote inazungumzwa Yanga SC. Wamewapa Yanga Airtime ya bure bila kulipia.

𝙉𝙪𝙠𝙪𝙪 ;

“Kufuzu kwa Yanga SC katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Mo Dewji na wa pili ni Simba SC. Wakati Mo Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua. Baada ya miaka 5 ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza ya Yanga wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi.”

©️ Ahmed Ally
Meneja wa habari Simba SC
____________________________

Kauli hizi zinatoa tafsiri nyingi, hii ni miongoni mwa hizo nyingi ;

𝙒𝙞𝙫𝙪 & 𝙈𝙖𝙪𝙢𝙞𝙫𝙪 ;

Kitendo cha Yanga SC kuingia robo fainali CAF-CL tukio hilo limefyeka kichaka kilichotumika kujifichia kwamba "Yanga hawajawahi kuingia robo fainali". Kichaka hicho kilitumika kwa miaka mingi kudharau mafanikio makubwa ya Yanga SC hata walipofika FAINALI CAF-CC, kuwa na makombe mengi ya ligi kuu (29) nk .. kinapofyekwa kichaka ulichozoea kujifichia k**a 'defensive mechanism' lazima UUMIE (𝙈𝙖𝙪𝙢𝙞𝙫𝙪) na uone WIVU (𝙒𝙞𝙫𝙪).

🇹🇿 Klabu ya kwanza Tanzania kucheza group stage CAF-CL & CC ni Yanga SC. Haya waliyafanya kipindi Mo Dewji akiwa hafikiriwi k**a atakuja kuwekeza Simba SC. Mo Dewji ashukuriwe pia ?!

Mo Dewji alikuja Simba kipindi ambacho Yusuph Manji anaondoka Yanga (2018) baada ya kutawala soka la Tanzania akiwa kwenye mchakato wa kufanya Mabadiliko kutoka kuwa Yanga asili kuwa kampuni ili klabu iifanye vizuri kimataifa that's why Yanga aliingia group stage CAF-CC mara 2 katika misimu (3). Sababu ya kuondoka inafahamika.

Kuondoka kwa Manji ilikuwa ni fursa kwa Mo Dewji kutawala soka la Tanzania na kujikita kwenye lengo alilolihubiri Manji (Kufanya vizuri kimataifa) akafanikiwa huku wenzao Yanga wakirudi nyuma (Bakuli).

Ujio wa (GSM) ulikuja kuendeleza ndoto ya Yusuph Manji na Yanga SC Kufanya vizuri kimataifa na kwa 70% wanaelekea kufanikiwa.

Kusema Yanga SC wameingia robo fainali wakushukuriwa ni Mo Dewji na Simba ni kauli iliyojaa WIVU, MAUMIVU na DHARAU.

Yanga imejihakikishia kuvuna Dola 900,000 (zaidi ya Sh2.3 bilioni) kwa kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa AfrikaMabin...
26/02/2024

Yanga imejihakikishia kuvuna Dola 900,000 (zaidi ya Sh2.3 bilioni) kwa kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wamefuzu hatua hiyo baada ya juzi kuichapa CR Belouizdad mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam

Wananchi walisubiri miaka 25 kutinga hatua ya makundi na sasa wanafurahia mafanikio makubwa zaidi

Mkakati wa Yanga sasa ni kuvuka robo fainali na pengine kuweka rekodi ya kipekee katika mashindano ya CAF msimu huu

K**a Yanga itafanikiwa kutinga nusu fainali basi dau litaongezeka hadi kufikia Sh3.1 bilioni huku ikifanikiwa kutinga fainali itavuna Sh5.1 bilioni. K**a itaibuka na ubingwa itavuna zaidi ya Sh10.2 bilioni

26/02/2024

Just woooh!!!!

... 🛬 𝙆𝙐𝙀𝙇𝙀𝙆𝙀𝘼 𝙍𝙊𝘽𝙊 𝙁𝘼𝙄𝙉𝘼𝙇𝙄Mpaka sasa bado timu (2) hazijafuzu robo fainali CAF-CL kukamilisha timu nane (8).𝙂𝙧𝙤𝙪𝙥 (A)1....
26/02/2024

... 🛬 𝙆𝙐𝙀𝙇𝙀𝙆𝙀𝘼 𝙍𝙊𝘽𝙊 𝙁𝘼𝙄𝙉𝘼𝙇𝙄

Mpaka sasa bado timu (2) hazijafuzu robo fainali CAF-CL kukamilisha timu nane (8).

𝙂𝙧𝙤𝙪𝙥 (A)

1. 🅿️ 10 — TP Mazembe 🇨🇩 ☑️
2. 🅿️ 10 — Mamelodi 🇿🇦 ☑️
3. 🅿️ 04 — Nouadhibou 🇲🇷
4. 🅿️ 04 — Pyramids 🇪🇬

𝙂𝙧𝙤𝙪𝙥 (B)

1. 🅿️ 11 — ASEC Mimosas 🇨🇮 ☑️
2. 🅿️ 06 — Simba SC 🇹🇿
3. 🅿️ 06 — Wydad Athletic 🇲🇦
4. 🅿️ 04 — Jwaneng Galaxy 🇧🇼

𝙂𝙧𝙤𝙪𝙥 (C)

1. 🅿️ 09 — Petro Atletico 🇦🇴 ☑️
2. 🅿️ 08 — Esperance 🇹🇳
3. 🅿️ 05 — Al-Hilal 🇸🇩
4. 🅿️ 04 — Etoile du Sahel 🇹🇳

𝙂𝙧𝙤𝙪𝙥 (D)

1. 🅿️ 09 — Al-Ahly 🇪🇬 ☑️
2. 🅿️ 08 — Young Africans 🇹🇿 ☑️
3. 🅿️ 05 — CR Belouizdad 🇩🇿
4. 🅿️ 04 — Medeama 🇬🇭

Timu zilizofuzu mpaka sasa ;

1. 🇹🇿 Young Africans SC
2. 🇪🇬 TP Mazembe
3. 🇿🇦 Mamelodi Sundowns
4. 🇨🇮 ASEC Mimosas
5. 🇦🇴 Petro Atletico
6. 🇪🇬 Al-Ahly Cairo
7. ____________________
8. ___________________

📌 K**a msimamo wa makundi ukibaki k**a ulivyo Yanga SC watakutana na moja ya timu hizi hatua ya Robo fainali CAF-CL.

🇨🇩 TP Mazembe
🇨🇮 ASEC Mimosas
🇦🇴 Petro Atletico

Note : Yanga wanaongoza kwa idadi ya mabao ligi kuu 🇹🇿, lakini pia mpaka sasa wanaongoza kwa mabao ya kufunga kwenye group stage CAF-CL katika magroup yote.

Address


Telephone

+255625900157

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbabu Yanga news & Apdate posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mbabu Yanga news & Apdate:

Shortcuts

  • Address
  • Telephone
  • Alerts
  • Contact The Business
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share