21/04/2023
KWANINI WAHINDI WALIOPANGA KARIAKOO/UPANGA WANAMILIKI UCHUMI.
Jifunze Mambo Saba 07. Kutoka kwa Wahindi na Ukuze Biashara yako.
*01. Hawajengi na kuacha pesa iwe kwenye biashara.*
- Maisha ni kupanga na kuchagua, unaweza kujenga, ukanunua magari.
- Wahindi wao wanaishi kwenye nyumba za kupanga ili mpunga wao ufanye kazi nyingine.
*02. Nyumba sio asset ni libality.*
Huu ni mjadala mkubwa sana.
Nyumba ya kupangisha (rentals) ni asset – Ni nyumba ya biashara.
Nyumba ya kuishi ni liability – You can choose what to belive.
- No wonder, Wahindi wengi huwaoni wakikimbia kwenda kujenga...
Kwenye maisha jambo la msingi ni kuzalisha pesa.
- Sasa k**a unaweza kufanya biashara ikalipa maradufu, kwa nini ukazike pesa kwenye nyumba ya kuishi?
*03. Wanapanga karibu na sehemu ya biashara ili wasitumie nauli.*
Wahindi wanaishi mjini.
Hawapandi magari na kulipa nauli, wanatembea. Akili Mtu wangu
- Wanatumia scooter kutembelea mjini, Sio kwamba hawana magari, wanayo.
Lakini tabia zao ni kukata costs za maisha kadri iwezekanvyo.
*04. Wanaishi karibu na sehemu ya biashara ili wasinunue chakula.*
Wanakula chakula cha kupika nyumbani.
Ukiishi karibu na kwako hii ndo faida.
- ukilipa 10K ya chakula kila siku, kwa mwezi ni 300K.
- Wazeiya wanakula nyumbani ili kusev costs.
- Ndo maana wanaishi karibu na kazini.
*05. Wanaishi karibu na biashara ili wasipoteze muda mwingi njiani.*
Kuna gharama kubwa unaingia kwa kukaa saa 2 njiani ukienda kazini.
Unaweza kuona ni kawaida lakini unapoteza muda mwingi sana.
Saa 2 kwenda na kurudi kwa siku = saa 4, wiki = saa 28, mwezi = saa 112...
*06. Hawakai mbali kuepuka kununua magari makubwa ya kwendea kazini.*
Mtu anaishi kibaha, anatumia pesa nyingi kuweka mafuta ya gari kwenda kazini.
Mhindi yeye anataka kutembea kwa miguu tu. Au basi anunue scooter ya kuzungukia mjini tu.
*07. Wanakaa mjini karibu na huduma zote muhimu.*
Ukiishi mjini unaokoa nauli nyingi za kwenda kupata huduma sehemu mbalimbali.
-Hospitali zipo karibu.
- Masoko yapo karibu.
- Ofisi za umma zipo karibu.
- Shule zipo karibu.
Unaokoa mengi kwa kuishi mjini.
Tumia Mbinu hizi za Wahindi Kibiashara 😂😂
📱 0758 672 833