Casa

Casa MEDIA

Mshereheshaji na mchekeshaji maarufu, Emmanuel Mathias anayejulikana k**a MC Pilipili amefariki dunia leo Novemba 16,202...
16/11/2025

Mshereheshaji na mchekeshaji maarufu, Emmanuel Mathias anayejulikana k**a MC Pilipili amefariki dunia leo Novemba 16,2025.

Taarifa zinaeleza kuwa, MC Pilipili alisafiri kuelekea jijini Dodoma ambapo jioni ya leo alitarajiwa kwenda kufanya kazi yake ya ushereheshaji jijini humo, lakini akafikvwa na mauti

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya General, Dodoma, Ernest Ibenzi ambaye amethibitisha taarifa hizo na kueleza kuwa MC Pilipili amefikishwa hospitalini hapo akiwa tayari amefariki dunia.

Msiba huu mzito umewashtua na kuwagusa wengi, ikiwemo mashabiki, wasanii wenzake na wadau wa tasnia ya burudani ambao wameendelea kuonyesha masikitiko kupitia mitandao ya kijamii.

Mabingwa wa soka wa Tanzania Yanga imepangwa Kundi B la hatua ya Makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika na mi...
03/11/2025

Mabingwa wa soka wa Tanzania Yanga imepangwa Kundi B la hatua ya Makundi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika na miamba ya soka Afrika Ahly ya Misri.

Mbali ya Al Ahly, timu nyingine ambazo imepangwa nazo katika Droo iliyofanyika leo Mjini Cairo, Misri ni ASFAR ya Morocco na JS Kabylie ya Algeria.

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imepangwa Kundi D katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa 2025/202...
03/11/2025

Klabu ya Simba SC ya Tanzania imepangwa Kundi D katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa 2025/2026, droo iliyofanyika leo mchana mjini Cairo, Misri.

Simba sc watakuwa na kazi kubwa mbele yao baada ya kupangwa kundi moja na miamba ya soka barani Afrika Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia, Atlético Petróleos de Luanda ya Angola, na Stade Malien ya Mali.

29/10/2025

Wananchi wamechoma masanduku ya kura

29/10/2025

Soweto mbeya Hali ilivyo muda huu

29/10/2025

Update maandamano yanayoendelea Tanzania

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemk**ata na linamuhoji, Jenifer Bilikwiza Jovin (Niffer) (26) mkazi Ma...
27/10/2025

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemk**ata na linamuhoji, Jenifer Bilikwiza Jovin (Niffer) (26) mkazi Masaki Peninsula, Kinondoni kwa tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, hasa siku za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.

Jeshi hilo limemk**ata Jenifer Tarehe 27,10.2025 majira ya saa 9 mchana eneo la Sinza Kumekucha ambapo wamesema hatua zaidi za kisheria zinaendelea kuzingatiwa dhidi ya mtuhumiwa huyo.

Taifa la Tanzania 🇹🇿 Kwa mara ya kwanza katika history ya mashindano ya CAF Interclub linafakiwa kuingiza makundi timu n...
26/10/2025

Taifa la Tanzania 🇹🇿 Kwa mara ya kwanza katika history ya mashindano ya CAF Interclub linafakiwa kuingiza makundi timu nne.

Tangu mashindano ya CAF Champions League pamoja na CAF Confederation Cup yaanzishwe , Tanzania haikuwahi peleka timu 4 makundi,awamu hii ndio imetemgenezwa history hii kubwa ambayo haikuwahi kutokea ndani ya taifa la Tanzania.

Young Africans Sports Club 🔰 pamoja na Simba Sports Club 🦁 wamefuzu kucheza hatua ya makundi kwenye mashindano ya CAF Champions League.

Azam FC pamoja na Singida Black Stars wao wamefanikiwa kufuzu kucheza makundi ya CAF Confederation Cup, pongezi Kwa vilabu vyote vilivyofanikiwa kufuzu kucheza mashindano hayo makubwa barani Afrika,ngazi za vilabu..

Klabu ya Yanga Sc imemtangaza Kocha Pedro Gonçalves (49) 🇵🇹  kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans 🇹🇿 Pedro amerithi mikoba ...
25/10/2025

Klabu ya Yanga Sc imemtangaza Kocha Pedro Gonçalves (49) 🇵🇹 kuwa Kocha Mkuu wa Young Africans 🇹🇿

Pedro amerithi mikoba ya Kocha Romain Folz aliyeachana na klabu ya YANGA Siku chache zilizopita.

Klabu ya Azam imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21...
24/10/2025

Klabu ya Azam imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004. Klabu hiyo imefuzu baada ya kuifunga KMKM FC ya Zanzibar magoli 7-0.

Azam FC wameweka rekodi ya kufuzu hatua ya makundi shirikisho kwa kufunga jumla ya magoli 9 baada ya kushinda mchezo wa mkondo wa kwanza magoli 2-0 Uwanja wa New Amaan. Wafungaji Japhet Kitambala (2), Iddy Seleman (2), Abdul Suleiman 'SOPU' (2) pamoja na Paschal Msindo goli moja (1).

Kocha Florentine Ibenge ameweka rekodi ya kuwa Kocha wa kwanza kuwapeleka Azam Fc hatua ya makundi, Pascal Msindo katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya KMKM aliweka rekodi ya kufunga goli lake la kwanza katika michuano hii ya CAFCC.

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imeahirisha Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa (CHADEMA...
24/10/2025

Mahak**a Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es Salaam imeahirisha Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa (CHADEMA), Tundu Lissu hadi Novemba 3, 2025, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuendelea kutokana na kukosekana kwa Shahidi.

Wakili wa Serikali Mkuu Renatus Mkude aliieleza Mahak**a kuwa upande wa Jamhuri ulikuwa tayari umeshatoa ushahidi kupitia mashahidi watatu, lakini shahidi wa tatu, Mkaguzi wa Polisi na Mtaalamu wa Uchunguzi wa Kielektroniki Samwel Kaaya, alishindwa kuwasilisha vielelezo vyake vya flash disk na memory card baada ya Mahak**a kukataa kuvipokea.

“Kwa sasa hatuna shahidi mwingine aliye tayari kutoa ushahidi kwa kuwa waliopangwa wanatoka nje ya Dar es Salaam na wanahitaji maandalizi zaidi. Kwa mujibu wa kifungu cha 302 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), tunaomba ahirisho,” alisema Mkude.

Kwa mujibu wa Wakili huyo wa Serikali, tarehe 3 Novemba 2025 ilikuwa tayari imepangwa katika ratiba ya kesi hiyo, hivyo aliomba shauri hilo liendelee siku hiyo.

Hata hivyo, Lissu alipinga ombi hilo la kuahirishwa akidai kuwa sababu zilizotolewa na upande wa Jamhuri hazina msingi wa kisheria.

Kutokana na hatua hiyo, Jaji Ndunguru, alisema Mahak**a imezingatia hoja za pande zote mbili na kubaini kuwa ombi la kuahirisha lina msingi wa kisheria kwa kuwa upande wa mashtaka haujawahi kukosa shahidi tangu shauri lianze, hivyo kesi inaahirishwa hadi Novemba 3, 2025.

23/10/2025

Treni ya Mwendokasi (SGR) imeripotiwa kuacha njia yake na kupata ajali katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo ikiwa inatokea Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma ambapo Abiria wawili walioongea na casamedia wamesema hawajamuona yeyote aliyejeruhiwa isipokuwa ni hofu tu iliyowapata wachache.

"Haijafahamika chanzo ila treni imehama kwenye reli k**a inavyoonekana kwenye video na picha, hatujaambiwa chochote ila kuna Viongozi na Maaskari wameanza kufika hapa sio mbali na hapa Stesheni Ruvu" - amesema mmoja wa Abiria hao.

Msemaji wa Shirika la Reli (TRC) Fredy Mwanjala akizungumza kwa njia ya simu, amekiri kupokea taarifa za ajali hiyo ambapo tumemnukuu akisema “tumepokea hizo taarifa za Treni kupata ajali na kwa kuwa ndio kwanza tumezipata kwa sasa Mkurugenzi Mkuu na Katibu Mkuu wa Wizara wote tunaelekea eneo la tukio na tunatoa taarifa baadae baada ya kufanya tathmini ya kina na Wataalamu”

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Casa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share