Bongo Simulizi

  • Home
  • Bongo Simulizi

Bongo Simulizi Karibu kwenye dunia ya simulizi za kutisha!
(3)

Hapa utapata hadithi za kutisha, za kichawi, simulizi za maisha, mapenzi yenye drama, na matukio ya kushtua yanayokufanya ushike pumzi hadi mwisho.

Kulikuwa na mwanamke mmoja aliyempenda mwanaume wa chuo kwa moyo wake wote. Alijitoa kwa kila hali: alimsaidia pesa za c...
14/05/2026

Kulikuwa na mwanamke mmoja aliyempenda mwanaume wa chuo kwa moyo wake wote. Alijitoa kwa kila hali: alimsaidia pesa za chakula, ada, na hata kumfariji wakati alipokuwa na shida. Upendo wake ulikuwa wa kweli na wa kujitolea, bila kutarajia malipo.

Baadaye, alipata ujauzito kutokana na uhusiano wao. Lakini mwanaume yule, ambaye hapo awali alifurahia msaada wake, ghafla akabadilika na kusema:
Siko tayari kuwa baba. Huo ujauzito siwezi kuubeba.

Mwanamke yule akaumia sana, lakini akaamua kubeba jukumu peke yake. Alijifungua mtoto, lakini mtoto alizaliwa na changamoto ya mikono isiyofanya kazi vizuri.

Mwanaume alipokuja kumuona mtoto, akasema kwa ukali na kukataa kabisa:
Huyu mtoto si wangu wa kumlea. Siwezi kuhusika na maisha ya namna hii.

Kisha akawaacha mama na mtoto bila msaada.

Mwanamke hakukata tamaa. Alimlea mtoto wake kwa upendo, uvumilivu na maombi mengi, akipambana na maisha peke yake. Miaka ilivyopita, mtoto alipata matibabu na hali yake ikaanza kuboreka hadi akapona kabisa.

Mtoto huyo, akiwa amekua na akili na bidii kubwa, alifanikiwa sana maishani hadi kuwa mfanyabiashara mkubwa na tajiri, akisaidia watu wengi wenye changamoto k**a yake.

Siku moja, baba yake wa damu alikuja bila kujua, akitafuta msaada kwa maisha yake yaliyokuwa yameanguka. Alipoletwa mbele ya mmiliki wa kampuni, alishtuka kumkuta yule mtoto aliyemkataa zamani akiwa ameketi kwenye nafasi ya uongozi.

Mwanamke akamwambia kwa utulivu:
Upendo wangu haukushindwa na mateso. Nilijenga maisha ya mtoto huyu hata ulipomkataa wewe.

Funzo la maisha:
Usikatae wajibu kwa sababu ya hali ngumu. Na usimdharau mtu kwa changamoto zake za leo—maumivu ya leo yanaweza kuwa ushindi mkubwa wa kesho.

Mwalimu mkuu wa shule moja ya gharama alisimama getini akiwa amekunja mikono yake kwa ukali. Mbele yake, alikuwa kijana ...
14/05/2026

Mwalimu mkuu wa shule moja ya gharama alisimama getini akiwa amekunja mikono yake kwa ukali. Mbele yake, alikuwa kijana mdogo na wazazi wake waliokuwa wamechoka, wakimsihi mwalimu huyo amruhusu mtoto wao aingie darasani kwani walikuwa wamepungukiwa nusu ya ada ya shule.
​Mwalimu yule, kwa kiburi na dharau, aliwatazama wazazi wale na kusema: "Hapa siyo kituo cha kutoa misaada! K**a hamna pesa, mumuondoe huyu mwanafunzi hapa kizembe. Bora mumutume mwanenu aokote makopo mitaani, hapa hakuna nafasi ya maskini!"
​Wazazi wale walishusha vichwa chini kwa unyonge, wakashika mikono ya mtoto wao na kuondoka huku wakilia kwa dhalili hiyo mbele ya watu.

Miaka 20 iliyopita, mwalimu yule aliyekuwa sasa amezeeka na kufilisika baada ya shule yake kufungwa, alikuwa amekaa kando ya barabara akisubiri msaada wa matibabu. Gari moja la kifahari lilisimama, na akashuka mwanamume mtanashati ambaye ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa hospitali ile kubwa ya kanda.
​Mwanamume yule alimtazama mwalimu na kusema: "Mwalimu, unanikumbuka? Mimi ndiye yule mtoto uliyemwambia aende akaokote makopo kwa sababu ya ada. Wazazi wangu walinipeleka kuokota hayo makopo kweli, wakayauza kwa miaka mingi ili nipate elimu. Yale makopo uliyodhani ni uchafu, ndiyo yaliyonijengea uwezo wa leo kuwa daktari na mmiliki wa hospitali hii unayohitaji msaada."
​Mwalimu alishindwa hata kuinua uso wake, akijuta kwa maneno ya dharau aliyowahi kuyatoa kwa watu waliokuwa wakipambana na hali yao.

​Hii Ni funzo zito:

Walimu, msiwadhalilishe wanafunzi wala wazazi wao kwa sababu ya umaskini. Mtoto anayeshindwa kulipa ada leo anaweza kuwa mtu mkubwa wa kusaidia jami kesho. Elimu ya kweli hujengwa kwa hekima, huruma na heshima, si kwa maneno ya kuumiza mioyo.
Na kwa wazazi wanaopitia hali ngumu, msikate tamaa. Kila jasho na kila sacrifice mnayofanya kwa ajili ya watoto wenu lina thamani kubwa mbele ya Mungu. Endeleeni kupambana, maana kesho ya watoto wenu inaweza kubadilisha historia ya familia yenu.

Binti mmoja, akiwa amependeza sana katika vazi lake la mahafali (graduation), alikuwa amezungukwa na marafiki zake mataj...
14/05/2026

Binti mmoja, akiwa amependeza sana katika vazi lake la mahafali (graduation), alikuwa amezungukwa na marafiki zake matajiri huku wakipiga picha za furaha chuoni. Furaha na harufu ya marashi ya thamani vilijaa hewani. Ghafla, alitokea mzee mmoja akiwa amevaa ovaroli lililochakaa na kuanza kumshangilia kwa mbali akisema, "Hongera mwanangu! Umeifanya familia ijivunie!"
​Binti huyo, kwa kuona haya na dharau kubwa mbele ya marafiki zake, alimfuata yule mzee na kumpiga mkono mkali wa kumkataa, huku akiziba pua kwa ishara ya karaha: "Ona unavyonuka! Unanidhalilisha mbele ya marafiki zangu na uvundo wako wa maji taka. Usijaribu kunifuata tena hapa chuoni, mimi sikutambui!"
​Yule mzee alinyamaza, machozi yakimlenga na kumtoka waziwazi. Alishika mfuko wake wa plastiki uliokuwa na zawadi ndogo ya maua, kisha akageuka na kuondoka kimyakimya huku akichechemea, akiuacha upendo wake ukiwa umekataliwa.

​Binti huyo hajui kuwa harufu anayoikimbia leo ndiyo iliyompa yeye heshima ya kuitwa "Msomi". Kwa miaka minne, baba yake alikuwa anaingia kwenye mashimo ya maji taka (vyoo vya kunyonya), akibeba kinyesi cha watu usiku kucha ili apate pesa ya kumlipia binti huyo ada ya shule.
​Wazazi hutoa miili na nguvu zao k**a sadaka ili watoto wao wapendeze na wasome. Kila tone la jasho na uvundo uliomjaa baba yake, ndivyo vilivyotengeneza marashi na nguo za thamani ambazo binti huyo anazitumia leo kujivunia. Baba alikubali kuitwa "Mchafu" na jamii, ili mwanawe aitwe "Daktari" au "Mwalimu".
​Leo binti anaona aibu kutambulika na mtu aliyekuwa tayari kugusa uchafu ili yeye aishi maisha safi.

​Hii Ni Funzo Zito:
​Usidharau mtu yeyote, hasa mzazi wako, bila kujali hali yake ya maisha. Hakuna kazi inayodhalilisha duniani k**a haina haramu. Aibu kubwa si kuwa na mzazi anayefanya kazi duni, bali aibu kubwa ni kumdharau yule aliyetoa utu wake ili wewe upate thamani.

Askari mmoja, kwa kiburi cha cheo chake, anampiga teke mama mzee aliyekuwa akiuza matunda kando ya barabara. Bidhaa za m...
13/05/2026

Askari mmoja, kwa kiburi cha cheo chake, anampiga teke mama mzee aliyekuwa akiuza matunda kando ya barabara. Bidhaa za mama huyo zinasambaa kila mahali. Askari huyo anamfokea mama huyo kwa dharau, huku akikejeli hata kovu la moto lililo mkononi mwa mama huyo: "Angalia hata ngozi yako ilivyoharibika, unanichafulia mji na takataka zako!
​Ukweli mchungu:
Askari huyo hajui kuwa kovu lile la moto mkononi mwa mama huyo ndilo linalomfanya yeye awe hai leo. Miaka mingi iliyopita, wakati askari huyu akiwa mtoto mdogo ndani ya nyumba iliyokuwa ikiungua moto, mama huyo mpitaji wa njia, alijitolea maisha yake, akaingia kwenye moto ule na kumwokoa. Alipata kovu lile ili mtoto yule ambae ni Askari leo apone.

Leo askari anamdharau yule aliyetoa maisha yake kwa ajili yake.

Hii Ni funzo zito: Usidharau mtu yeyote, bila kujali hali yake ya maisha. Hujui ni nani aliyewahi kuwa nguzo ya maisha yako wakati ukiwa mnyonge. Cheo ni dhamana, lakini utu ni kitu cha thamani zaidi.

Ndugu zangu samaani, Kuna changamoto kidogo, Ndio mahana tuna chelewa kutoa next part ya Ndoa kifo.
12/05/2026

Ndugu zangu samaani, Kuna changamoto kidogo, Ndio mahana tuna chelewa kutoa next part ya Ndoa kifo.

Snake Boy: huu dada Alizani amependwa
12/05/2026

Snake Boy: huu dada Alizani amependwa

Hii ni simulizi gani jamen?
12/05/2026

Hii ni simulizi gani jamen?

Uruma yake Ndio mwanzo yamateso yake.K**a unajuwa jina ya simulizi hii weka comment 🙏
12/05/2026

Uruma yake Ndio mwanzo yamateso yake.
K**a unajuwa jina ya simulizi hii weka comment 🙏

Mary aliendelea kupokea zawadi kutoka kwa ALLY.  Swali kwa wanadada wote. Je, unaweza kumkataa mwanaume ambaye nakupa pe...
11/05/2026

Mary aliendelea kupokea zawadi kutoka kwa ALLY. Swali kwa wanadada wote. Je, unaweza kumkataa mwanaume ambaye nakupa pesa na zawadi mbalimbali kila Siku ?

Katika kila hatua, neno la Mungu ndio mwongozo wetu. Nikiwa na timu yangu hapa, tunawaombea baraka tele. Mungu awafungul...
10/05/2026

Katika kila hatua, neno la Mungu ndio mwongozo wetu. Nikiwa na timu yangu hapa, tunawaombea baraka tele. Mungu awafungulie milango ya heri na amani katika kila jambo mnalofanya.
​Que la grâce de Dieu vous accompagne ce soir. Merci d'être une communauté si fidèle. Mungu awabariki sana! 🙏

Ndoa kifo Part 5:​Safari yetu inaendelea, lakini hali imekuwa tete sana. Mama yake Mary ni mgonjwa sana na anateseka kwa...
10/05/2026

Ndoa kifo Part 5:

​Safari yetu inaendelea, lakini hali imekuwa tete sana. Mama yake Mary ni mgonjwa sana na anateseka kwa maumivu makali kitandani. Kila anayemtazama anabaki na maswali mengi moyoni mwake.

​JE, UNAHISI NINI KIMESABABISHA UGONJWA HUU?
​Nataka kusikia maoni yako wewe mdau wa Ndoa Kifo:

Unahisi ni nani au ni kitu gani kiko nyuma ya ugonjwa huu?
​Dondosha comment yako hapa chini 👇. Mawazo yenu ni muhimu sana kabla ya kuachia Part 5!

Address

Kalangalala

30101

Telephone

+255682711910

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bongo Simulizi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Bongo Simulizi:

  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share