Machinga Tv

Machinga Tv 𝗛𝗮𝗯𝗮𝗿𝗶 | 𝗘𝗹𝗶𝗺𝘂 | 𝗕𝘂𝗿𝘂𝗱𝗮𝗻𝗶。
Official Machinga Tv page.

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limepinga agizo la serikali, kuwataka wasichana waliopata mimba...
18/07/2025

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, limepinga agizo la serikali, kuwataka wasichana waliopata mimba kuendelea na masomo. Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki CENCO, limesema Shule zake hazitatekeleza agizo hilo la serikali.

Kupitia barua ya wazi, walioijibu serikali kupitia Wizara ya Elimu, Kanisa Katoliki ambalo lina Shule zaidi ya 18, 000 linasema, agizo hilo la serikali linakwenda kinyume na kanuni za kupata elimu nchini humo.

Aidha, Kanisa hilo linasema kuwaruhusu wasichana waliopata mimba kuendelea na masomo, wakiwa wajawazito, kutasababisha upotofu mkubwa wa maadili na nidhamu miongoni mwa wanafunzi.

Kanisa hilo linasisitiza kuwa halitakuwa tayari, kuwa na msichana mjazito darasani, na badala yake, watakaokuwa katika hali hiyo, watahamishiwa kwenye shule za serikali.

Mvutano huu unakuja wakati huu Katiba ya DRC, ikitoa usawa wa watu wote kupata elimu lakini kwa muda mrefu wasichana wajawazito wamekuwa wakitengwa na kuacha masomo.

18/07/2025

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na TANAPA na wananchi wa maeneo ya jirani, kuanzia tarehe 6 hadi 15 Julai, 2025 wamefanya operesheni mkoani Morogoro, hususan kwenye ushoroba kati ya Hifadhi za Taifa za Mikumi na Nyerere. Katika operesheni hiyo, ekari 614 za mashamba ya bangi ziliteketezwa, kilogramu 3,741.9 za bangi kavu na kilogramu 1,706 za mbegu za bangi zilik**atwa na kambi 72 za wakulima wa bangi zilisambaratishwa huku watuhumiwa tisa (9) wakik**atwa.

18/07/2025

Mafunzo ya siku tatu yaliyofanyika Geita Mjini kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutoka mikoa ya Geita na Kagera, washiriki wameelezwa kuhusu majukumu mapya waliyonayo kufuatia kuwepo kwa sheria mbili mpya za uchaguzi.

Sheria hizo ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024 pamoja na Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ya Mwaka 2024.

Akizungumza kwa niaba ya Mjumbe wa INEC, Mratibu wa Mafunzo Geita Mjini Mawazo Bikenye amesema kuwa sheria hizo mpya zimeongeza maeneo mapya ya utekelezaji ambayo hapo awali hayakuwapo kwenye sheria za zamani.

Amebainisha kuwa maeneo hayo ni pamoja na kushughulikia maombi ya watu wanaotaka kupiga kura nje ya vituo walivyojiandikisha, usimamizi wa kura zitakazopigwa magerezani.

Mafunzo hayo yaliyokutanisha washiriki 98 yamelenga kuhakikisha Maafisa wa Uchaguzi wanakuwa tayari kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo na maelekezo yote yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Yaliyojili kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ijumaa hii
18/07/2025

Yaliyojili kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania ijumaa hii

17/07/2025

Mwanasiasa mkongwe na mstaafu wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema yeye ni mwanachama wa kawaida na hivyo hana wajibu wa kuzungumzia msimamo wa chama chake wa 'No Reforms No Election'.

Mbowe aliyasema hayo leo Julai 17, 2025 jijini Dodoma baada ya kushiriki uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

17/07/2025

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kusalimiana na Freeman Mbowe, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA, katika uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika JKCC, Julai 2025.

17/07/2025

Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete wakati akitoa neno kwenye uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, jijini Dodoma alidokeza siri kuwa Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo kuna kipindi aliteleza kuondoka CCM.

17/07/2025

Mrembo anawashauri wanaume watafute wanawake wa hadhi yao itawasaidia kuona wanawake hawapendi hela.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mwalimu Dorosela Salvatory...
17/07/2025

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mwalimu Dorosela Salvatory (45), mkazi wa Manispaa ya Geita na mwalimu wa Shule ya Sekondari Nyanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, mtuhumiwa anayetuhumiwa kuhusika na tukio hilo ni Nickson Johson (54), ambaye pia ni mkazi wa Manispaa hiyo. Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa linamhoji mtuhumiwa huyo kuhusiana na mauaji hayo.

Mwili wa mwalimu Dorosela ulikutwa Julai 15, 2025 ndani ya nyumba yake iliyopo Mtaa wa Uwanja, Kata ya Nyankumbu, akiwa tayari amefariki dunia. Ripoti ya awali inaeleza kuwa marehemu alipatikana akiwa na majeraha ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, ishara kuwa alishambuliwa kwa ukatili mkubwa.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo na taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Aidha, Jeshi hilo limewataka wananchi waendelee kuwa watulivu na kutoa ushirikiano wakati uchunguzi ukiendelea. Wameeleza kuwa yeyote atakayebainika kuhusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

17/07/2025

Mwanamitandao na mwalimu, Jacki Mngoni, amemtetea msanii Dogo Patten baada ya kugoma kujibu maswali ya shule katika mahojiano, akieleza kuwa wasanii hawapaswi kufanya mahojiano bure.

Jacki amesema mahojiano huwapa changamoto wasanii, hasa wanapokumbwa na mashambulizi mitandaoni, hivyo ni haki yao kulipwa k**a kifuta jasho. Pia amekosoa baadhi ya wanahabari kwa kukosa taaluma ya uandishi na kushughulika na habari za udaku badala ya maendeleo ya taifa.

Kauli yake imeibua mjadala kuhusu thamani ya kazi ya wasanii na nafasi ya wanahabari katika kujenga jamii.

17/07/2025

Jeshi la Uhamiaji Mkoani Geita limewak**ata wahamiaji haramu kutoka nchi ya Burundi na Maenneo mengine wapatao 126 ambao tayari walikuwa wameishaingia ndani ya mkoa wa Geita huku wakieleza sababu mbalimbali zilizowafanya kuingia kinyume cha sheria.

Akizungumza na Wanadishi wa Habari Kamishina Msaidizi Mwandamizi , James Mwanjotile ambaye ni Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Geita amesema kuanzia robo ya Mwisho wa Mwaka wa Fedha kuanzia 2024/2025 kutoka April mpaka Juni 30 Mwaka huu tayari wameondosha takribani wahamiaji 593 .

Aidha Mwanjotile amesema wanaendelea na Oparesheni maalumu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola katika kuhakikisha wanaendelea kudhibiti raia wa Kigeni ambao wamekuwa wakiingia kinyume cha sheria ndani ya Mkoa wa Geita .

15/07/2025

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa rai kwa waratibu wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na wasimamizi wa Uchaguzi , Wasaidizi ngazi ya Jimbo , Maofisa Uchaguzi na Maofisa wanunuzi watakaokwenda kusimamia Uchaguzi Mkuu kuhakikisha wanafuata sheria na Kanuni za Uchaguzi pamoja na kutenda haki ili kuepukana na kuwa moja ya vyanzo vya Malalamiko kwa wanasiasa katika zoezi hilo la Uchaguzi Mkuu.

Rai hiyo imetolewa Mjini Geita na Mh.Jaji wa Mahak**a Kuu Tanzania ambaye pia Mjumbe wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Bi. Asina Omari wakati akifungua Mafunzo ya Siku Tatu kwa Maofisa 98 kutoka Mikoa miwili ikiwemo Mkoa wa Kagera pamoja na Mkoa wa Geita ambapo amewataka Maofisa hao kufuata miongozo itakayotolewa na Tume hiyo wakati wa Uchaguzi .

" Shirikisheni vyama vyote vya siasa vyenye Usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia Matakwa ya katiba sheria kanuni na Maelekezo mbalimbali ya Tume Mjiepushe kuwa vyanzo vya Malalamiko kutoka kwa vyama vya siasa na wadau wa Uchaguzi hakikisheni Mnazingatia Ipasavyo katiba sheria , Kanuni miongozo na Maelekezo mbalimbali yakiyotolewa na yatakayotolewa na Tume , " Jaji wa Mahak**a kuu ya Tanzania na Mjumbe wa (INEC) Bi. Asina Omari.

Aidha Jaji Asina amewataka Maofisa hao kuhakikisha Taarifa zote zinazohitaji ufafanuzi katika Zoezi la Uchaguzi zitolewe na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na si mtu Binafsi na kuwataka kusimamia viapo vyao katika kutunza siri na kujitoa au kutokuwa sehemu ya Chama cha Siasa katika kipindi chote cha Uchaguzi.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Machinga Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Address
  • Alerts
  • Claim ownership or report listing
  • Want your business to be the top-listed Media Company?

Share